Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mkuu Chige , Thanks for this. Kuna Watanzania wenzetu uwezo wao wa kuona mbali ni mwisho wa pua zao!. Tunajenga SGR, ile treni ina uwezo wa kuvuta mabehewa zaidi ya 100, ya 40ft container zikiwa double, zimepakatana!. SGR ukikamilika, huo mzigo wa kubebwa na SGR ili ijiendeshe kwa faida utatoka wapi?.
Niliuliza hili swali
Sikuwahi kujibiwa!.
Jibu la mzigo wa kuishibisha reli ya SGR ni bandari ya Bagamoyo.
P
Well and good. Lakini tuliaminishwa vinginevyo na tukapiga makofi na vifijjo na kuona everything was wrong au ni mimi sikuelewa?
 
Hoja yako imeegemea upande mmoja.

Unasema huu mradi una faida sana kwetu tofauti na wanavyotuaminisha selikali kwamba mkataba umekaa kinyonyaji.

Tumekuuliza una mkataba tuone jinsi tutakavyofaidika ili tuzidi kuwadharau hawa seilikali? Huna.

Hivyo huu unabaki kuwa upuuzi kama ulivyo upuuzi mwingine tu.
Serikali gani hiyo unayoiamini? Hii serikali ambayo waziri Mkuu anadanganya umma tena akiwa kwenye Nyumba za ibada ndo Una taka tuiamini?
 
Porojo at work!
wa
Kila mwenye akili timamu anafahamu Jiwe nae ni miongoni mwa wezi wakubwa waliopata kutokea nchi hii.

Katumia billions of TZS kununua ndege, hata nikikuuliza wewe na ukoo wako wote ni wapi tenda ilitangazwa, hamuwezi kuwa na majibu! Ili asikaguliwe, akaamua kuhamishia Wakala wa Ndege za Serikali Ikulu, huku akiacha misukule yake ikiimba nyimbo za mapambio!!

Halafu hivi hujishtukii unavyosema "tunataka kila kitu wazi wazi" wakati utawala wa JPM ndio uliongoza kuficha yale yanayofanyika huko serikalini?!
Dhambi yenu kwa watanzania ni kubwa, haitapita bure mtailipa.
Sisi siyo wajinga...

Hatujasahau mnakuja na propanganda za kitoto hivi?!!
Mchina ni bepari tu kama Marekani na mabebeberu wengine.
 
Bandiko lako limekaa kisomi sana sijui kama hapa akina Wakudadavua, NdegeJohn na kifupikirefu kama watachomoka.
😀😀😀😀wote wamejikausha . amebaki #Crimea yeye anataka aoneshwe mkataba tu 🤡🤡🤡🤡
 
Nyie pigeni debe mkumbuke uo mkataba utakuja kua kama mikataba ya Madin Yan wazee wetu watakua wamesha sain wajukuu wakija kuzinduka na akil zao apo Baadae nakutaka kudai haki yao watakuja kupelekwa Miga Na hawato amin Macho yao tusiwe na Tamaa kama Ile Bandar ni muhim kwa mnavyo ielezea sidhan kama nchi ukiamua kuweka fungu hata la miaka 10 kwa ajil ya Bandar tu kama itashindwa tujengen Bandar ya uwezo wetu
 
Pili, lakini pia inaweza ikajengwa kwa mkopo. Hapo kwenye mkopo, ndipo China ilisema itaikopesha TZ. Lakini kama ujuavyo unapotaka kukopa unakopa kwa masharti. Kama hukubaliani na masharti, mwenye pesa hawezi kukupa. Lakini mkopaji pia lazima aangalie kama anayamudu masharti. Kama masharti ni magumu saana, huwezi kukopa. Na hapo ndipo iliyonekana kuwa masharti ya Mchina ni magumu mno. Kuna nchi ziliwahi kukopeshwa kwa mashrarti kama hayo na sasa zinajuta.
Mkuu ksk, nimesoma andiko lako, lakini nadhani kuna mambo uliyoandika hayako sawa.

Moja ni hilo hapo nililo-'quote'.

Siyo sahihi kusema Mchina "anatukopesha" pesa tujenge bandari ya Bagamoyo. Mchina anataka ajenge bandari ya Bagamoyo, na aiendeshe yeye mwenyewe aonavyo inafaa.
chige, hebu njoo hapa ulisemee hili, kama una uelewa tofauti.

Pili, unapokosea pia, mimi sikusoma popote alipodai mleta mada kwamba yeye ndiye alihusika na kutayarisha "Review", hapa nadhani unachanganya mambo mawili tofauti. Huyu mbeba mikoba anaweza akawa ndiye anaanda 'literature review' kwa maelekezo ya mtafiti mwenyewe. Anatayarisha na pengine kutafuta maandiko yanayotakiwa kupitiwa (kusomwa) katika uandaaji wa "Review", kama ndiyo 'outcome' ya utafiti unaofanywa.

Mkuu chige, hili nalo linakuhitaji ulitolee ufafanuzi..

Kuhusu Kikwete kukamilisha mkataba kabla hajaondoka. Hili nalo linaweza kuwa na sababu zake.

Nilipata kusikia kwamba hapakuwa na muda wa kutosha (uliokuwa umesalia) katika ngwe yake kukamilisha hii kazi.

Na kwa kweli isingekuwa busara kwa kiongozi kuharakisha mradi mkubwa kama ule kana kwamba hapatakuwepo na serikali inayokuja kuendeleza alipoachia yeye. Hata hivyo kufanya hivyo kungefanya watu watilie mashaka sana nia yake ya kufanya haraka kiasi hicho, na hasa ikibainika kwamba mkataba ulikuwa ni wa hovyo.
Wewe usidhani hawa viongozi hawajali 'legacy' zao, hata baada ya kutoka madarakani. Hakuna kiongozi anayetaka kuacha sifa mbaya kwenye historia ya nchi aliyoiongoza.
 
SEHEMU YA PILI.

Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Wachina Watachukua Mapato YOTE ya Bandari ya Bagamoyo.

Hii ni moja ya hoja zinazotolewa na Wazalendo wetu wanaopinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari, Deusdedit Kakoko nae alipata kusema “…Wachina wanataka kuchukua mapato yote, na wanataka wasilipe kodi kwa miaka 30.”

Ukweli ni kwamba, haya ni madai ya kushangaza!

Ni madai ya kushangaza kwa sababu ni jambo lisiloingia akilini. Na ikitokea Wachina wakachukua MAPATO YOTE basi Tanzania tutaweka historia mpya duniani kwa sababu hakuna kitu kama hicho popote pale duniani!

Labda niseme jambo moja! Aya yangu hiyo hapo juu ni namna tu ya kusema kiungwana kwamba MADAI HAYO NI UONGO!

Kakoko kasema Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30! Hata hivyo, hatuambii ni kodi ya aina gani wanayotaka wasamehewe!

Kubwa zaidi, maelezo ya Kakoko yalikuwa yamekaa ki-propaganda mno… propaganda zile zile za ki-MATAGA za kujifanya wao ndo Wazalendo sana na wana uchungu sana na hii nchi wakati ni WANAFIKI tu, ambao “uzalendo” wao ulikuwa kwa JPM, na sio kwa nchi!

Ni kutokana na uongo huu wa Kakoko ndo maana haikushangaza kwa mara ya kwanza kuwaona Wachina wakioka mbele na kumshutumu Kakoko kwamba ni MWONGO.

Kwa mfano, gazeti la The Citizen la October 28, 2019 lilimnukuu Mwakilishi wa Uwekezaji wa China Merchant Group, Mr. Moosa Mao akisema:-


Na hata kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mr. Mao aliandika:-

View attachment 1765244

China Merchant Group ndio walitarajiwa kuwekeza kwenye Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hapa tuweke kumbukumbu sawa linapokuja suala la kodi kwa kuangalia muktadha wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Katika hali ya kawaida, kutakuwa na awamu mbili zinazohusiana na kodi kwenye mradi huu.

Awamu ya kwanza ni wakati wa shughuli za ujenzi wa bandari, na awamu ya pili ni pale bandari itakapoanza kufanya kazi.

Wakati wa ujenzi, tunatarajia vifaa vingi vitaagizwa kutoka nje, ingawaje tutakuwa Viumbe wa Ajabu sana endapo tutaruhusu uingizaji hadi wa vifaa ambavyo wenyewe tunavyo, kama vile saruji.

Kuhusu hilo la vifaa, hapa Mchina namtarajia atakuwa ameomba asemehewe kodi ya uingizaji wa hivyo vifaa!

Na kwa bahati, hatakuwa amefanya dhambi yoyote kwa sababu Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, yaani VAT Sura ya 148, na Sheria ya Fedha ya mwaka 2017, 2018 na 2019 zinatoa mwanya kwa Mwekezaji kuomba msamaha wa kodi “on imported capital goods”.

Hata ukiingia kwenye tovuti kuu ya serikali utakuta maneno haya:-


Hivyo, hapo utaona wazi kwamba ni suala la kisheria! Na jambo kama hilo sio Tanzania tu bali sehemu mbalimbali duniani huwa wanafanya hivyo ili kuvutia uwekezaji!!

Kitaalamu, suala hilo linaitwa Tax Incentives. Na hata uki-Google “Tax Incentives in Tanzania”, moja kwa moja utakutana na link ya TRA ikiwa juu kabisa ya matokeo ya utafutaji; yaani Google Search Results!

Suala la kodi na ushuru bandari itakapoanza kufanya kazi.

Kama nilivyosema hapo awali, Mhandisi Kakoko alituambiwa “Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30,” huku Wazalendo wengine wakituambia TRA hawataruhusiwa hata kutia pua hapo bandarini!

Hapa ieleweke kwamba, popote pale duniani kodi ni MALI YA SERIKALI, na ndio maana, ukisoma hiyo screenshot ya Twitter kutoka kwa Moosa Mao, amekanusha suala la eti TRA hawataruhusikiwa kukusanya kodi!

Na ndio maana, wewe milikishwa ekari 1000 na baba yako, kisha tumia pesa zako mwenyewe kufanya uwekezaji bila kuomba hata senti moja kutoka popote pale!

Pamoja na yote hayo, ukimaliza tu uwezekaji wako na kuanza kufanya biashara, TRA wanakuwa wageni wako wa kudumu, ingawaje hukuchangiwa chochote na yeyote!

Lakini kwa upande mwingine, popote pale duniani, serikali huwa zinasamehe baadhi ya kodi. Bandari ya Bagamoyo ikishaanza kufanya kazi, tunatarajia kuwepo angalau kodi zifuatavyo:-

  • Kodi ya Ongezeko la Thamani… VAT on imported goods
  • Kodi ya Mapato (Income Tax)
  • Ushuru wa Uingizaji Bidhaa (Import Duty)
  • Ushuru wa Forodha, na zingine.
Sasa basi, tuseme wewe na mimi, or anyone ameagiza magari au bidhaa yoyote ambayo sio miongoni mwa bidhaa zilizo kwenye kundi la msamaha wa kodi!

Hilo likifanyika, Importer atalazimika kulipa angalau moja ya kodi nilizotaja hapo juu! Kodi hiyo ni LAZIMA IKUSANYWE NA TRA kwa sababu, kama nilivyosema awali, always, Kodi ni Mali ya Serikali.

Sasa je, kuna uwezekano Mchina akataka msamaha wa kodi baada ya bandari kufanya kazi?

Jibu ni NDIYO!

Kutokana na uzoefu niiopata kutoka kuwa Mbeba Mikoba wa Beberu, na kwa kuangalia “case studies” za bandari zingine ambako Mchina amewekeza, hapo kuna uwezekano mkubwa Mchina akaomba msamaha wa Income Tax. HOW?

Bandari ikishaanza kufanya kazi, Mchina atakuwa anatoa huduma kadhaa kama vile kuhifadhi mizigo, kupandisha na kupakuwa mizigo, kuzitoza meli ambazio zitakuwa zinafunga nanga hapo bandarini, n.k.

Kwa kutoa huduma hizo, ina maana Mchina atakuwa analipwa pesa!! Katika mazingira ya kawaida, pesa anazopata ni mapato yanayostahili kukatwa kodi!

Ni hiyo kodi itakayotokana na hizo huduma ndiyo ambayo sina shaka Mchina atataka asamehewe!! Na huu ndio ukweli ambao kwa makusudi, Mzalendo Kakoko hakutaka kusema ukweli, na badala yake akafanya majumuishi kwamba Mchina anataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, bila kutaja ni kodi ipi!

Katika hili la kodi, nililazimika kumtumia email yule Researcher niliyekuwa nae, kwa sababu mimi binafsi sikupata fursa ya kuonana na watendaji wa serikali!

Nililazimika kumtumia email na kumuuliza ingawaje tayari nilishakuwa nafahamu majibu ya maswali yangu. Hata hivyo, nilitaka tu kujiriidhisha kutoka kwake, kwa sababu yeye ni mzoefu sana kwenye haya mambo ya uwekezaji duniani!

Jibu lake lilikuwa hili hapa chini:-

View attachment 1765245
Swali hilo nilimuuliza miaka 2 iliyopita, na mtaona jibu lake linaenda sawa na jibu la Moosa Mao!

Aidha, miongoni mwa maswali ambayo watu wamekuwa wakijiuliza ni kwamba: Sasa kama TRA watakuwa wanachukua kodi, Mchina atarudisha vipi pesa yake!

Jibu la hilo swali unatakiwa kujiuliza: Je, Mamlaka ya Bandari huwa wanakusanya kodi? Kama hawakusanyi, je mapato yao yanatoka wapi? Jibu la swali la pili ndilo jibu la swali la Mchina atarudisha vipi mapato yake!

Umetumwa? Kama ulikuwa unamfanyia beberu Research Literature Review, sie hatutaki huo mradi wa Bagamoyo, for the sake of National Interest, hatutaki huo Mradi wa kijambazi wa Kichina. Kama umetumwa umepotea, rudisha hizo taarifa kwa waliokutuma, mnataka kukausha nchi yetu..
 
Umetumwa? Kama ulikuwa unamfanyia beberu Research Literature Review, sie hatutaki huo mradi wa Bagamoyo, for the sake of National Interest, hatutaki huo Mradi wa kijambazi wa Kichina. Kama umetumwa umepotea, rudisha hizo taarifa kwa waliokutuma, mnataka kukausha nchi yetu..
NONSENSE!
 
NONSENSE!

Shithole black kid... Ww unawajua wachina kuliko mie.. Idiot..!! Mkataba unaujua au unaongea stupid issues zako hapa, eti mtaalam wa literature review, ukajiona mtaalam wa mikataba, you are lost kid.. Pumbaf
 
Shithole black kid... Ww unawajua wachina kuliko mie.. You an idiot..!! Mkataba unaujua au unaongea stupid issues zako hapa, eti mtaalam wa literature review, ukajiona mtaalam wa mikataba, you are lost kid.. Pumbaf
NONSENSE!
 
Dhambi yenu kwa watanzania ni kubwa, haitapita bure mtailipa.
Sisi siyo wajinga...

Hatujasahau mnakuja na propanganda za kitoto hivi?!!
Mchina ni bepari tu kama Marekani na mabebeberu wengine.
Jadili mada, kama imekuzidi kimo, piga kimya!
 
Ndugu yangu Kalamu1,

Kama ulivyom-quote ksk na kunitaka nifafanue kipande ulichom-quote! Nami nitaongezea mengine kutoka kwenye andiko lake!

Mosi, inaonesha wazi kwamba hakusoma au amesoma juu juu, na ndo maana kuanza na kuanza tu, ameanza na habari za mkopo!!

ksk, ujenzi wa bandari peke yake ulipangiwa USD 10 Billion! Hiyo ni pesa nyingi sana!! Hiyo ni 30% ya bajeti yetu ambayo hata hivyo pesa zinapotolewa hazifikii! Kwa maana nyingine, tukisema kiasi halisi cha bajeti ambacho serikali imekuwa ikitoa kwa taasisi, USD 10B inaweza kuwa 50% ya pesa inayotolewa na serikali kwa mwaka ku-finance budget!

Nimekupa maelezo hayo uone ni namna gani pesa hiyo ilivyo nyingi! Na kwa wingi huo, hakuna taasisi duniani inayoweza ku-risk kutoa mkopo wa USD 10 Billlion kwa nchi maskini!

With respect to our research uliyojaribu kuni-undermine, Mchina ametoa mikopo Sri Lanka, Greece, na Djibouti... hizo ni case studies ingawaje kupo kwingine!

Changanya mikopo ya nchi hizo 3 bado thamani yake haifiki pesa iliyokusudiwa kujengewa Bagamoyo!

Kutokana na ukweli huo, ungesoma ungekuta nimesema wazi mradi ulitakuwa kuwa financed na BOT Scheme... Build-Operate-Transfer. Kote duniani, BOT inamfanya Investor agharamie (Build) mradi mzima, akishamaliza, anauendesha (Operate) kwa miaka kadhaa kama mlivyokubaliana.

Ile miaka ikishaaisha, anaurudisha (Transfer) mradi kwa mmiliki halisi!

Hii kitu tunaona kama ajabu lakini hata Bongo inafanyika sana na wafanyabiashara!!

Kwahiyo hapo hakuna suala la mkopo bali Mwekezaji anagharamia mradi kwa "pesa zake"!

Faida atakayopata mwekezaji ni mapato (SIO KODI) yanayotokana na huduma mbalimbali atakazotoa hapo bandarini! Atatoza meli zinazofunga gati, atatoza gharama za upakiaji na upakuaji mizigo, atatoza gharama za kuhifadhi mizigo, n.k!

Kwa kifupi, atapata kile kama ambacho TPA au TICTS anapata leo hii, lakini kwa kawaida Mchina huwa anaomba apate msamaha wa kodi ya mapato kwenye hizi pesa anazoingiza!
 
Umetumia nguvu nyingi sana kutushawishi wakati tunamsimamo wetu tayari tangia awali.

Waswahili wanasema kumpigia mbuzi gitaa.
 
Kalamu1 na ksk,

Tunaendelea!

ksk anadai nimedanganya ninaposema niliandika Literature Review! What's the big kwenye kuandika Literature Review hadi ukaona nadanganya?! Hivi kuna mtu ambae anaweza kuwa na angalau shahada moja ya chuo kikuu halafu akashindwa kuandika LR? Au kwavile utafiti ni wa Mzungu?!

Sasa ngoja tu niongeze hapo hapo... sio tu Mzungu bali ni Mzungu Msomi kweli kweli, wala simkaribii hasa ukizingatia kule alikosoma lakini pamoja na yote hayo, bado aliniamini kutokana na mtu wa kati aliyekuwa amemhakikishia uwezo wangu!!!

ksk, aliyekuambia Literature Review ni proposal ni nani?! Ina maana tujaze server kuelimishana kwamba Literature Review sio proposal but just a part of proposal?

Kalamu1, kwamba niliandika kwa maelekezo yake, jibu ni YES ingawaje sio kiiiivile! Amacho kilinisaidia na ku-gain confidence yake kwa haraka ni kwavile tayari alinikuta nina uelewa wa kutosha kuhusu mradi husika!

Hapa JF nimeandika sana kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo hata kabla sijakutana na yule Mzungu! Yeye baada ya kuonana nae, of course, alinipatia English Documents, na akaniachia uhuru wa kutafuta Swahili documents kwa sababu hafahamu Kiswahili!
 
Umetumia nguvu nyingi sana kutushawishi wakati tunamsimamo wetu tayari tangia awali.

Waswahili wanasema kumpigia mbuzi gitaa.
Jamaa kalala na kudamkia humu ndani...sio kwa nguvu hii anayoitumia...ni km hana kazi nyingine zaidi ya huu uzi...yupo kwa kazi maalumu.

Sasa sijajua kwenye huu uzi yupo pekeake au wapo team nzima. na km wapo team nzima kwa maslai ya nani?
Why waste so much energy na time tryn to convice people?
Mwendazake na kakoko walitumia less than 5minutes kutueleza...the guy has spent almost 48hrs tryn to clean up the mess.

Kizuri cha jiuza na kibaya cha jitembeza na debe tupu ndio linalopiga kelele...naona jamaa anautembeza huu mradi, which means huu mradi ni debe tupu nothing in it.
 
Kalamu1 na ksk,

Tuendelee na hoja ya tatu kwamba kwanini JK hakusaini! Hapa mmegusia hoja ya msingi sana manake wale Wazalendo Fake wanakuja hapa na kuanza matusi huku wala hawajui kinajadiliwa nini!

Kwa akili zao za Uzalendo Fake wanadhani JK ndie alisaini mkataba!

sks, kilichomfanya JK asisaini mkataba sio kwa sababu aliuona kaa la moto, bali wakati wake hapakuwa na mkataba wowote uliotakiwa kusainiwa!

Ambacho alifanya JK ni kukutanisha pamoja Investor ambao wana-Include Oman Fund, na baada ya hapo ikasainiwa Agreement Framework on Infructure Development.

Ile Framework ilikuwa ni kama dira ya kila upande kuangalia maslahi yake, na ilikuwa iwe expired mwaka mmoja baadae ambapo JK ingekuwa ameshatoka madarakani!

Baada ya ku-expire ile framework, ndipo walitakiwa kukutana na ku-negotiate na wakikubaliana ndipo mkataba usainiwe!

Mchina kama Mwekezaji, akatoa proposal yake ya nini angetaka kiwe lakini kukubalika au kukataliwa kwa mapendekezo yake ingekuwa ni baada ya ku-expire huo muda, na kwahiyo, ingekuwa utawala mwingine na sio utawala wa JK.

Hivyo basi, niendelee kusisitiza hapakuwa na mkataba wowote uliosainiwa na ndio maana hakuna aliyewahi kusikia kwamba serikali imevunja mkataba na China, bali stori zilizopo ni "serikali yaendelea na majadiliano na China"!

Baada ya expiration period kupita, ndipo China Merchant Group ikakutana na watu wa Serikali ya Magu, na kuanza majadiliano rasmi, ili hatimae ndipo mkataba usainiwe!

Ambacho kinafanywa na hii timu ya serikali, ni kupitia zile proposal za Mchina... zipo walizokubali, na zipo walizokataa na ndo maana hadi kesho hawajafikia tamati!
 
Jamaa kalala na kudamkia humu ndani...sio kwa nguvu hii anayoitumia...ni km hana kazi nyingine zaidi ya huu uzi...yupo kwa kazi maalumu.

Sasa sijajua kwenye huu uzi yupo pekeake au wapo team nzima. na km wapo team nzima kwa maslai ya nani?
Why waste so much energy na time tryn to convice people?

Kizuri cha jiuza na kibaya cha jitembeza na debe tupu ndio linalopiga kelele...naona jamaa anautembeza huu mradi, which means huu mradi ni debe tupu nothing in it.
Na wewe ulivyo zuzu, kila wakati bado unarudi kwenye uzi!! Unaacha kujadili mada, unajadili mtu... VERY STUPDI! Kama mada imekuzidi kimo, ipotezee tu, badala ya kuwa kama mtoto wa kike mpenda majungu!
 
Jamaa kalala na kudamkia humu ndani...sio kwa nguvu hii anayoitumia...ni km hana kazi nyingine zaidi ya huu uzi...yupo kwa kazi maalumu.

Sasa sijajua kwenye huu uzi yupo pekeake au wapo team nzima. na km wapo team nzima kwa maslai ya nani?
Why waste so much energy na time tryn to convice people?

Kizuri cha jiuza na kibaya cha jitembeza na debe tupu ndio linalopiga kelele...naona jamaa anautembeza huu mradi, which means huu mradi ni debe tupu nothing in it.
Huo mradi ungekua na maana kama Bandari za Tanga, Dar na Mtwara zingekua zimeelemewa na mizigo, ila mpaka sasa hazijatumika mpaka ukomo wake, hizo bidhaa zitatoka wapi kama sio hizi hizi zinazokuja kwenye bandari hizo.

Hata kama watajenga viwanda kwenye eneo la mradi kwanini wasijenge sasa kwenye bandari zilizopo na kuziboresha??
 
Back
Top Bottom