Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Mkuu; Bado hujaelewa, kutambua na kukubali kwamba hapa tulipo ni Tanzania na sio huko ulikotaja? Hata hivyo hujazuiwa kwenda kuishi huko.
Feel FREE to go.
Wapi mkuu wakati pwani ni kwangu. Ushauri bora angesema tuungane kupigania serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenye. Mfano wa jimbo la znz.

Kwa maana kila jimbo itatengeza sheria sawa na kanuni ya kidemokrasia ya wengi hufunga Sheria. Wachache huvumilia.

Na kwamba ukienda Rome tii shera za rome
 
Serikali haifuati dini yoyote, kwa hivyo hatutegemei serikali isome vitabu vya dini zote duniani ili kutunga sheria zake.
Stereotypes:

Serikali yetu inejipambanua ina imani.

Imani ya Ujamaa. Kwani Ujamaa ni imani.

Kimsingi Ujamaa ni imani isiyoamini uwepo wa mungu.

Kimsingi wajamaa wameficha uhalisia kuwa Ujamaa ni upagani.

Je Ujamaa ni universal faith, value and ideology

Hapana.

Je ktk nchi ambao hakuna universal values ni value gn hupaswa kuwa ndio mwongozo wa nchi.

Jibu tunayo case study ya wanafunzi wa kiislam. Waliporuhusiwa wao tu kuvaa uniform with dressing code.

Kwa case study hiyo hiyo inapaswa kutumika kwa idara za polisi na vikosi vya jeshi.

Kwann ninyi wenzetu hamna uwezo wa kuvumilia values za wengine.

Mnataka nchi iongezwe na values za imani ya kipagani pekee. Kwani waislam wakiwa hivyo nanyi mkavaa kwa mujibu wa imani zenu za kipagani unapungukiwa na nini.
 
Hapana; unakosea sana kukazania imani ya dini yako ndio uwe mwongozo wa serikali. Siyo kosa lako tu, kwani wapo wengi hata wakatristo kupenda kutumia serikali kufanikisha imani zao. Ni kosa kuchanganya serikali (ambacho ni chombo cha mabavu) na dini (ambayo inajengwa kwa ushawishi).
 
Serikali ni chombo cha mabavu???? Uko contaminated.

Serikali inaundwa kutokana na chama. Kazi ya chama ni kushawishi makundi mbalimbali yanayounda watanzania kwa kuaccomodate values zao ktk sera na itikadi ya chama husika. Ambapo sera na itikadi hizo ni muhimu zile na universal values. Na ikikosekana basi si vema kuwalazimisha kundi fulani kufata itikadi na imani nyingine ambayo ni kinyume na imani yake.

By the way kila serikali ina imani. Imani ya serikali ya ccm ni Ujamaa. Ujamaa ni imani.

Kama ambavyo dini ni imani.

Hivyo Ujamaa ni dini.

Dini onayopinga uwepo wa Mungu na viambata vyake kama uwepo wa dini (upagani).


Msiwalazimishe watz wote kufata imani ya kipagani. Ni kufuru
 
Sitachangia chochote maana siamini kama uko timamu kichwani.
 
Wazazi wa, miaka hii, kila kitu mnataka under control. Sasa hao watoto wataweza, kweli? Lazima wapitie, kila, hatua, na mavazi ili wakae vizuri kwa, ajili ya, mapambano ya, maisha.
 
Brother hijab siyo sketi au gauni, hivi utaruka vikwazo na gauni? Au kupita juu kamba ?

Hao unaosema tunafahamu sana hadi unaona askari kuvaa hijab tayari basic military training walishatoka huko.

Tuondoe ubishani tuwe serious kabisa na fani.
 
Brother hijab siyo sketi au gauni, hivi utaruka vikwazo na gauni? Au kupita juu kamba ?

Hao unaosema tunafahamu sana hadi unaona askari kuvaa hijab tayari basic military training walishatoka huko.

Tuondoe ubishani tuwe serious kabisa na fani.
Ndugu hebu nambie kwa mfano huko somalia askari wa kike wanavishwa vibukta wakati wa mazoezi.

Hijab ina style nyingi kadiri ya mazingira ya kazi.

Ndio maana ktk andiko langu sijaandika hijab. Nimeandika mavazi au uniform zenye stara.

Ktk mataifa hayo mengine hutumia uniform zenye stara zisizokiuka misingi ya imani za kila kundi.
 
Naumia nini nyoe kwa watz wenzenu ku identify values zao wakati zimeandikwa ktk katiba.

Kwanini tusifate katiba. Kwanini dhana za serikali zinafasiriwa na kada moja sawa na values za imani zao binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…