Tutasoma yote hayo huko baadae, lakini kwa sasa nina haya machache:
1. Hakuna nchi yoyote duniani isiyopigania maslahi yake; isipokuwa labda hizi zetu za 'Banana Republic' ambazo maslahi ya viongozi wake ndiyo yanayowekwa mbele zaidi ya yale ya nchi husika.
China wana maslahi, ndiyo maana ya hiyo BRI; kwa hiyo kama nchi inao viongozi wenye akili timamu hawawezi kusubiri mpaka waambiwe na "mabeberu" ni wapi maslahi ya nchi zao yalipo.
Kama wanajua maslahi ya nchi zao yako wapi, basi watafanya uamzi sahihi kuhusu mradi ulio na manufaa kwa nchi zao.
Tuna miaka zaidi ya sitini sasa tukijiamlia mambo yetu. Tunao watu waliosoma vizuri na kuelewa mambo vizuri karibu katika kila fani. Hatuna visingizio tena vya kusema hatuna raslimali watu. Iliyopo sasa ni kutojua tu jinsi ya kuitumia vyema raslimali hiyo.
Acha mchina aje na BRI yake atuonyeshe anataka kufanya nini, na sisi tumueleze mategemeo yetu ni nini, bila ya aibu au woga wowote.
Tujadiliane, tukikubaliana, ajenge kwa makubaliano tuliyofikia pamoja na yeye; kama hatukubaliani juu ya matakwa yake, aende zake, na wala isiwe tena hizi kelele za mabeberu hivi au mabeberu vile. Huu utakuwa ni uamzi wetu.
Na hii haituzuii kuingia kwenye mapatano mengine juu ya mradi huo, eti kwa kuogopa tu "mabeberu".
Tayari Biden na BoJo wanajadili uwezekano wa kuweka $65 Billion mezani kwa kazi hiyo ya kupambana na BRI. Hatuwezi kuwaogopa hawa wala mwingine yeyote, kama tunajua maslahi yetu ni yapi.Hizo enzi za kuyumbishwa na kugawanywa zimepitwa na wakati - ni maslahi yetu pekee ndiyo yaliyo muhimu.
Na si hawa pekee, yaani China na Mabeberu tunaoweza kushirikiana nao kujenga mradi huo, na sio lazima iwe mmoja, wawili au kundi lwa wawekezaji. Huu ni mradi mkubwa, kwa hiyo kila mtu anaweza kushiriki ankoona kunamfaa, na tutakaribisha aje tujadili, tukiafikiana anajiunga.
Tunaweza pia kuanza kujenga sisi wenyewe taratibu, kama Lamu inavyojengwa hivi sasa, baada ya kukosa mwekezaji wa kuuchukua kama huyo BRI na wengine.
2. Ukweli ni kwamba, Tanzania na pwani yake ipo pazuri mno. Wenzetu hapo juu wanahangaika kwelikweli kujiuza bila ya mafanikio yoyote.
Ni viongozi wetu tu watumie akili zao na uzalendo wao ili nchi yetu ifaidike na mahali ilipowekwa kijiografia.
Dunia ni kijiji!!
Haya mawazo yanatuchelewesha sana.
Kuna watu wenye mawazo kama yako walipinga sana Boda boda kufanya biashara ya kubeba abiri .
Leo hii hakuna ajira zaidi ya boda boda .
Kuna wakati ni lazima maamuzi yenye tija yafanyike.
Wazalendo wajinga wametuaminisha kuwa kila mradi ukifanywa na mtanzania wa kutoka kule Songombingo jirani na mzalendo feki basi ndio unatija na maslahi kwa nchi.
Nakupa mfano .
Miradi yote iliyofanywa na Watanzani wenzetu ina wizi mkubwa sana na imefanywa kwa kiwangao cha chini sana.
Mtu anapewa mradi wa bil. 10 anaufanya kwa kiwango cha chini kwa kutumia material hafifu ili abakiwe na trilion tano akajenge miradi yake binafsi huku Taifa likibaki na hasara.
Kuna stendi moja ya Wilaya ya Korogwe iliyokuwa imezinduliwa mwaka 2018 kwa Sifa nyingi . Mkurugenzi akasifiwa sana ,Mkandarasi ajaitwa mzalendo mkubwa kumbe na kila aina ya sifa.
Miaka mitatu tu leo stendi ile inatifuliwa kila sehemu kufanyiwa ukarabati.
Mabilioni ya pesa yamepotea na wahusika ni mabilionea.
Wanufaika wakubwa wa kandarasi zinazoliibia taifa hua ni watetezi wakubwa sana wa kauli za wawekezaji wanatuibia huku wao wakituibia fedha zetu za ndani zinazopatikana kwa kuwaumiza wafanyakazi na wafanyabiashara.
Kuna watu walioshiba kwa kuliibia taifa hili kupitia ofisi za umma kama hao wakurugenzi wa Bandari hawajui shida wanazopata maskini na watoto wao wanaosoma shule za kata na kisha kukosa ajira mana hakuna wawekeji wakubwa wanaoingiza mitaji toka nje.
Bandari ya Bagamoyo itajengwa mana ina tija kwa malaki ya vijana wa kitanzania wasio na ajira ukilinganisha na miradi iliyojengwa ambayo itapoteza ajira nyingi na pato kubwa la halmashauri zetu lakini bado imefanyika ili kuzibeba nchi jirani hasa Rwanda.
Huoni kuwa Reli itaua biashara za mabasi na malori?
Huoni kuwa mabasi na malori yanalipa Latra mamilioni ya fedha?
Huoni kuwa miji yote yalipokua yanalala malori na mabasi itakufa na biashara zitadoda na watu kukosa ajira?
Huoni kuwa halmashauri zilizokuwa zinakusanya ushuru kwa mabasi ya abiria kila siku zitakosa mamilioni ya fedha?
Huoni kuwa vituo vingi vya mafuta vitalosa mapata na hivyo ,motor vehicle licence, Ewura,Rea, Tarura, VAT, Tanroad na wamiliki na wafanyakazi wao wote watakosa mapato ?
Je, kuna wasomi waliofanya utafiti na kugundua kuwa kwa nchi maskini kama Tanzania Treni ya umeme haifai na haina tija kwa Watu wengi zaidi ya kundi dogo sana la wanasiasa na watalii??
Treni ya umeme ikiendeshwa kibiashara watu wengi watakuwa hawana uwezo wa kuipanda mana itabidi iwe ghali kama ndege au zaidi.
Treni ya umeme ikiendeshwa kama huduma rahisi kwa wananchi bila kujali faida itakua ni hasara kubwa kwa Taifa.
Huduma ya treni umeme inafaa kwenye nchi zilizoendelea sana ambazo huduma za msingi kama Nyumba ,elimu ya juu, afya n.k vinapatikana kwa mifumo rasmi.
Leo hii kila mwananchi anajijengea nyumba yake mwenyewe au anapangisha kwa kunyonywa na mwenye majumba halafu unaleta biashara za starehe kama ndege utalii wa ndani, treni ya umeme n.k utegemee kupata wateja wa ndani?
Mtu anawaza kujenga kakibanda kake aepukane na kodi zisizo na udhibiti halafu apate pesa za kupanda ndege ? Labda awe mwizi!!!
Mama Samia na Spika ndugai wekeni midahalo ya Wazi ya hii miradi mikubwa ili wazalendo wa kweli na wale feki waliokuwa wanatumia mitutu ya bunduki kulazimisha kuitwa wazalendo kumbe walikua ni Wauzalendo basi wajulikane !