Jamani hii ni hujuma ya wazi kwa wamiliki wa mabasi;
Serikali sikivu ni ile inayotatua kero, Lakini Tunashangaa sana badala ya kutatua Zinazidishwa: HAIWEZEKANI
Mtakumbuka Enzi za mkurugenzi Kabwe aliyetumbuliwa na magufuli kwa ufisadi kupitia Stand,
Sitaki kugusia makando kando ya uendeshaji mbovu na ukosefu wa huduma mhimu stendi kuu.
HOJA MHIMU ni lini mabasi yalikuwa kero kusogeza huduma kwa wananchi?
Je, kama Wamiliki wa mabasi watakapoamua kuitafsiri kuwa hii fukuza fukuza mabasi mtaani ni hujuma dhidi ya SGR Ipate wateja WATAKUWA WAMEKOSEA?
Je, hatuoni tunahatarisha SGR nayo kuhujumiwa kama wenye mabasi wakiamua kujibu?
WENYE MABASI ni wafanya biashara, Wanamikopo bank wanadaiwa marejesho;
Wenye mabasi wamewekeza Brand na ujenzi wa ofisi zao kwa gharama kubwa zaidi bilioni za fedha ili kuweka mazingira rafiki kwa abiria kupumzika wakijiandaa na safari LEO ghafla unawaambia ONDOKENI pekekeni magari stendi hivi mnajua maumivu ya kuwekeza?
Mnataka abiria warudi kwenye gombea gombea stendi ili kulinda Vizimba na mapato ya stendi huku mkipuuza utu na staha za wananchi?
Mnataka mkafungie mabasi yote stendi ili muanze kuyaruhusu kutoka kwa muda maalum jamani zama zimebadilika, kwanini hamtaki kubadilika?
AU ILE KAULI YA MSAFIRI KAFIRI ndiyo bado inawatawala vichwani?
MNATAKA ABIRIA anaetoka/kwenda mkoani kwa gharama ya nauli ya 60k, Then Akishuka maghufuli, Alake wapi kama ni gesti hiyo gharama anapata wap, au kwenda kwake akodi bajaji 50k Au pengine
kupoteza mali zake kwa kuibiwa stend, ACHILIA MBALI Kero na usumbufu wa wakata tiketi, wabeba mizigo n.k
Mnataka abiria wakimbie kero hizo wakapande sgr, Je wenye mabasi mikopo watalipaje?
Yote 9 kwanza kwanini kujiamulia mambo ambayo si kero ndiyo mnayafanya kero?
Biashara ya mwendokas imewashinda na abiria wapo kibao.
MNAKAA KIKAO KUZUIA WAFANYA BIASHARA WATAOTAFTA ABIRIA MTAANI MBAONA NI SAWA?
VIONGOZI kwa hili mnazingua sana mnatia hasira sana kwetu wananchi tunatamani japo tungetembeza makonzi vichwani mwenu lakini tunawaheshimu na kuwaomba Msijifikilie ninyi tupunguzieni kero na sisi wananchi.
Ninyi huko barabarani hata kukaa foleni tu hamuwezi mnapita na ving'ola ila sisi kutwa kutuongezea usumbufu ni haki kweli?
TABOA GOMENI HII NI HUJUMA, Mkirudi MAGUFULI si Kwanza kuna uchawi mkubwa sana stend ya Magufuli HAPAFAI MTAFILISIKA.