TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Wanabodi,
nashauri jee tupige ndege wawili kwa jiwe moja?, au tuendelee kufanya chaguzi zetu kwa mazoea?
Ndege wa kwanza ni uchaguzi wa serikali za mitaa, usifanyike tena mwaka 2024 wala usisimamiwe tena na Tamisemi, na badala yake ufanyike mwaka 2025 pamoja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
Chaguzi hizi ni uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi Mkuu, na husimamiwa na Tamisemi, huku ndiko madudu ya ajabu ya ukiukwaji wa demokrasia kuanzia.
Chama kinachoshinda serikali za mitaa, ndicho chama kinachokuja kushinda uchaguzi Mkuu unaofuata. ni tufanye uchaguzi wote kwa siku moja, na kusimamiwa na Tume moja huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar wanaweza kufanya chaguzi 5 kwa siku moja, Tanzania hatuwezi kushindwa kufanya chaguzi 4 kwa siku moja!. Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 halafu uchaguzi Mkuu 2025, kwa sasa tufanye mabadiliko ya katiba na sheria, halafu 2025 tufanye chaguzi zote 4 kwa siku moja, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa.
Paskali
Naunga Mkono hoja!.Mimi nashauri uchaguzi wa serikali za mitaa usogezwe mpaka mwaka kesho na sheria ziwekwe vizuri. Wataalamu wengi wanasingizia muda wakati huo huo wanasema sheria zinahitaji kubadilishwa. Hivyo hakuna sababu ya kwenda kwenye uchaguzi ambao kwa ulivyo sasa utashusha na kupunguza uaminifu wa hata uchaguzi wa mwakani. Ingekuwa rahisi zaidi kama chaguzi za serikalli za mitaa na uchaguzi mkuu kuchanganywa. Nashauri kwa nia nzuri maana bila hivyo kuanzia mwisho wa uchaguzi huu ambao kwa sheria hizi utalalamikiwa kama ule uliopita tu.
Mwaliko ni umekosewa, ni kikao cha kutunga kanuni!.Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika amesema wamealikwa kwenye kikao Cha kupitia Kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa Lakini hawajapewa rasimu ya Kanuni Ili wazipitie na kikao ni June 15
Viongozi wanaomba ushauri wa wanachama katika Mazingira hayo wafanye nini?
Ayo tv
Mwaliko ni umekosewa, ni kikao cha kutunga kanuni!.Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika amesema wamealikwa kwenye kikao Cha kupitia Kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa Lakini hawajapewa rasimu ya Kanuni Ili wazipitie na kikao ni June 15
Viongozi wanaomba ushauri wa wanachama katika Mazingira hayo wafanye nini?
Ayo tv
Sasa hivi Urais sio lazima mtu awe na shahada??Waongeze vigezo vya washiriki katika hizi chaguzi.
Serikali za Mitaa iwe lazima mtu awe na Astashahada Kikomo cha miaka 5
Udiwani iwe lazima mtu awe na stashahada Kikomo cha Miaka 10
Ubunge iwe lazima Shahada, uwe na kikomo cha miaka 15
Urais iwe lazima mtu awe na Shahada
Hivyo vyote viwe kwenye vyuo vinavyotambulika na TCU
Wote lazima waandike mali walizo nazo na kuziweka hadharani kabla ya kupitishwa
Wagombea huru wawe
Viti maalumu waondolewe maana hawana msaada katika taifa
Majimbo ya Uchaguzi yawekwe kutokana na idadi ya watu angalau
Mkuu ndengisivilii ,karibu mitaa hiiKwa tume ipi kaka? wewe ni mdau ambae unatakiwa uanze kutoa makala kuhusu kuboreshwa kwa tume ya uchaguzi ili ipatikane tume huru ya uchaguzi, kuongea ukweli sio dhambi kaka.