SEHEMU YA PILI.
Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Wachina Watachukua Mapato YOTE ya Bandari ya Bagamoyo.
Hii ni moja ya hoja zinazotolewa na Wazalendo wetu wanaopinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari, Deusdedit Kakoko nae alipata kusema “…Wachina wanataka kuchukua mapato yote, na wanataka wasilipe kodi kwa miaka 30.”
Ukweli ni kwamba, haya ni madai ya kushangaza!
Ni madai ya kushangaza kwa sababu ni jambo lisiloingia akilini. Na ikitokea Wachina wakachukua MAPATO YOTE basi Tanzania tutaweka historia mpya duniani kwa sababu hakuna kitu kama hicho popote pale duniani!
Labda niseme jambo moja! Aya yangu hiyo hapo juu ni namna tu ya kusema kiungwana kwamba MADAI HAYO NI UONGO!
Kakoko kasema Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30! Hata hivyo, hatuambii ni kodi ya aina gani wanayotaka wasamehewe!
Kubwa zaidi, maelezo ya Kakoko yalikuwa yamekaa ki-propaganda mno… propaganda zile zile za ki-MATAGA za kujifanya wao ndo Wazalendo sana na wana uchungu sana na hii nchi wakati ni WANAFIKI tu, ambao “uzalendo” wao ulikuwa kwa JPM, na sio kwa nchi!
Ni kutokana na uongo huu wa Kakoko ndo maana haikushangaza kwa mara ya kwanza kuwaona Wachina wakioka mbele na kumshutumu Kakoko kwamba ni MWONGO.
Kwa mfano, gazeti la
The Citizen la October 28, 2019 lilimnukuu Mwakilishi wa Uwekezaji wa China Merchant Group, Mr. Moosa Mao akisema:-
Na hata kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mr. Mao aliandika:-
View attachment 1765244
China Merchant Group ndio walitarajiwa kuwekeza kwenye Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Hapa tuweke kumbukumbu sawa linapokuja suala la kodi kwa kuangalia muktadha wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Katika hali ya kawaida, kutakuwa na awamu mbili zinazohusiana na kodi kwenye mradi huu.
Awamu ya kwanza ni wakati wa shughuli za ujenzi wa bandari, na awamu ya pili ni pale bandari itakapoanza kufanya kazi.
Wakati wa ujenzi, tunatarajia vifaa vingi vitaagizwa kutoka nje, ingawaje tutakuwa Viumbe wa Ajabu sana endapo tutaruhusu uingizaji hadi wa vifaa ambavyo wenyewe tunavyo, kama vile saruji.
Kuhusu hilo la vifaa, hapa Mchina namtarajia atakuwa ameomba asemehewe kodi ya uingizaji wa hivyo vifaa!
Na kwa bahati, hatakuwa amefanya dhambi yoyote kwa sababu Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, yaani VAT Sura ya 148, na Sheria ya Fedha ya mwaka 2017, 2018 na 2019 zinatoa mwanya kwa Mwekezaji kuomba msamaha wa kodi “on imported capital goods”.
Hata ukiingia kwenye
tovuti kuu ya serikali utakuta maneno haya:-
Hivyo, hapo utaona wazi kwamba ni suala la kisheria! Na jambo kama hilo sio Tanzania tu bali sehemu mbalimbali duniani huwa wanafanya hivyo ili kuvutia uwekezaji!!
Kitaalamu, suala hilo linaitwa Tax Incentives. Na hata uki-Google “Tax Incentives in Tanzania”, moja kwa moja utakutana na link ya TRA ikiwa juu kabisa ya matokeo ya utafutaji; yaani Google Search Results!
Suala la kodi na ushuru bandari itakapoanza kufanya kazi.
Kama nilivyosema hapo awali, Mhandisi Kakoko alituambiwa “Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30,” huku Wazalendo wengine wakituambia TRA hawataruhusiwa hata kutia pua hapo bandarini!
Hapa ieleweke kwamba, popote pale duniani kodi ni MALI YA SERIKALI, na ndio maana, ukisoma hiyo screenshot ya Twitter kutoka kwa Moosa Mao, amekanusha suala la eti TRA hawataruhusikiwa kukusanya kodi!
Na ndio maana, wewe milikishwa ekari 1000 na baba yako, kisha tumia pesa zako mwenyewe kufanya uwekezaji bila kuomba hata senti moja kutoka popote pale!
Pamoja na yote hayo, ukimaliza tu uwezekaji wako na kuanza kufanya biashara, TRA wanakuwa wageni wako wa kudumu, ingawaje hukuchangiwa chochote na yeyote!
Lakini kwa upande mwingine, popote pale duniani, serikali huwa zinasamehe baadhi ya kodi. Bandari ya Bagamoyo ikishaanza kufanya kazi, tunatarajia kuwepo angalau kodi zifuatavyo:-
- Kodi ya Ongezeko la Thamani… VAT on imported goods
- Kodi ya Mapato (Income Tax)
- Ushuru wa Uingizaji Bidhaa (Import Duty)
- Ushuru wa Forodha, na zingine.
Sasa basi, tuseme wewe na mimi, or anyone ameagiza magari au bidhaa yoyote ambayo sio miongoni mwa bidhaa zilizo kwenye kundi la msamaha wa kodi!
Hilo likifanyika, Importer atalazimika kulipa angalau moja ya kodi nilizotaja hapo juu! Kodi hiyo ni LAZIMA IKUSANYWE NA TRA kwa sababu, kama nilivyosema awali, always, Kodi ni Mali ya Serikali.
Sasa je, kuna uwezekano Mchina akataka msamaha wa kodi baada ya bandari kufanya kazi?
Jibu ni NDIYO!
Kutokana na uzoefu niiopata kutoka kuwa Mbeba Mikoba wa Beberu, na kwa kuangalia “case studies” za bandari zingine ambako Mchina amewekeza, hapo kuna uwezekano mkubwa Mchina akaomba msamaha wa Income Tax. HOW?
Bandari ikishaanza kufanya kazi, Mchina atakuwa anatoa huduma kadhaa kama vile kuhifadhi mizigo, kupandisha na kupakuwa mizigo, kuzitoza meli ambazio zitakuwa zinafunga nanga hapo bandarini, n.k.
Kwa kutoa huduma hizo, ina maana Mchina atakuwa analipwa pesa!! Katika mazingira ya kawaida, pesa anazopata ni mapato yanayostahili kukatwa kodi!
Ni hiyo kodi itakayotokana na hizo huduma ndiyo ambayo sina shaka Mchina atataka asamehewe!! Na huu ndio ukweli ambao kwa makusudi, Mzalendo Kakoko hakutaka kusema ukweli, na badala yake akafanya majumuishi kwamba Mchina anataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, bila kutaja ni kodi ipi!
Katika hili la kodi, nililazimika kumtumia email yule Researcher niliyekuwa nae, kwa sababu mimi binafsi sikupata fursa ya kuonana na watendaji wa serikali!
Nililazimika kumtumia email na kumuuliza ingawaje tayari nilishakuwa nafahamu majibu ya maswali yangu. Hata hivyo, nilitaka tu kujiriidhisha kutoka kwake, kwa sababu yeye ni mzoefu sana kwenye haya mambo ya uwekezaji duniani!
Jibu lake lilikuwa hili hapa chini:-
View attachment 1765245
Swali hilo nilimuuliza miaka 2 iliyopita, na mtaona jibu lake linaenda sawa na jibu la Moosa Mao!
Aidha, miongoni mwa maswali ambayo watu wamekuwa wakijiuliza ni kwamba: Sasa kama TRA watakuwa wanachukua kodi, Mchina atarudisha vipi pesa yake!
Jibu la hilo swali unatakiwa kujiuliza: Je, Mamlaka ya Bandari huwa wanakusanya kodi? Kama hawakusanyi, je mapato yao yanatoka wapi? Jibu la swali la pili ndilo jibu la swali la Mchina atarudisha vipi mapato yake!