Wakuu,
Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Ndani ya saa 72 zijazo mabadiliko haya yataonekana kwa wengi.
Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.
Thread hii itatumika
kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.
Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu
App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.
Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.
Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.
Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.
Asanteni sana!