Wanabodi,
nashauri jee tupige ndege wawili kwa jiwe moja?, au tuendelee kufanya chaguzi zetu kwa mazoea?
Ndege wa kwanza ni uchaguzi wa serikali za mitaa, usifanyike tena mwaka 2024 wala usisimamiwe tena na Tamisemi, na badala yake ufanyike mwaka 2025 pamoja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
Chaguzi hizi ni uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi Mkuu, na husimamiwa na Tamisemi, huku ndiko madudu ya ajabu ya ukiukwaji wa demokrasia kuanzia.
Chama kinachoshinda serikali za mitaa, ndicho chama kinachokuja kushinda uchaguzi Mkuu unaofuata. ni tufanye uchaguzi wote kwa siku moja, na kusimamiwa na Tume moja huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar wanaweza kufanya chaguzi 5 kwa siku moja, Tanzania hatuwezi kushindwa kufanya chaguzi 4 kwa siku moja!.
Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 halafu uchaguzi Mkuu 2025, kwa sasa tufanye mabadiliko ya katiba na sheria, halafu 2025 tufanye chaguzi zote 4 kwa siku moja, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa.
Paskali