Mabasi ya mikoani inabidi muwe na muda maalum wa kuwasha na kuzima TV

Mabasi ya mikoani inabidi muwe na muda maalum wa kuwasha na kuzima TV

Beba flash jaza vile unavyopenda kuangalia iwe movies au video za miziki ukiona namna gani waombe wachomoe ushamba wao waweke ujanja wako safi kabisa na ukiongea nao vizuri hawakatai mteja ni mfalme popote pale hata kwenye ndege
 
Nikiwa safarini muda mrefu napenda kujisomea na kuangalia mandhari kuliko kuangalia TV au kusikiliza muziki.
 
Mkuu kweni huko Uingereza Mabasi hayana Runinga?!
Hakuna ujinga huo
Hayo huko ndio makasiriko ya Mungu mnakufa kila siku kwa ajali
Dereva mjinga badala ya kusikiliza gari kama lina tatizo lolote hata kelele za ingine au kama kuna lolote hawezi kujua maana ni viroba na mziki
. Kusema la haki ni ushamba sana huo kupiga kelele kwani umepanda Bus likufikishe point A to B kama ni mpenzi wa mziki si uweke headset zako?

Huku ni announcements tu kama uko wapi basi hakuna hata kuongea na mtu kwani hamjuani

😄 huko kukaa na mtu siti moja kaishakuwa mshikaji wako mpaka begi eti unamwambia niangalizie aisee
 
Maana halisi ya biashara binafsi.

Kwani mtu kama anadhani wanafanya hovyo si anaanzisha yake halafu anaifanya vizuri zaidi?
Wewe utafurahi umepanda bus zinaonyeshwa movies za Wamarekani wanawatwanga Iran au Israel wanawapiga Wapalestina??
 
Huduma zao huwa zipo classified pale mlangoni wana Tv wengine wifi wengine beverages kwahiyo kama kuna huduma hapo inakukera ni bora usitumie hilo bus maana ni usafiri wa umma we utasema zima Tv mwingine atasema washa.

Itabidi wamsikilize aliesema washa maana tayari walishaainisha huduma hiyo ipo wewe ambae huridhiki na huduma ya public inatakiwa uangalie ustaarabu wa kutumia usafiri binafsi
 
Nikiwa safarini muda mrefu napenda kujisomea na kuangalia mandhari kuliko kuangalia TV au kusikiliza muziki.
Chukua flash jaza movie za nature wanyama na mazingira then kampe kondakta mwambie ondoa huyo Koffi Olomide na bongo movie za kiduanzi weka hapa tuone kinachotokea maporini huku tu-refresh memory
 
Yaani kwa Tz TV ni big deal! Na mbaya zaidi hizo TV wanawekaga madude yaleyale miaka nenda rudi.
Natamani kusiwepo na TV kabisa, basi ikibidi kuwe na makala maalumu za tafiti toka vyuo vya kilimo, biashara, n.k; sio kulazimishana kula matakataka
 
hamjuani

😄 huko kukaa na mtu siti moja kaishakuwa mshikaji wako mpaka begi eti unamwambia niangalizie aisee
Sisi huku mtu ukikaa naye siti moja mnakuwa kama marafiki wa siku nyingi unaweza ukashangaa kanunua vipande vya Mafenesi anakugawia kama huko Usukumani unakuta Basi zima linakula Miwa na Dereva naye anagaiwa kipande ili awawahishe muendako.
 
Wewe utafurahi umepanda bus zinaonyeshwa movies za Wamarekani wanawatwanga Iran au Israel wanawapiga Wapalestina??

Kwa hakika sana tu kwa sababu ninaheshimu mno biashara ya mtu.

Labda ungekuwa wazi tu mkuu tatizo lako hasa nini?

1. Ungependa biashara za watu kufuata matakwa yako? Au:

2. Ungependa mageuzi tu maana hii kwako imekuwa too monotonous?

Zingatia mawili hayo ni tofauti.
 
Yaani kwa Tz TV ni big deal! Na mbaya zaidi hizo TV wanawekaga madude yaleyale miaka nenda rudi.
Natamani kusiwepo na TV kabisa, basi ikibidi kuwe na makala maalumu za tafiti toka vyuo vya kilimo, biashara, n.k; sio kulazimishana kula matakataka
Hutaki we chukua simu yako vaa earphone usikilize vyako
 
Nyimbo zenyewe wanazoweka Sasa
Za uchi uchi tu
Ukisafiri na mzazi ni sheeda
 
Yaani kwa Tz TV ni big deal! Na mbaya zaidi hizo TV wanawekaga madude yaleyale miaka nenda rudi.
Natamani kusiwepo na TV kabisa, basi ikibidi kuwe na makala maalumu za tafiti toka vyuo vya kilimo, biashara, n.k; sio kulazimishana kula matakataka
Inaonekana masikini huwa wanapenda zaidi entertainments muda wote, bongo zao zinakosa imaginations na content nyingine nje ya TV.
 
Kwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.

Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.

Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.
Kama una safiri njia ya Kaskazin yaani Dar to Arusha au Dar to Tanga panda Tahmeed
 
Back
Top Bottom