zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Ndio Maana halisi ya usafiri wa Uma ukitaka unavyovipendelea wewe safiri na usafiri wako Binafsi Mangi
Nikiwa safarini muda mrefu napenda kujisomea na kuangalia mandhari kuliko kuangalia TV au kusikiliza muziki.Beba flash jaza vile unavyopenda kuangalia iwe movies au video za miziki ukiona namna gani waombe wachomoe ushamba wao waweke ujanja wako safi kabisa na ukiongea nao vizuri hawakatai mteja ni mfalme popote pale hata kwenye ndege
Hakuna ujinga huoMkuu kweni huko Uingereza Mabasi hayana Runinga?!
Mara nyingi kwenye Tickets unakuta huwa wanatangaza kuwa Basi lina WIFI TV nk. Ni bora ukakata Basi lisilo na Elecronic Entertainment.Nunua bus lako weka hiyo sheria mbona simple tu mkuu🤣🤣
Wewe utafurahi umepanda bus zinaonyeshwa movies za Wamarekani wanawatwanga Iran au Israel wanawapiga Wapalestina??Maana halisi ya biashara binafsi.
Kwani mtu kama anadhani wanafanya hovyo si anaanzisha yake halafu anaifanya vizuri zaidi?
Wengi wanapenda muziki sasa kuliko wasiopendaMara nyingi kwenye Tickets unakuta huwa wanatangaza kuwa Basi lina WIFI TV nk. Ni bora ukakata Basi lisilo na Elecronic Entertainment.
Nunua bus lako weka hiyo sheria mbona simple tu mkuu🤣🤣
Chukua flash jaza movie za nature wanyama na mazingira then kampe kondakta mwambie ondoa huyo Koffi Olomide na bongo movie za kiduanzi weka hapa tuone kinachotokea maporini huku tu-refresh memoryNikiwa safarini muda mrefu napenda kujisomea na kuangalia mandhari kuliko kuangalia TV au kusikiliza muziki.
Sisi huku mtu ukikaa naye siti moja mnakuwa kama marafiki wa siku nyingi unaweza ukashangaa kanunua vipande vya Mafenesi anakugawia kama huko Usukumani unakuta Basi zima linakula Miwa na Dereva naye anagaiwa kipande ili awawahishe muendako.hamjuani
😄 huko kukaa na mtu siti moja kaishakuwa mshikaji wako mpaka begi eti unamwambia niangalizie aisee
Wewe utafurahi umepanda bus zinaonyeshwa movies za Wamarekani wanawatwanga Iran au Israel wanawapiga Wapalestina??
Hutaki we chukua simu yako vaa earphone usikilize vyakoYaani kwa Tz TV ni big deal! Na mbaya zaidi hizo TV wanawekaga madude yaleyale miaka nenda rudi.
Natamani kusiwepo na TV kabisa, basi ikibidi kuwe na makala maalumu za tafiti toka vyuo vya kilimo, biashara, n.k; sio kulazimishana kula matakataka
Inaonekana masikini huwa wanapenda zaidi entertainments muda wote, bongo zao zinakosa imaginations na content nyingine nje ya TV.Yaani kwa Tz TV ni big deal! Na mbaya zaidi hizo TV wanawekaga madude yaleyale miaka nenda rudi.
Natamani kusiwepo na TV kabisa, basi ikibidi kuwe na makala maalumu za tafiti toka vyuo vya kilimo, biashara, n.k; sio kulazimishana kula matakataka
Hutaki we chukua simu yako vaa earphone usikilize vyako
Kama una safiri njia ya Kaskazin yaani Dar to Arusha au Dar to Tanga panda TahmeedKwa baadhi ya watu ni mateso unasafiri na bus muda wote wa safari kuanzia asubuhi mpaka jioni TV imewashwa ni mwendo wa kubadilisha tu kwaya, kaswida, bongo flavours, movies na comedy mbovu.
Yani kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari TV haizimwi isipokuwa saa ya matangazo ya biashara za Vigour Doctor, sabuni na mafuta ya ukwaju na dakika 10 tu za kuchimba dawa.
Kwenye safari inabidi nusu ya safari hasa safari inapoanza TV izimwe halafu nusu ya pili ya safari ndio TV iwashwe, kama bus linasafiri masaa 12, masaa 6 TV isiwashwe.