Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Nimekimbilia kwenye hitimisho. Kule nitarudi baadaye.
===
Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!
Bahati mbaya haujafafanua namna gani Ugiriki ilikubalina kwa staili ipi na Mchina namna ya kuendesha bandari hiyo. Pia sioni maelezo ya Ugiriki inanufaika vipi kimapato kutokana na umiliki wa mchina kwenye bandari hiyo kwa 67% .
Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!
Tusisahau namna Wachina walivyokuwa wana'handle' ndugu zetu kwenye makampuni yao enzi za awamu ya "nne". Ukumbuke sipingi BRI.
Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?
Mkuu, hapa hapa unachafua mada yako bila sababu za maana. Kwa hiyo, unataka kuuaminisha umma kuwa uwanja wa ndege wa Chato utawanufaisha watanzania wanaoishi Chato pekee!?
Tafadhali, jielekeze kwenye kusimamia objectivity katika hili.
 
Mkuu Chige , Thanks for this. Kuna Watanzania wenzetu uwezo wao wa kuona mbali ni mwisho wa pua zao!. Tunajenga SGR, ile treni ina uwezo wa kuvuta mabehewa zaidi ya 100, ya 40ft container zikiwa double, zimepakatana!. SGR ukikamilika, huo mzigo wa kubebwa na SGR ili ijiendeshe kwa faida utatoka wapi?.
Niliuliza hili swali
Sikuwahi kujibiwa!.
Jibu la mzigo wa kuishibisha reli ya SGR ni bandari ya Bagamoyo.
P
Pasco,

Hilo swali lako ni la msingi sana, na binafsi nimeshauliza sana hapa JF! Nimeshawahi kuhoji tumeandaa mazingira yapi ya makusudi ya kuifanya SGR iwe productive! Hadi kesho, sijapata jibu la hilo swali.

Watu wanashindwa kuelewa kwamba, miradi ya aina hii inatakiwa kutengenezewa strategies kuhakikisha inakuwa utilized! Ulaya na Marekani kuna reli, lakini hadi kesho transporters wanatumia barabara!!

Hapo ndipo nikahoji, what's so special kitakachowafanya transporters wetu waachane na malori na kutumia SGR ikiwa hakuna miradi ya makusudi kwa ajili ya ku-utilize hiyo SGR!
 
Jadili hoja, kwa sababu ni mjinga tu ndie anaweza kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba!!
Mada yako imeegemea upande mmoja.

Unataka tusiiamini selikali ambayo ndio yenye mkataba, ila unataka tukuamini wewe unae watetea wachina ambae huna mkataba na umeandika kwa kudhani.

Sasa ili mada yako ionekane ya maana weka mkataba hapa.
 
Kipindi JPM yupo, mlimsema Kwa maneno yote yeye kujiegemeza Kwa wachina, inakuwaje tena Kwenye mradi huu wenye Mashaka makubwa, mnawaponda wazungu na kuwasifia wachina tena??

Tz ni kiwanda cha wanafki

Hata hivyo, mtetezi wa sheria asipozijua sheria zenyewe, huwa ni mtu wa ajabu na mganga njaa,

Utetezi wa huu mradi, ni marejeo ya mwandishi Mzee Mao kutoka China akiutetea mradi wao, lakini ameshindwa kabisa kuonyesha masharti yaliyoko Kwenye Mkataba

Wasomi na wapenda nchi, tunasema, uwekezaji huu, kuna wengi watahongwa ili kuuza Utu wao na kuiuza nchi Yao wenyewe Kwa manufaa Yao wenyewe,

Hivyo, kama hakuna Mkataba, yoote hayo yaliyoandikwa, ni malipo mazuri ya wachina kuja Kwa mwandishi
 
Chige asante sana kwa uzi uliosheheni nyama na virutubisho muhimu.

Nikiri wazi kuwa hii ndio mara ya kwanza kupata au kusoma maelezo ya kina na ya kitaalam kuhusu suala zima la Bandari ya Bagamoyo. Ndio "ripoti" au makala ya kwanza ambayo iko balanced, ambayo inafungua mlango wa mjadala mpana na njia ya kufikia maamuzi sahihi.

Kuna kifungu kimoja cha Biblia kinasema - Mithali 29:12
"MWENYE KUTAWALA AKISIKILIZA UONGO
BASI WATUMISHI WAKE WOTE WATAKUWA WAOVU"

Maneno hayo yalitimia kikamilifu kwa hayati Rais Magufuli na Serikali yake. Alipenda sifa na kusikia mambo anayopenda kusikia hivyo basi watumishi wake (washauri, wapambe na mashabiki wake) waligeuka waovu.
Ni kama ulivyosema walikuwa wazalendo kwa Magufuli na CCM lakini ni maadui kwa maendeleo na maslahi ya Nchi ya Tanzania.
Tuwapuuze. Tuwapinge. Tusonge mbele.

Endelea kuleta nondo ili tuweze kufanya michango chanya kwa mustakabali wa nchi yetu. Ubarikiwe sana Chige!
 
Hivi nyie watu huwa hamsikii mpaka damu iwatoke masikioni eeh? Tumeshasema miradi ya wizi wizi na ujanja ujanja iliishia wakati wa Kikwete, kuanzia Magu na kuendelea tunataka kila kitu wazi wazi. Wakati wa kutuchezea akili ulienda na kikwete. Tunataka miradi ya win win situation.
Btw, ardhi yetu ya bagamoyo na uhuru wetu vina thamani zaidi kuliko maisha ya huyo mtoto aliyekamatwa na sembe.
Jiwe alibungua akili zenu mmebaki kumiliki vichwa vitupu.....Uwanja mliojenga huko Chato una faida gani sasa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Wajinga wengi huwa mnawaza namna hii HOJA haipigwi RUNGU jibu hoja zake kwa details kama alivyofanya yeye

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Hana hoja, bali ameegemea upande mmoja wa kumtetea mchina na kujaribu kuponda na kuonesha kwamba Magufuli alikuwa mjinga.

Tumemwambia una maktaba uweke hapa kusapoti mada yako? Hana!

Hilo tu kwamba na yeye kaandika tu kwa hisia mada inakuwa ni ya kipumbavu.
 
Jiwe alibungua akili zenu mmebaki kumiliki vichwa vitupu.....Uwanja mliojenga huko Chato una faida gani sasa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Kwa sababu chato kumejengwa uwanja basi na bagamoyo nako tuingie hasara nyingine?

Huoni kama wewe ndio umebunguliwa hilo bichwa?
 
Bahati mbaya haujafafanua namna gani Ugiriki ilikubalina kwa staili ipi na Mchina namna ya kuendesha bandari hiyo. Pia sioni maelezo ya Ugiriki inanufaika vipi kimapato kutokana na umiliki wa mchina kwenye bandari hiyo kwa 67% .
Kimsingi hapo nimeshasema tayari kwa sababu, hapo umiliki wa bandari ya Piraeus ni wa Ugiriki na China, huku kila mmoja akifaidika na kiwango chake cha umiliki!

Manufaa ya ziada kwa Ugiriki ni kodi, kama nilivyosema posts za awali kwamba, kodi siku zote ni mali ya serikali ingawaje pia serikali inaweza kusamehe baadhi ya kodi!

Wakati wa operation, kodi kubwa inayosamehewa na serikali ni income tax. Kwa mfano, bandari ya Piraeus ikitengeneza faida ambayo $100 zinatakiwa kuwa gawio, ina maana China atapata $67.

Wachina walivyo, kwenye hiyo $67 yake, atataka asikatwe income tax. Study ya Piraeus pia inaonesha China ilitaka isamehewe income tax, lakini hakuna taarifa za ndani kuangalia ni income tax ipi, kwa sababu bandarini kuna income generation sources nyingi!
Tusisahau namna Wachina walivyokuwa wana'handle' ndugu zetu kwenye makampuni yao enzi za awamu ya "nne". Ukumbuke sipingi BRI.
Bila shaka unamaanisha Wachina huwa wanalipa kiduchu! Siwezi kukubali wala kukataa kwa hilo, lakini jambo lililo wazi ni kwamba, ajira zitakuwepo bila kujali ujira utakuwaje!
Mkuu, hapa hapa unachafua mada yako bila sababu za maana. Kwa hiyo, unataka kuuaminisha umma kuwa uwanja wa ndege wa Chato utawanufaisha watanzania wanaoishi Chato pekee!?
Tafadhali, jielekeze kwenye kusimamia objectivity katika hili.
Hata hao wana-Chato wenyewe hautawanufaika kivile na uwanja huo!!

Na nimetoa mfano wa Chato kwa sababu, boths projects zina tuhuma za kuwapo kutokana na marais wa miradi husika!

Kwamba, Bagamoyo Port si lolote si chochote lakini JK aliutaka ili kupendelea kwao Bagamoyo!

Na hicho ndicho kinasemwa kuhusu Uwanja wa Chato!!

Na ndipo nikasema, Bandari ya Bagamoyo ni tofauti na Uwanja wa Chato, kwa sababu,mosi, bandari huwa zinatoa ajira nyingi sana tofauti na uwanja wa ndege, hususani kama uwanja wenyewe ni wa aina ya Uwanja wa Chato!

Na kwavile kwa kawaida bandari hutoa ajira nyingi, na hapo hapo kutakuwa na Industrial Complex, haina ubishi kwamba pale kutakuwa na ajira nyingi zitakazonufaisha Watanzania wote, kama ilivyo Bandari ya Dar es salaam!
 
Chige asante sana kwa uzi uliosheheni nyama na virutubisho muhimu.

Nikiri wazi kuwa hii ndio mara ya kwanza kupata au kusoma maelezo ya kina na ya kitaalam kuhusu suala zima la Bandari ya Bagamoyo. Ndio "ripoti" au makala ya kwanza ambayo iko balanced, ambayo inafungua mlango wa mjadala mpana na njia ya kufikia maamuzi sahihi.

Kuna kifungu kimoja cha Biblia kinasema - Mithali 29:12
"MWENYE KUTAWALA AKISIKILIZA UONGO
BASI WATUMISHI WAKE WOTE WATAKUWA WAOVU"

Maneno hayo yalitimia kikamilifu kwa hayati Rais Magufuli na Serikali yake. Alipenda sifa na kusikia mambo anayopenda kusikia hivyo basi watumishi wake (washauri, wapambe na mashabiki wake) waligeuka waovu.
Ni kama ulivyosema walikuwa wazalendo kwa Magufuli na CCM lakini ni maadui kwa maendeleo na maslahi ya Nchi ya Tanzania.
Tuwapuuze. Tuwapinge. Tusonge mbele.

Endelea kuleta nondo ili tuweze kufanya michango chanya kwa mustakabali wa nchi yetu. Ubarikiwe sana Chige!
Umenyegeshwa na maneno mengii lakini hamna kitu kwenye hili andiko lake.

Tunataka wanaotetea na kupinga huo mradi waweke mkataba hapa ili tuuone tujue wapi pabaya na wapi pazuri. Vinginevyo wote wanakuwa wapuuzi tu.
 
Hana hoja, bali ameegemea upande mmoja wa kumtetea mchina na kujaribu kuponda na kuonesha kwamba Magufuli alikuwa mjinga.
Hilo ndo tatizo lako! Hutaki kisemwe chochote unachohisi ni negative kwa JPM!

Pole sana, na kazi unayo ndugu mwananchi mzalendo!!!
 
Umenyegeshwa na maneno mengii lakini hamna kitu kwenye hili andiko lake.

Tunataka wanaotetea na kupinga huo mradi waweke mkataba hapa ili tuuone tujue wapi pabaya na wapi pazuri. Vinginevyo wote wanakuwa wapuuzi tu.
Bwah! Bwah! Bwah! Bwah! Angalia unavyohangaika!!!

Huyo Kakoko ambae aliwaambia Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30, aliwaonesha mkataba unaothibitisha madai yake?!
 
Hilo ndo tatizo lako! Hutaki kisemwe chochote unachohisi ni negative kwa JPM!

Pole sana, na kazi unayo ndugu mwananchi mzalendo!!!
Wewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.

Na kazi unayo sana ndugu mwanachi beberu wa kichina
 
Mada yako imeegemea upande mmoja.

Unataka tusiiamini selikali ambayo ndio yenye mkataba, ila unataka tukuamini wewe unae watetea wachina ambae huna mkataba na umeandika kwa kudhani.

Sasa ili mada yako ionekane ya maana weka mkataba hapa.
Serikali ipi unayotaka iaminike?!

Huyo Kakoko mwenyewe ana tuhuma za wizi, na ndio maana kasimamishwa! Sasa unataka tumwamini mtu mwenye tuhuma za wizi?!
 
Wewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.

Na kazi unayo sana ndugu mwanachi beberu wa kichina
kesha kufa kama wewe mzalendo ungezikwa nae bro
 
Wewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.

Na kazi unayo sana ndugu mwanachi beberu wa kichina
Pole sana!!

Kwa mfano, ulitaka niseme kitu positive kipi?! Kununua ndege? Kujenga Chato International Airport?! Kipi hasa ambacho ulitarajia nikiseme?!
 
Bwah! Bwah! Bwah! Bwah! Angalia unavyohangaika!!!

Huyo Kakoko ambae aliwaambia Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30, aliwaonesha mkataba unaothibitisha madai yake?!
Ndio maana nikasema wote nyie, wewe na kakoko ni wapumbavu maana mnakuja tu na blaa blaa ya kila mtu kutetea upande wake unaompa kula badala ya kuleta mkataba tuusome.

We huoni % kubwa ya wachangiaji hapa wanataka mlete mkataba badala ya kuja na hizi porojo tupu?
 
Back
Top Bottom