Maboresho katika sekretarieti ya ajira: Kwanini mtu wa 'degree' asiruhusiwe kuomba kazi za wenye 'diploma'?

Hizi sifa za kijinga ndizo zimelifikisja taifa letu hapa tulipo, aliyetoa hoja ametoa ulinganifu wake ktk eneo na lengo la uzalishaji hapa yuko sahihi wewe unatoa ulinganifu wako ktk eneo la weledi pia huenda uko sahihi. Hapa unathibisha kuwa umekurupuka kutokana na ukweli kuwa duniani kote wazalishaji (nguvu kazi kubwa huandaliwa kwa level ya diploma) na wale wachache hupata degree kwa lengo la kiongozi/utawala.
 
Hii nchi bhana!
Supervisor anataka muwa surbodinate!

Akili zako umeziweka wapi?
 
Hiyo inaitwa Overqualification. Haijawahi kukubalika
 
Msoto noma sana!
 
Jibu kama hili nilijibiwa na customer care mmoja ajira portal. Hawa jamaa bwana wana majibu ya ovyo sana. Issue yangu ilikuwa ni hivi niliuliza watu higher Diploma kwann wanazinguliwa wakiomba nafasi za degree. Na huku na za diploma nako mfumo unagoma. Pia Kushindwa kuweka wazi mtu higher Diploma na advanced diploma tofauti yao ipo wapi. Alichonijibu ni kwamba serikali haiajiri watu wa higher Diploma kama vipi rudi chuo ulichosoma ukawaambie wakupe cheti Cha ordinary diploma uanze kuomba kazi za ordinary diploma. Hii ilishangaza sana. Hawa jamaa wa ovyo sana.
 
Sasa mbona alikujibu vizurii,au wewe ulitaka akupe majibu ganii??
 
Labda na Mimi unisaidiee higher diploma na advanced diploma tofautii yake ni nini??
 
Maake hapo point yake alikuambia serikali haiajirii watu wa higher diploma je? ni kwelii??
 
Mkuu nimekuulza unijibu tofautii ya advanced diploma na higher diploma ni ipii?? Nipe tofautii yake Nina maana yangu
Advanced diploma ilikuwa inatolewa zamani vyuo vya kati. Na ilikuwa inachukua miaka 3. Na ilikoma 2010. Higher diploloma(NTA LEVEL 7) inatolewa mpaka sa hv na vyuo vya kati ambavyo vipo chini ya NACTE na miaka miwili(2) na mara nyingi hupatikana in kesi mtu ameshindwa kukamilisha degree (NTA level 8) kutokana sababu mbalimbali ikiwemo yeye mwenyewe kuomba kuishia hapo. DIT, NIT, ATC wanatoa hii.
 
A
Maake hapo point yake alikuambia serikali haiajirii watu wa higher diploma je? ni kwelii??
Yaah?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…