Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

Kwa mujibu wa LATRA, watoa huduma hao wamekuwa wakitumia fursa ya kuanza safari mapema (Saa 9 Usiku hadi 11 Alfajiri) kwa kufanikisha malengo ya kufanya mashindano huku kukiwa na wanaobashiri Basi linalofika mapema wakipata ushindi kwenye Kamari.
Kweli Bongo nyoso😂😂😂
 
Ujio wa katarama unampa shida kubwa ally's ndiyo maana kila kukicha latra wamekuwa mstari wa mbele kumsaidia ally's na kipigo cha kuisoma namba....
Katarama ndiyo chaguo la watu wa mwanza inajulikana sasa iweje latra inawauma ?
Ally's ni mkongwe kwenye hii game,hawa chipukizi wanakuja na kutoweka ila mkongwe anaendelea kubaki
 
Wanazi wamechangia sana ile mikeka imefanya madereva wakimbize sana hayo mabasi

Ila ligi yao tamu sana

Kwenye ligi la mabio wapo Happy Nation na Frester vipi wao hawajapigwa ban kuanza safari mida hiyo
Hujaja kwenye ligi ya Dar-Mbeya-Tunduma. Golden deer baba lao chuma saa 12 kasoro jioni inasoma stendi Uyole.

Wanazi wanazingua kupost hizo clips mitandaoni.
 
Juzi ahamisi Ally's hio ya Saa tisa ilifika Bariadi Mjini Saa 2 kasoro, hii ningeambiwa na mtu ningebisha nimeshuhudia mwenyewe.

Hata wewe una haki ya kubisha maana sio kitu cha kawaida.

Kwa inshu ile nikajisemea huyu hamalizi week.
 
Ilifika Bariadi SAA 9 ikitokea wapi?
 
Tatizo ni kuwa Tanzania kuna uzembe mwingi ,dereva mmoja hawezi kuendesha umbali huo wote pasipo kuchoka.Na wamiliki wa mabasi hawataki kuajili madereva 2 kwa kila basi.
Unataka kunambia dereva mmoja anaendesha kutoka MWZ-DSM?
 
Tatizo ni kuwa Tanzania kuna uzembe mwingi ,dereva mmoja hawezi kuendesha umbali huo wote pasipo kuchoka.Na wamiliki wa mabasi hawataki kuajili madereva 2 kwa kila basi.
Dar Mwanza hakuna madereva wawili kweli ?
mbadilishano ikiwa Dom
 
Dar Mwanza basi zote Ally's,Katarama,Happy Nation,Isamilo n,k madereva ni wawili.

Siungi mkono LATRA kuzuia,ila hii ligi ya Ally's Vs Katarama ni ngumu, iamuliwe mapema kwa namna nyingine na sio kuzuia kutoka saa tisa.
 
Back
Top Bottom