Maboresho katika sekretarieti ya ajira: Kwanini mtu wa 'degree' asiruhusiwe kuomba kazi za wenye 'diploma'?

Maboresho katika sekretarieti ya ajira: Kwanini mtu wa 'degree' asiruhusiwe kuomba kazi za wenye 'diploma'?

nimesoma Diploma, na nimesoma Degree ya Uhandisi
hii ndiyo tofauti niliyoiona, na najibu kwa upande wa kada yangu

wa Diploma yuko ki hands-on, amesomea praki (na theories) miaka yote X
wa Degree hawezi kava nafasi ya Diploma, maana yeye kule amekunywa theories tupu (tena zisizo na uhalisia kabisa kwenye mazingira ya kazi) , hata wire wa 2.5mm² hajui unafananaje
Ni kweli degrees kawa trained for administration na supervision

Diploma for production
 
Uo ni uroho wa madaraka kwanini ule share ya mwenzio.....mbna kwenye kusoma watu wa Diploma wakiomba kujazia vimiaka kadhaa mnagoma mnataka waanzie zero km wanatoka six
 
Hata

Hata nikiwa usingizini au ndotoni ukaniuliza nani bora kati ya mwenye degree na diploma nikakuambia bora ni mwenye diploma ninase makofi
Nina bint hapa ofisini hajui hata kuandika CV 🤣 , monthly report yenyewe kuandaa ilibidi aanze upya darasa sasa hadi unajiuliza research yake huyu aliandika nini?

bachelor zenu mnazo peana kama peremende huko vyuoni miaka hii,
kwakweli mna haki ya kujitutumua nazo mana ni aibu tu.
 
Ni kweli degrees kawa trained for administration na supervision

Diploma for production
Nadhan wewe sasa ndio umejibu kitaalamu kabisa na umeelewa vyema context ya huu mjadala sio bwana mmoja hapo juu ,

na ninadhani huenda katoka familia ya watu wasio soma ndio maana anaona bachelor kama almasi tena zama hizi !? na hapo huenda hata sifa za masters hana anatusumbua na "pass" tu hapa.
 
Au unakuta Kuna ajira ya certificate ila kwa kuwa mtu uliunga hadi degree ,basi qualifications ya certificate uwezi apply wakati ume attach certificate,dip and bachelor Ila wao Wana consider elimu ya bachelor tu ,dip.au certificate uliyo attach uwezi ku apply ,wabadilishe mfumo.kwa kweli kwa mtu alieanzia certificate hadi degree
Sasa mtu umegraduate varsity na Gamba lako la GPA ya 3.5 and above afu ukalilie ajira ya cheti?lol mbona inakuwa Kama elimu haijakukomboa sasa🤣umelose miaka kibao , duh hii hatare na nusu🤣🤣
 
Nadhan wewe sasa ndio umejibu kitaalamu kabisa na umeelewa vyema context ya huu mjadala sio bwana mmoja hapo juu ,

na ninadhani huenda katoka familia ya watu wasio soma ndio maana anaona bachelor kama almasi tena zama hizi !? na hapo huenda hata sifa za masters hana anatusumbua na "pass" tu hapa.
Hahah na wewe una bachela au mastaz?🤣au diplomacy Kama mimi?🤣🤣🤣
 
Huo ni upumbavu.
Kwahy kisa mahindi yanatoa unga bc tusonge mahindi instead of unga.? Huo c upumbavu.
Kwanza degree zenyewe ni nadharia tuu hvy endeleeni kupambana na degree zenu. Waliowekwa degree na diploma wana akili timamu ingekuwa ni sahihi unavyotaka bc kusingekuwepo na hy diploma.
 
ahida ni wenye degree wakishaajiriwa tu wanawasilisha madai wana degree hivyo wanataka wapandishwe vyeo kulingana na elimu yao maana yake ile nafasi aliyoajiriwa mwanzo inabaki tena tupu na kuanza kuipa taasisi gharama ya mshaahara mpya ambao yenyewe haijajiandaa nao
 
Wewe umefanyia utafiti wako kwenye kada ya ufundi, mimi nimefanyia utafiti wangu kwenye ELIMU kwa ngazi zote nimepita diploma na nimepita pia degree na nilicho kiona kwa ushahidi kabisa ni kwamba

walimu wengi wa diploma ndio wanao fanya vizuri zaidi kwenye ufundishaji na wanaeleweka vizuri na wanafunzi kuliko walimu wa shahada na hasa wale walimu walio toka form six moja kwa moja chuo kwakweli mwengi ni weupe sana sana hata kwenye student management ni zero kabisa.
Hata kwenye hiyo hiyo elimu umkute yule wa zamani waliokuwa wanaitwa walimu daraja c na b umkute darasani kwa kulitawala darasa wanafunzi wanamwelewa balaa ua umkute daraja A kachukuwa diploma kwa kutawala darasa wa digree atamweze kwa ufundishaji nili chokiona Mimi Huku chini vingi vile vya level ya juu kavisoma ila kijujuu digree ni undani TU wa kile kitu mfano animal cell anaishia nuclear wa juu anaenda ndani kidogo hiyo nuclear anasoma nucleus
 
Tofauti ya Diploma na degree
1. Salary
2. Skills
Sasa mtu kama kaona anaweza kuomba kazi inayotaka Diploma kwanini asiruhusiwe si maamuzi yake??.

Mfano Dereva wa Bus umkataze asiendeshe IST, utumishi wanafeli sana hapa.
Diploma anasomea ujuzi zaidi (technician) ndo maana vyuo vya kati mara nyingi elimu yake ni ya vitendo zaidi.

Pili mtu wa degree atakubali kulipwa mshahara wa ngazi ya diploma?
 
Sasa mtu umegraduate varsity na Gamba lako la GPA ya 3.5 and above afu ukalilie ajira ya cheti?lol mbona inakuwa Kama elimu haijakukomboa sasa🤣umelose miaka kibao , duh hii hatare na nusu🤣🤣
Kikubwa ujue lengo la kusoma kwako ninini!? Ukilijua hilo huwezi kuhangaika
wala kuwehuka na GPA za kwenye manila card,

Degree kwa karne ya sasa ni elimu ya kawaida kabisa wapo wengi tu vijijini huko wanalima nyanya na wala sio ya kukaa unajisifu sifu kwa watu utaonekana kiumbe wa ajabu sana kwa zama za leo kutafuta kuheshimika kwa kuwa na degree.

Maskini wa akili yeyote huona elimu ni kizingiti kwake kufanya kazi fulan akiamini hii ni kazi ya chin ya level yangu nk. Wakati huo huo anahangaika hata hela ya kununulia bagia ale.

Narudia tena hizo arrogance ndio zinafanya vijana wengi wanabaki kuwa tegemezi majumbani mwanzo hadi wanafika 40yrs kisa tu kutukuza degree.

Hebu tuhame huko kwanza zile zama za kutukuza bachelor's zilisha pita kitambo sana jichanganyeni kutafuta riziki vijana achaneni na hizo degree arrogance.
 
Umemjibu kwa hasira sana ila kakuelewa na siku nyingine aache ujinga . Yaani anataka kusema mtu aliyekaa darasani miaka 5 na mmoja wa internship ili awe MD ni sawa na mtu aliyeishia diploma, nabaki nacheka kwa sauti ndogo
Huwezii kumlinganishaa na ndio maana huwezii kukutaaa MD analalamikiaa kutokuruhusiwaa kuomba kazi za diploma
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
inaonekana wewe umesoma ila elimu yako haijakusaidia,kila level ya elimu inatolewa kwa ajilii ya kutatua aina Fulani ya tatizo,ndio maana engineer ana degree ila hawezii na hajuii hata kujengaa nyumbaa,na Fundi na technician wanaandaliwaa kwa ajilii ya kufanyaa kazii kwa vitendo japo na wao hawawezii kudesign,,,,,,,,mwenye degree hawezii kuomba kazi ya diploma akakubaliwa kwa sababu 1.Mwenye diploma huyo akiajiriwa supervisor wake au mkuu wake wa kazi anakuwa mwenye degree,je akiajiriwa mwenye degree mwenzake mkalingana elimu utakataa kutumwa tumwa coz mnalingana elimu 2.Kiwango Cha mshahara,Sheria inataka kila mtu alipwe kulingana na kiwango chake Cha elimu so watakuwa wanavunja Sheria na hawakutendei hakii kukulipa mshahara wa diploma wakati una degree yako.
 
Acheni tamaa!! Pambanieni hizo zenu za degree na wa dip nao wapambanie zao. Kumbuka mtu wa dip pia hawezi kuomba za wenye degree.
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
Pole Mkuu,

Mpaka unaandika Thread hii, it means hiyo Degree yako haijakusaidia chochote. Unasema mwenye degree ana ufanisi kazini? Kwamba amemzidi skills mwenye Diploma? Una uhakika na usemacho?

Wewe Una Degree lakini still unalia Lia kutaka favor, ndo ujue mwenye diploma ni mtu wa field na kupractice sio ww uliyemezeshwa Theory ambaye Hadi Leo unadhani maisha ni Hadi uajiriwe.

Mkuu, nimesoma Diploma then Degree Ila kiutendaji maofisini na viwandani mostly Diploma wanapiga kazi fresh.

Badili mtazamo wako Mzee.
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
Utakubali mshahara wa Diploma ukishaingia, huku ukiona mwenye digrii kama wewe kakupita 250k?
 
Back
Top Bottom