Mabasi ya mikoani inabidi muwe na muda maalum wa kuwasha na kuzima TV

Kwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.

Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.

Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.
Usafiri wa bus ya mikoani ni wa kimasikini sanaa ni kero kwa mtu diplomant au corporate, kelele ni nyingi ku simama sima bila maelezo kuambwa tiketi mara kwa mara wakati mgine imesonzia unaamshwa ghafra, sijui nani kawambia kwamba kuangalia TV au video ndo burudani tu,
 
Kweli.
Kwanza waachane nazo kabisa.

Sisi tumekuja kusafiri. Si kutazama muziki wala movies. Hivyo vyote tunavyo nyumbani.
Mtu wa kusafiri safiri kila wiki atakuwa anaboreka kiasi kgani kusikiliza nyimbo hizo hizo na movie hizo hizo kila anaposafiri na hilo basi lenu?
 
Sema mkuu watu tunatofautiana sana wengine wanapenda sana hii Hali.

Mabasi ya mkoani ukipanda tu Tyr unakuta tamthiliya ya mkojani ama yule jamaa madebe mwanzo mwisho.

Binafisi Kwa ulimwengu wa Sasa Tv hazina nafasi Tena simu zetu zinatosha kutupa furaha uipendayo mchawi bando tu
Kwny safari ndegu hata hiyo simu utaichoka...lbd uweke Hollywood Movies
 
Sisi huku mtu ukikaa naye siti moja mnakuwa kama marafiki wa siku nyingi unaweza ukashangaa kanunua vipande vya Mafenesi anakugawia kama huko Usukumani unakuta Basi zima linakula Miwa na Dereva naye anagaiwa kipande ili awawahishe muendako.
😂😂😂
Na hakuna raha kama kukaa na jinsia Me, wengi wao wanajua kujali balaa, unamuomba umuegemee au umuwekee miguu na hawakatai maskiini..!!

tunawapenda sana wanaume wetu..!
 
Nilisha mpisha mdada mzuri aje akae, mara akaja mama mtu mzima ,yule dada akaenda kukaa na mwamba mwingine, huku akiniangalia kwa tabasamu, yani nilinuna safari nzima yule mama akinipigisha stories namjibu kwa kifupi na kwa hasira😁😁😁😁😁😁
 
Kwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.

Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.

Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.
Bila kusahau matumizi ya AC
 
Nilisha mpisha mdada mzuri aje akae, mara akaja mama mtu mzima ,yule dada akaenda kukaa na mwamba mwingine, huku akiniangalia kwa tabasamu, yani nilinuna safari nzima yule mama akinipigisha stories namjibu kwa kifupi na kwa hasira😁😁😁😁😁😁
Huyo mama hakuwa hata lishangazi ujipatie chochote kitu?
 
Nilisha mpisha mdada mzuri aje akae, mara akaja mama mtu mzima ,yule dada akaenda kukaa na mwamba mwingine, huku akiniangalia kwa tabasamu, yani nilinuna safari nzima yule mama akinipigisha stories namjibu kwa kifupi na kwa hasira😁😁😁😁😁😁
Hiyo mbaya sana mkuu ulijikuta jentromanii mwenyewe 🤣🤣🤣🤣 halafu kikaumana aiseee
 
Watu wanaangalia sio biashara ila wanawezaje kuwa bora katika biashara yaooo

Mkuu kuongelea kunguni kwenye bus ni moja ya hoja dhoofu sana.

Kwani kunguni wanaletwa na nani humo?

Hivyo vyuma si vinanunuliwa vipya?
 
Sisi huku mtu ukikaa naye siti moja mnakuwa kama marafiki wa siku nyingi unaweza ukashangaa kanunua vipande vya Mafenesi anakugawia kama huko Usukumani unakuta Basi zima linakula Miwa na Dereva naye anagaiwa kipande ili awawahishe muendako.
😄 🤣 😂 😆 😄
Wajanja wakawawekea madawa ya kulevya wakabeba kila kitu
Ila Wasukuma wakarimu sana kwa kweli
 
Mkuu kuongelea kunguni kwenye bus ni moja ya hoja dhoofu sana.

Kwani kunguni wanaletwa na nani humo?

Hivyo vyuma si vinanunuliwa vipya?
Kunguni wanaletwa na abiriaa mwenyewe especially wanafunzi
 
Back
Top Bottom