- Thread starter
- #141
Masharti kama yapi?!Watu wa JK mnapoteza muda, hakuna asiyeona umuhimu wa huo mradi; Tatizo masharti ya mradi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Masharti kama yapi?!Watu wa JK mnapoteza muda, hakuna asiyeona umuhimu wa huo mradi; Tatizo masharti ya mradi
Halafu wanaboa sana wanavyojiona eti wao ndo wazalendo sana kuliko wengine wakati kimsingi, "uzalendo" wao upo kwa Mwendazake na wala sio kwa taifa!Kwa kifupi ni WANAFIKI wanaotaka kuvaa joho lisilowatosha UZALENDO...
Mada imezidi upeo wao...
Bahati mbaya haujafafanua namna gani Ugiriki ilikubalina kwa staili ipi na Mchina namna ya kuendesha bandari hiyo. Pia sioni maelezo ya Ugiriki inanufaika vipi kimapato kutokana na umiliki wa mchina kwenye bandari hiyo kwa 67% .Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!
Tusisahau namna Wachina walivyokuwa wana'handle' ndugu zetu kwenye makampuni yao enzi za awamu ya "nne". Ukumbuke sipingi BRI.Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!
Mkuu, hapa hapa unachafua mada yako bila sababu za maana. Kwa hiyo, unataka kuuaminisha umma kuwa uwanja wa ndege wa Chato utawanufaisha watanzania wanaoishi Chato pekee!?Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?
Pasco,Mkuu Chige , Thanks for this. Kuna Watanzania wenzetu uwezo wao wa kuona mbali ni mwisho wa pua zao!. Tunajenga SGR, ile treni ina uwezo wa kuvuta mabehewa zaidi ya 100, ya 40ft container zikiwa double, zimepakatana!. SGR ukikamilika, huo mzigo wa kubebwa na SGR ili ijiendeshe kwa faida utatoka wapi?.
Niliuliza hili swali
Sikuwahi kujibiwa!.Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...
Wanabodi Kuna msemo usemao "ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji tia maji" Tanzania tunajenga reli ya SGR, wenzetu Kenya wametangulia, ila reli yao imeanza kwa kuwa ni a white elephant. Jee kuna haja ya sisi Watanzania tujifunze kwa wenzetu, kuiepusha reli yetu kuwa tembo mweupe, au wao...www.jamiiforums.com
Jibu la mzigo wa kuishibisha reli ya SGR ni bandari ya Bagamoyo.
P
Mada yako imeegemea upande mmoja.Jadili hoja, kwa sababu ni mjinga tu ndie anaweza kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba!!
Wajinga wengi huwa mnawaza namna hii HOJA haipigwi RUNGU jibu hoja zake kwa details kama alivyofanya yeyeMkuu umelipwa pesa ngapi ili kuupugia chapuo hivi huu mradi?,
Jiwe alibungua akili zenu mmebaki kumiliki vichwa vitupu.....Uwanja mliojenga huko Chato una faida gani sasaHivi nyie watu huwa hamsikii mpaka damu iwatoke masikioni eeh? Tumeshasema miradi ya wizi wizi na ujanja ujanja iliishia wakati wa Kikwete, kuanzia Magu na kuendelea tunataka kila kitu wazi wazi. Wakati wa kutuchezea akili ulienda na kikwete. Tunataka miradi ya win win situation.
Btw, ardhi yetu ya bagamoyo na uhuru wetu vina thamani zaidi kuliko maisha ya huyo mtoto aliyekamatwa na sembe.
Hana hoja, bali ameegemea upande mmoja wa kumtetea mchina na kujaribu kuponda na kuonesha kwamba Magufuli alikuwa mjinga.Wajinga wengi huwa mnawaza namna hii HOJA haipigwi RUNGU jibu hoja zake kwa details kama alivyofanya yeye
Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Kwa sababu chato kumejengwa uwanja basi na bagamoyo nako tuingie hasara nyingine?Jiwe alibungua akili zenu mmebaki kumiliki vichwa vitupu.....Uwanja mliojenga huko Chato una faida gani sasa
Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Kimsingi hapo nimeshasema tayari kwa sababu, hapo umiliki wa bandari ya Piraeus ni wa Ugiriki na China, huku kila mmoja akifaidika na kiwango chake cha umiliki!Bahati mbaya haujafafanua namna gani Ugiriki ilikubalina kwa staili ipi na Mchina namna ya kuendesha bandari hiyo. Pia sioni maelezo ya Ugiriki inanufaika vipi kimapato kutokana na umiliki wa mchina kwenye bandari hiyo kwa 67% .
Bila shaka unamaanisha Wachina huwa wanalipa kiduchu! Siwezi kukubali wala kukataa kwa hilo, lakini jambo lililo wazi ni kwamba, ajira zitakuwepo bila kujali ujira utakuwaje!Tusisahau namna Wachina walivyokuwa wana'handle' ndugu zetu kwenye makampuni yao enzi za awamu ya "nne". Ukumbuke sipingi BRI.
Hata hao wana-Chato wenyewe hautawanufaika kivile na uwanja huo!!Mkuu, hapa hapa unachafua mada yako bila sababu za maana. Kwa hiyo, unataka kuuaminisha umma kuwa uwanja wa ndege wa Chato utawanufaisha watanzania wanaoishi Chato pekee!?
Tafadhali, jielekeze kwenye kusimamia objectivity katika hili.
Umenyegeshwa na maneno mengii lakini hamna kitu kwenye hili andiko lake.Chige asante sana kwa uzi uliosheheni nyama na virutubisho muhimu.
Nikiri wazi kuwa hii ndio mara ya kwanza kupata au kusoma maelezo ya kina na ya kitaalam kuhusu suala zima la Bandari ya Bagamoyo. Ndio "ripoti" au makala ya kwanza ambayo iko balanced, ambayo inafungua mlango wa mjadala mpana na njia ya kufikia maamuzi sahihi.
Kuna kifungu kimoja cha Biblia kinasema - Mithali 29:12
"MWENYE KUTAWALA AKISIKILIZA UONGO
BASI WATUMISHI WAKE WOTE WATAKUWA WAOVU"
Maneno hayo yalitimia kikamilifu kwa hayati Rais Magufuli na Serikali yake. Alipenda sifa na kusikia mambo anayopenda kusikia hivyo basi watumishi wake (washauri, wapambe na mashabiki wake) waligeuka waovu.
Ni kama ulivyosema walikuwa wazalendo kwa Magufuli na CCM lakini ni maadui kwa maendeleo na maslahi ya Nchi ya Tanzania.
Tuwapuuze. Tuwapinge. Tusonge mbele.
Endelea kuleta nondo ili tuweze kufanya michango chanya kwa mustakabali wa nchi yetu. Ubarikiwe sana Chige!
Hilo ndo tatizo lako! Hutaki kisemwe chochote unachohisi ni negative kwa JPM!Hana hoja, bali ameegemea upande mmoja wa kumtetea mchina na kujaribu kuponda na kuonesha kwamba Magufuli alikuwa mjinga.
Bwah! Bwah! Bwah! Bwah! Angalia unavyohangaika!!!Umenyegeshwa na maneno mengii lakini hamna kitu kwenye hili andiko lake.
Tunataka wanaotetea na kupinga huo mradi waweke mkataba hapa ili tuuone tujue wapi pabaya na wapi pazuri. Vinginevyo wote wanakuwa wapuuzi tu.
Wewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.Hilo ndo tatizo lako! Hutaki kisemwe chochote unachohisi ni negative kwa JPM!
Pole sana, na kazi unayo ndugu mwananchi mzalendo!!!
Serikali ipi unayotaka iaminike?!Mada yako imeegemea upande mmoja.
Unataka tusiiamini selikali ambayo ndio yenye mkataba, ila unataka tukuamini wewe unae watetea wachina ambae huna mkataba na umeandika kwa kudhani.
Sasa ili mada yako ionekane ya maana weka mkataba hapa.
kesha kufa kama wewe mzalendo ungezikwa nae broWewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.
Na kazi unayo sana ndugu mwanachi beberu wa kichina
Pole sana!!Wewe hutaki kisemwe chochote ambacho ni positive kwa JPM, na hili nmeona umelirudia mara nyingi sana kwenye hii mada yako.
Na kazi unayo sana ndugu mwanachi beberu wa kichina
Ndio maana nikasema wote nyie, wewe na kakoko ni wapumbavu maana mnakuja tu na blaa blaa ya kila mtu kutetea upande wake unaompa kula badala ya kuleta mkataba tuusome.Bwah! Bwah! Bwah! Bwah! Angalia unavyohangaika!!!
Huyo Kakoko ambae aliwaambia Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30, aliwaonesha mkataba unaothibitisha madai yake?!