Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

Nyie mnaoshabikia mwendo kasi siku usikie basi limeua mkeo, mumeo, mtoto au ndugu yako yeyote wa karibu sidhani kama utaendelea kushangilia huu upuuzi, juzi johanvia ya musoma dar imeua pale morogoro chanzo ni mwendokasi
 
Nyie mnaoshabikia mwendo kasi siku usikie basi limeua mkeo, mumeo, mtoto au ndugu yako yeyote wa karibu sidhani kama utaendelea kushangilia huu upuuzi, juzi johanvia ya musoma dar imeua pale morogoro chanzo ni mwendokasi
Kufa tutakufa tu mkuu ajali popote inaweza kutokea hata ukiwa unasafiri na daladala
 
Hii ligi huwa inanishangaza kitu kimoja tu, hizo katarama ukikuta wanazi wanavozifia alafu kaangalie mikeka sasa utashangaa mwenyewe.

Yaani kwenye mikeka ni tofauti na wanavozisifia,

Mikeka ya mwezi mzima ally's ndo huwa inafungua geti mara nyingi kuliko gari zote ila sasa wanazi wakute wanasifia katarama!

Kuna jamaa anasema katarama anafika dodoma saa 3 asubui kama vile ni jambo la ajabu!! Wakati hao wote wanatoka saa 9 usiku dodoma wanapitaga wote saa 3
 
Wanazi wa Katarama ni wajinga sana yaani wanaongeaga pumba sana
 
Ila kwa wapenzi wa hayo mabasi bado wataendelea yasubiri.
Hao wengine watakosa masoko vile vile.

Hapo imefanyika kufungia basi zote. Ila watalalamika kwa Sagini watafunguliwa
Allys ana gari nyingi sana na zilizofungiwa ni ebf 3 na dxs 3 bado kuna farsi weupe EBG, kuna EBU,DVA sasa huyo katarama ana gari tatu zote zimepigwa ban
 
huyu mshereheshaji ndio amewaponza.!
 
Allys ana gari nyingi sana na zilizofungiwa ni ebf 3 na dxs 3 bado kuna farsi weupe EBG, kuna EBU,DVA sasa huyo katarama ana gari tatu zote zimepigwa ban
Ndio mkuu, Ally's ana akili sana. Katarama kapewa akina DXS roho za paka wamchekeche humo road, muda huohuo zipo DVA na EBG zinatembea zimerelax.

Kumbuka DXS (Most wanted, Winchester) ndio ziliwatuliza kina Tungi's, Travel Partner na wengine waliojileta race na bado zipo mzigoni😂😂
 
Bora yamefungiwa maana mwendo wao ulikuwa ni wa hatari kuliko hatari yenyewe......huwa nashangaa nikiona watu wakifurahia mwendokasi na kuwekeana mpaka pesa kwa ajili ya mshindi....
 
Anayenunua Mchina tatu badala ya Polo moja ndiye mwenye akili ya biashara

Si umeona kampuni kongwe kama Abood na Shabiby wamehama kutoka Scania Marcopolo na Volvo sasa hivi ni mwendo wa Yutong
Kwa polo abiria 60 kwa Hela ya polo mchina una abiria 180 mchina fasta mtaji unarudii polo hadi miaka 10 mchina miaka 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…