Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Kuwe na option yakufuta thread, mkuu Melo fanyia kazi wazo hilo sio mnang’ang’ania nyuzi zetu kama msafu ama biblia!, La mwisho kabisa kuwa na member wa blue tiki na la nyongeza kabisa kuwa na kitufe cha kupiga ban mod yeyote atayezingua!
 
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Ndani ya saa 72 zijazo mabadiliko haya yataonekana kwa wengi.

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!
[emoji1545][emoji1545][emoji1534][emoji626]
 
Kuwe na option yakufuta thread,mkuu melo fanyia kazi wazo hilo sio mnang’ang’ania nyuzi zetu kama msafu ama biblia!,la mwisho kabisa kuwa na member wa blue tiki na la nyongeza kabisa kuwa na kitufe cha kupiga ban mod yeyote atayezingua!
Unataka tusibakie na record za uzi zako...
 
Ushauri wangu,wekeni option ya kumfanya member aweze kupewa warning kabla hajapigwa BAN ili ajue ajirekebishe vipi.

Wengi humu hawako comfortable na id zao wanazotumia sasa kutokana na walipigwa life ban Id zao za zamani kutokana mods kuhisi hisi watu hovyo,watu tunawasiliana PM kwa mambo ya maana siku mods wakiamka vibaya mtu anakula life ban ukihitaji urudi PM ktk acc yako kuangalia yale mliyoshauriana na member mwenzio uyafanyie kazi ktk maisha halisi huwezi tena ku-access chochote.

Ni ushauri tu nimetoa.
 
Tunaomba Kipengele cha Kupata Data Zetu kiwepo ndugu Maxence Melo kama Vile Twitter, Facebook na Social Media zingine zifanyavyo
 
Ndugu Max mimi naomba mniambie kwanini ni mimi peke yangu ndio napigwa Ban kila nikifuta Comments tena Ban zangu hua za kuanzia mwezi hadi miezi 7.

Why only me? Wakati sio mwenyewe ninaefuta michango. Kuna watu humu ni vinara wa kufuta Comments ila hawajawahi kupigwa ban ila mm nikifuta tu.. nakula ya miezi
Inauma sana😞😞😔😔
Screenshot_20220204-182724~2.png
Screenshot_20210413-104028~2.png
 
Ndugu Max mimi naomba mniambie kwanini ni mimi peke yangu ndio napigwa Ban kila nikifuta Comments tena Ban zangu hua za kuanzia mwezi hadi miezi 7. Why only me?? Wakati sio mwenyewe ninaefuta michango. Kuna watu humu ni vinara wa kufuta Comments ila hawajawahi kupigwa ban ila mm nikifuta tu.. nakula ya miezi
Inauma sana😞😞😔😔
View attachment 2239898View attachment 2239900
Hebu subiri kwanza ni kwamba comment uliyoiandika mwenyewe ukifuta ni kosa au maana sijaelewa hizo reasons hapo juu
 
Mbona mi sipati notification?

Kuna watu tunawablock ila bado wakianzisha mada twaona mada zao

Kwanini msiweke ukimtia mtu block usione mada yoyote anayoanzisha wala hata changizo zake zozote zile

Pia kwanini msituwekee uwezo wa kuzuia mada fulani, tusizione kabisa ie mada za kukashfu dini za wengine etc
Safi sana jitu Umeli Block bado unapata Mada zake za hovyo
 
Kuna jukwaa linaitwa jukwaa la wakubwa, naomba pamoja na mengine maboresho haya yaweke urahisi wa jukwaa hilo kufikika kirahisi, maana mpaka sasa sijajua wanaopaswa kushiriki kwenye hilo jukwaa wanatakiwa kuwa na vigezo gani.
 
Unataka tusibakie na record za uzi zako...

Haina maana kung’ang’ania nyuzi zetu hayo mambo ya kizamani sana hakuna application yeyote yenye mifumo ya kidikteta namna hii, sema ingekuwa ni vyema kila mwana jamii forum akachunguzwa vizuri kama hana mambo ya konakona anapewa blue tiki ili kuwatofautisha na matapeli matapeli uchwara hapa Jf, nadhani umenipata jafee!
 
Back
Top Bottom