Eti unasema? "...maelfu ya Hekari za kutokea mtukula mpaka Tanga yatakayokufa bila shughuli yoyote ya kiuchumi?"
Dola 16 na ushee kwa pipa linalopita hapo siyo shughuli? Kwa siku yatapita mapipa mangapi, unajua mkuu? Hiyo ni hela ndogo? Na hayo mafuta yakiisha, si ardhi bado ipo?
Unajua kuna jambo tunapokua kwenye ulaji wa kodi za wananchi tunalisahau.
Serikali ni watu wachache waliopewa dhamana ili wasimamie mifumo tuliyojiwekea.
Lakini kuna mamilioni ya watu wanaishi maisha yao ya kila siku hata kama pangekua hakuna serikali wangeishi raha mustarehe.
Lakini serikali bila watu wanaofanya shughuli zao na kulipa kodi haiwezi kuwa na nguvu ya kiuchumi. China na Marekani zinahangaika Dunia nzima ili watu wao wapate masoko makubwa zaidi sio tu tu wabanane kule ndani wenyewe kwa wenyewe.
Hujanielewa !
Kuna maelfu ya Hekari za Ardhi kutokea Mtukula mpaka Tanga ambayo huwezi ukalima,ukajenga,ukafungua Hoteli,ukafungua ,baa,ukaweka soko,ukaweka kiwanja cha mpira , ukajenga Josho la ng'ombe,ukajenga shule ,ukajenga kiwanda , ukachimba madini hata kama utagundua kuwa yapo, ukapanda miti ,ukatunza misitu, ukachimba kisima ,yaani ni maelfu ya ekari toka Mtukula mpaka Tanga hayataruhusiwa kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji au biashara kwa mwananchi maskini zaidi ya mabeberu na serikali inayolinda maslahi ya mabeberu wa Kirumi yaani Ulaya na Marekani !
Ardhi ya Bagamoyo kwenye Bandari kubwa Barani Afrika kutakua na shuguli nyingi za migahawa, mahoteli,nyumba za kupanga wafanyakazi wengi sana,biashara ya mabasi,daladala, mama lishe, wamachinga, viwanda vingi, Malori Maelfu kwa maelfu toka nchi jirani kuja kuchukua mizigo hivyo yataweka mafuta kwenye Sheli zetu na kutuingizia kodi ,pesa za Ewura,Tanroad,Rea, tarura n.k. Pia Biashara za magereji kutokana na magari kuwa mengi , ajira za walinzi ambao ni watu wa kawaida kabisa n.k.
Kwa hiyo kuleta stori za uzalendo wa ardhi ya Bomba la mafuta na kupinda ardhi ya Bandari ya Bagamoyo ni Uzalendo feki wa kikabila kwa sababu yule ni wa Pwani na yule ni wa mtukula . Tuwe wazalendo wa kweli wanaojali nchi yetu bila kujali nani amekaa kwenye ofisi ya Magogoni. Jambo jema ni jema tu hata likifanywa na mkoloni. Tuweke ushabiki pembeni.
Kenya kupitisha lile bomba ilikua ni shughuli kutokana na gharama kubwa ya kufidia ardhi kwa mabeberu wenye ardhi kule. Na ardhi yao ni ndogo hivyo mtu anamiliki ardhi na anapanga bei anayotaka alipwe . Wakakimbilia huku kwenye ardhi ya serikali inayoweza kuichukua bure na kumpa mwekezaji bila mwananchi kupata kitu anachoona kinamtosha.