Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?

Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?

Kumradhi mleta mada nimesoma heading ya uzi tu. Nitarudi baadaye kusoma bandiko zima. Lakini, nimeona kwanza nitoe maoni yangu haya:

Naona umuhimu wa kuongeza muda wa awamu kutoka miaka mitano kuwa miaka minane. Hii miaka mitano, inatuumiza ki-mali na ki-hali.
 
Wanabodi,
nashauri jee tupige ndege wawili kwa jiwe moja?, au tuendelee kufanya chaguzi zetu kwa mazoea?

Ndege wa kwanza ni uchaguzi wa serikali za mitaa, usifanyike tena mwaka 2024 wala usisimamiwe tena na Tamisemi, na badala yake ufanyike mwaka 2025 pamoja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Chaguzi hizi ni uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi Mkuu, na husimamiwa na Tamisemi, huku ndiko madudu ya ajabu ya ukiukwaji wa demokrasia kuanzia.

Chama kinachoshinda serikali za mitaa, ndicho chama kinachokuja kushinda uchaguzi Mkuu unaofuata. ni tufanye uchaguzi wote kwa siku moja, na kusimamiwa na Tume moja huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar wanaweza kufanya chaguzi 5 kwa siku moja, Tanzania hatuwezi kushindwa kufanya chaguzi 4 kwa siku moja!. Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!

Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 halafu uchaguzi Mkuu 2025, kwa sasa tufanye mabadiliko ya katiba na sheria, halafu 2025 tufanye chaguzi zote 4 kwa siku moja, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa.

Paskali
Mimi nashauri uchaguzi wa serikali za mitaa usogezwe mpaka mwaka kesho na sheria ziwekwe vizuri. Wataalamu wengi wanasingizia muda wakati huo huo wanasema sheria zinahitaji kubadilishwa. Hivyo hakuna sababu ya kwenda kwenye uchaguzi ambao kwa ulivyo sasa utashusha na kupunguza uaminifu wa hata uchaguzi wa mwakani. Ingekuwa rahisi zaidi kama chaguzi za serikalli za mitaa na uchaguzi mkuu kuchanganywa. Nashauri kwa nia nzuri maana bila hivyo kuanzia mwisho wa uchaguzi huu ambao kwa sheria hizi utalalamikiwa kama ule uliopita tu.
Naunga Mkono hoja!.
Nimetoa hoja kama hii mara mbili, Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana! kisha

Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?

Na sikuishia kuandika tuu jf, bali nimendikia makala
View attachment 2987132

Na kuisema wazi kwenye mikutano ya mapendekezo!.
View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=xTaadxXIHp2ExGXB

P
 
Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika amesema wamealikwa kwenye kikao Cha kupitia Kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa Lakini hawajapewa rasimu ya Kanuni Ili wazipitie na kikao ni June 15

Viongozi wanaomba ushauri wa wanachama katika Mazingira hayo wafanye nini?

Ayo tv
Mwaliko ni umekosewa, ni kikao cha kutunga kanuni!.
Ila nijuavyo mimi sheria mpya ya uchaguzi imeifuta sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, hivyo nawashauri Chadema wahudhurie na kuomba uchaguzi wa serikali za mitaa ufanywe mwakani na usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi kama nilivyo shauri hapa Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?

Na hapa Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!

Waongeze vigezo vya washiriki katika hizi chaguzi.

Serikali za Mitaa iwe lazima mtu awe na Astashahada Kikomo cha miaka 5

Udiwani iwe lazima mtu awe na stashahada Kikomo cha Miaka 10

Ubunge iwe lazima Shahada, uwe na kikomo cha miaka 15

Urais iwe lazima mtu awe na Shahada

Hivyo vyote viwe kwenye vyuo vinavyotambulika na TCU

Wote lazima waandike mali walizo nazo na kuziweka hadharani kabla ya kupitishwa

Wagombea huru wawe

Viti maalumu waondolewe maana hawana msaada katika taifa

Majimbo ya Uchaguzi yawekwe kutokana na idadi ya watu angalau
Sasa hivi Urais sio lazima mtu awe na shahada??
 
Back
Top Bottom