Mabasi kulazimishwa warudi Magufuli ni hujuma: lengo SGR ipate wateja na kutafuta mapato stendi kuu

Mabasi kulazimishwa warudi Magufuli ni hujuma: lengo SGR ipate wateja na kutafuta mapato stendi kuu

Mara nyingi kitu kilicho nje ya utaratibu kikifanywa mara kwa mara(mara nyingi) na watu wale wale...hugeuka mazoea!

Tufuate utaratibu...

Basi ni lazima ianzie stendi...iache mapato...na abiria wanaofata utaratibu nao wapate usafiri...

Basi kukutoa mahala ulipo,kituoni kwako..hiyo ni favor!

Procedure lazima zizingatiwe!
 
Naungana na Chalamila kwa hili la mabasi ya abiria kwenda Mbezi
 
Stendi ni magufuli. Mabasi yawe na shuttle kama kwenye viwanja vya ndege. Ambapo abilia atalipia nauli pungufu ya daladala za kawaida.
 
Stendi ni magufuli. Mabasi yawe na shuttle kama kwenye viwanja vya ndege. Ambapo abilia atalipia nauli pungufu ya daladala za kawaida.
Hapo magufuli penyewe matundu ya choo yanayofanya kaz ni matatu tu, na moja tu ndiyo linabomba za maji
 
Naungana na Chalamila kwa hili la mabasi ya abiria kwenda Mbezi
Hapo magufuli zile frem ambazo zilipaswa kuwa ofisi yapo maduka ya unga wa lishe na njegele ofisi ziko ndani uchochoroni usiku unakabwa na waporaji
 
Chenjeu hawa. Sema muda utaongea ukweli tu.
Akili ya kawaida kabisa hata maji kukiwa na foleni huwekwa koki nyingi ,, sasa mkoa mzima stend moja hiyo ni akili au matope, wacha watunishe misuli yao muda utaamua
 
Kibongo bongo ukimiliki gari unaheuka kuwa ng'ombe wa maziwa. Serikali yako huwa inaoenda kupata kodi kwa njia ya mserereko.
Kwenye sekta nyingine huko mfano madini, Wachina wanajibebea tu na kodi hawalipi! Ndiyo serikali yako hii. Ina watu wasiopenda kuumiza vichwa vyao.
Bado wana mawazo ya kizamani kwamba mtu mwenye gari ana mahela mengi
 
Jamani hii ni hujuma ya wazi kwa wamiliki wa mabasi;

Serikali sikivu ni ile inayotatua kero, Lakini Tunashangaa sana badala ya kutatua Zinazidishwa: HAIWEZEKANI

Mtakumbuka Enzi za mkurugenzi Kabwe aliyetumbuliwa na magufuli kwa ufisadi kupitia Stand,

Sitaki kugusia makando kando ya uendeshaji mbovu na ukosefu wa huduma mhimu stendi kuu.

HOJA MHIMU ni lini mabasi yalikuwa kero kusogeza huduma kwa wananchi?

Je, kama Wamiliki wa mabasi watakapoamua kuitafsiri kuwa hii fukuza fukuza mabasi mtaani ni hujuma dhidi ya SGR Ipate wateja WATAKUWA WAMEKOSEA?

Je, hatuoni tunahatarisha SGR nayo kuhujumiwa kama wenye mabasi wakiamua kujibu?

WENYE MABASI ni wafanya biashara, Wanamikopo bank wanadaiwa marejesho;

Wenye mabasi wamewekeza Brand na ujenzi wa ofisi zao kwa gharama kubwa zaidi bilioni za fedha ili kuweka mazingira rafiki kwa abiria kupumzika wakijiandaa na safari LEO ghafla unawaambia ONDOKENI pekekeni magari stendi hivi mnajua maumivu ya kuwekeza?

Mnataka abiria warudi kwenye gombea gombea stendi ili kulinda Vizimba na mapato ya stendi huku mkipuuza utu na staha za wananchi?

Mnataka mkafungie mabasi yote stendi ili muanze kuyaruhusu kutoka kwa muda maalum jamani zama zimebadilika, kwanini hamtaki kubadilika?
AU ILE KAULI YA MSAFIRI KAFIRI ndiyo bado inawatawala vichwani?

MNATAKA ABIRIA anaetoka/kwenda mkoani kwa gharama ya nauli ya 60k, Then Akishuka maghufuli, Alake wapi kama ni gesti hiyo gharama anapata wap, au kwenda kwake akodi bajaji 50k Au pengine
kupoteza mali zake kwa kuibiwa stend, ACHILIA MBALI Kero na usumbufu wa wakata tiketi, wabeba mizigo n.k

Mnataka abiria wakimbie kero hizo wakapande sgr, Je wenye mabasi mikopo watalipaje?

Yote 9 kwanza kwanini kujiamulia mambo ambayo si kero ndiyo mnayafanya kero?
Biashara ya mwendokas imewashinda na abiria wapo kibao.
MNAKAA KIKAO KUZUIA WAFANYA BIASHARA WATAOTAFTA ABIRIA MTAANI MBAONA NI SAWA?

VIONGOZI kwa hili mnazingua sana mnatia hasira sana kwetu wananchi tunatamani japo tungetembeza makonzi vichwani mwenu lakini tunawaheshimu na kuwaomba Msijifikilie ninyi tupunguzieni kero na sisi wananchi.

Ninyi huko barabarani hata kukaa foleni tu hamuwezi mnapita na ving'ola ila sisi kutwa kutuongezea usumbufu ni haki kweli?

TABOA GOMENI HII NI HUJUMA, Mkirudi MAGUFULI si Kwanza kuna uchawi mkubwa sana stend ya Magufuli HAPAFAI MTAFILISIKA.
Kwani SGR haina abiria?
 
Back
Top Bottom