Mabasi ya mikoani inabidi muwe na muda maalum wa kuwasha na kuzima TV

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.

Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.

Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.
 
Sema mkuu watu tunatofautiana sana wengine wanapenda sana hii Hali.

Mabasi ya mkoani ukipanda tu Tyr unakuta tamthiliya ya mkojani ama yule jamaa madebe mwanzo mwisho.

Binafisi Kwa ulimwengu wa Sasa Tv hazina nafasi Tena simu zetu zinatosha kutupa furaha uipendayo mchawi bando tu
Ndio maana nikasema inabidi kwenye bus wafanye kubalance, nusu ya safari TV isiwashwe/izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe.
 
Maisha ya huko utayashangaa ukiingia katika mataifa mengine wanaojali na kuheshimu utu
Unamlazimishaje mtu asikilize makelele wakati hujui hawa watu mmekutana humo kwenye safari kama wana majonzi wakielekea msibani, wakiwa wagonjwa, wazee waliopitwa na haya wakitaka kuwa kimya
Wengine wafanyabiashara wakiwasiliana mara kwa mara
Tusichoshane ila sio sawa kabisa na ni kero
Natamani mmiliki mmoja wa mabasi akapiga marufuku mabasi yake kuwa na makelele kabisa yaani kimya kama Ulaya
Ujinga huu nje huwezi kuuona yaani hata kwenye viti pameandikwa ongea kwa simu polepole, hakuna hata radio ni kimya kabisa unalala zako tu
Kwani usipopiga mziki unakosa wateja?
 
Kwenye bus wapo pia ambao hawapendi TV au hiyo TV ndio inawapa stress.
Wengi wape,wengi hupendelea burudani hizo na imezoeleka na ni kama utamaduni.
Ila kwa sasa kuna maboresho,baadhi ya Bus zinaletwa kwa muundo wa Kila siti na TV zake.Waeza jarbu hizo,muhimu pochi inone
 
Kwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.

Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.

Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.
Na wale tunao shukia njian ?
 
Nunua bus lako weka hiyo sheria mbona simple tu mkuu🤣🤣
 
pole
Serikali iweke utaratibu kampuni za mabasi kuajili watu wasioishiwa maneno kama dotto magari kizimkazi ili wawe wanaongelesha madereva mwanzo wa safari hadi mwisho wa safari

hutaona mamiziki hayo
 
Back
Top Bottom