Mabasi ya wanafunzi yapewa kibali cha kuwa Daladala kwa muda wa miezi mitatu kukabili uhaba wa usafiri uliosababishwa na " level seat"

Mabasi ya wanafunzi yapewa kibali cha kuwa Daladala kwa muda wa miezi mitatu kukabili uhaba wa usafiri uliosababishwa na " level seat"

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Serikali imetoa ruksa kwa mabasi yenye rangi ya njano yanayobeba wanafunzi kutumika kama daladala wakati huu ambapo shule zimefungwa.

Mkurugenzi mkuu wa Latra amesema wamiliki wa school bus watapewa vibali vya kuweza kubeba abiria kwa kipindi cha miezi mitatu ili kufidia upungufu wa mabasi uliosababishwa na utaratibu mpya wa level seat.

Source Eatv habari!
 
Tunashukuru sana serikali kwa kuruhusu magari ya wanafunzi. Lakin bado tunaomba sana sana waruhusu coast na noa na magari ya watu binafsi yabebe watu. Shida ni kubwa sana.

Watu wanakaa kituon mda mref sana na wengingine wanapigania na kusababisha mgusano mkubwa sana.

Serikalo iliangalie hili. Kuna coast nyingi zimepak tu.zinasubir kukodiwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Zitumoke wakati huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu
 
Serikali imetoa ruksa kwa mabasi yenye rangi ya njano yanayobeba wanafunzi kutumika kama daladala wakati huu ambapo shule zimefungwa.

Mkurugenzi mkuu wa Latra amesema wamiliki wa school bus watapewa vibali vya kuweza kubeba abiria kwa kipindi cha miezi mitatu ili kufidia upungufu wa mabasi uliosababishwa na utaratibu mpya wa level seat.

Source Eatv habari!
Hatua nzuri hiyo. Nakumbuka miaka ya 70 Waziri Mkuu Sokoine aliruhusu kitu kama hicho. Mabasi ya mashirika ya umma na ya serikali (SU na ST) yalikuwa yakimaliza kupeleka wafanyakazi wa taasisi husika yanafanya kazi ya daladala kwa masaa kadhaa. Huu ni utumiaji mzuri wa mali ya umma.

Badala ya basi kukaa tu wizarani au kwenye shirika tangu saa mbili asubuhi linapoleta wafanyakazi wa hapo mpaka jioni wakati wa kuwarudisha, linasaidia kupunguza tatizo la usafiri jijini na wakati huohuo linatengeneza hela kidogo za kujiendeshea.
 
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu

Natamani Makonda aone hili swali lako!
 
Tunashukuru sana serikali kwa kuruhusu magari ya wanafunzi. Lakin bado tunaomba sana sana waruhusu coast na noa na magari ya watu binafsi yabebe watu. Shida ni kubwa sana. Watu wanakaa kituon mda mref sana na wengingine wanapigania na kusababisha mgusano mkubwa sana. Serikalo iliangalie hili. Kuna coast nyingi zimepak tu.zinasubir kukodiwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Zitumoke wakati huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwai coaster zilikatazwa? Mbona leonimepanda coaster ya posta?
 
Mingi au michache bwashee?!
Samahani kuuliza ndugu yangu. Wewe ni KE yaani umeolewa na mchaga ama ni ME umemuoa mchaga? Maana naona kama unapagazwa nao sana kuliko kawaida.

Hoja yake umeilewa au mahaba yako ya kuandika "bwashee" yamekupofusha hadi umeshindwa kuiona hoja yake?

nguvu anachoshangazwa nacho kama ugonjwa si mkubwa kiasi hico ni kwa nini kibali kitolewe kwa miezi mitatu kama vile ni jambo la kuendelea wakati tuliambiwa ni kwa mwezi mmoja tu?

Au Karantini bubu inaendelea mpaka mwezi wa saba?
 
Samahani kuuliza ndugu yangu. Wewe ni KE yaani umeolewa na mchaga ama ni ME umemuoa mchaga? Maana naona kama unapagazwa nao sana kuliko kawaida.

Hoja yake umeilewa au mahaba yako ya kuandika "bwashee" yamekupofusha hadi umeshindwa kuiona hoja yake?

nguvu anachoshangazwa nacho kama ugonjwa si mkubwa kiasi hico ni kwa nini kibali kitolewe kwa miezi mitatu kama vile ni jambo la kuendelea wakati tuliambiwa ni kwa mweiz mmoja tu?

Au Karantini bubu inaendelea mpaka mwezi wa saba?
Hiyo miezi mitatu ni maximum......kama shule zikifunguliwa lmmiliki ana hiyari ya kubeba wanafunzi na abiria kwa nyakati tofauti !

Ndio maana nimemuuliza ni mingi au michache maana kwa wamiliki wengine hiyo ni fursa muhimu kwao wangependa hata kibali kiwe cha mwaka mzima mwagito!
 
Serikali imetoa ruksa kwa mabasi yenye rangi ya njano yanayobeba wanafunzi kutumika kama daladala wakati huu ambapo shule zimefungwa.

Mkurugenzi mkuu wa Latra amesema wamiliki wa school bus watapewa vibali vya kuweza kubeba abiria kwa kipindi cha miezi mitatu ili kufidia upungufu wa mabasi uliosababishwa na utaratibu mpya wa level seat.

Source Eatv habari!
Hiyo miezi mitatu shule zitakuwa bado zimefungwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatua nzuri Lakini uwa najiuliza sana swali nairobi na dar upi mji una popolation kubwa ninapokuwa nairobi sijawahi kuona mtu anasimama kwenye matatu wakati nairobi ina wakazi milion 7 je shida yetu ni uchache wa daladala au ubovu wa miundombinu
Wabongo kwa kutaka dezo!!
Kwani nauli ya matatu ni shs ngapi kwa hela ya hapa?

Wabongo walio wengi wanataka starehe pasipo kulipia gharama.

Kenya nauli ni shs 50 sawa na 1200 ya hapa kwa kila safari..kwa hiyo wanalipia gharama ya levo siti.

Hii ni nauli ya kichwa, hakuna cha mwanafunzi wala polisi wala mwanajeshi, wote wanalipa nauli sawa.

Huko tuendako, kwa vile hata mwalimu halipi mauli, tusijeshangaa kukawa na maandamano ya kutaka kupanda daladala za watu bila kulipa nauli.

Hii ndiyo Tanzania.
Mwalimu halipi nauli wakati analipwa mshahara, polisi halipi, wala askari jeshi halipi, na wote wanalipwa mshahara lakini mwanafunzi asiyelipwa mshahara ni lazima alipe japo nusu nauli.

Ukisangaa ya Musa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom