secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Wana tabia ya kuvaa head phone hata kama wako kwenye kikao.Mbona hujaweka Ujuaji 😜😅 hawashauriki hao na visuruali vyao vichupa
Mkuu kumbe weye ni ticha.Kuna Dogo alikuja Field...Eti Site akawa anakuja na Jeans kubwaa na mayeboyebo makubwaa kichwani kanyoa kiduku
Nikamwambia Dogo peleka Ujinga huko nisikuone na mavazi hayo.
Hakurudi asee sjui alienda kupatia wapi field.
Ndio maana ndoa za siku hizi ngumu, mwaka tu watu wameshindwanaKujituma nakubaliana 100% huku vyuoni tumekimbizana na assignments siku ya deadline.
Walimu wameongea sanaa
Unatafuta visingizio ili usioe.Ndio maana ndoa za siku hizi ngumu, mwaka tu watu wameshindwana
Haaa haaa above 30 naogopa "kwa nini asiolewe mpaka leo", Gen Z jeuri. Sijui nitakumbilia wapiUnatafuta visingizio ili usioe.
Ticha huwa anafanyia Field Site.....Vilaza mpo wengiMkuu kumbe weye ni ticha.
Wasiwasi wako tu!Haaa haaa above 30 naogopa "kwa nini asiolewe mpaka leo", Gen Z jeuri. Sijui nitakumbilia wapi
Hawa angalau, tatizo lao wana haraka kwa kuona wamechelewa. Wanataka ndani ya miezi 6 uwe umemvisha shela. Sasa ukimpa matazamio ya 1 yr umchunguze anakukimbiaWasiwasi wako tu!
Huyo 30+ chukulia hajaolewa kwasababu Mungu amekuekea wewe.
Kumchunguza mtu muda mrefu sio guarantee ya ndoa kudumu.Hawa angalau, tatizo lao wana haraka kwa kuona wamechelewa. Wanataka ndani ya miezi 6 uwe umemvisha shela. Sasa ukimpa matazamio ya 1 yr umchunguze anakukimbia
Fresh graduates watii pia wapo, na bullying bosses pia ni wengi sanaUtii kwenye utaratibu sahihi. Utii wa kanuni. Anajikuta yupo negative kwenye kila kitu kiasi kwamba hata akikosea watu wanamuacha tu aingie kwenye 18
Nina rafiki yangu ana kampuni yake aliajiri hawa Gen Z kama 15. Anawapa mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Mwaka huu ka renew wanne tu. Wengine wote kaachana nao anaajiri upya. Wanampasua kichwa balaa.Gen Z wanajua kuwahi kazini mpaka boss awepo. Pumbavu, kama unaweza kuepuka kuajiri hawa watu usiwape kazi
Unalinganisha dogo wa USA na dogo wa Tz tena aliekulia Mbwibde?!Hakuna kitu, ni ujinga wa mabosi vilaza wanaogopa kushindwa maarifa
Hii ni timu ya Elon Musk inayofanya kazi na serikali ya US.....
View attachment 3229096
Hata umchukie vipi huwezi kuvua ualimu wako, hatukukulazimisha uliamua kusomea mweyeweTicha huwa anafanyia Field Site.....Vilaza mpo wengi
Ni kweli kabisa wala sipingani na hayoSiku zote Mwanzo huwa ni mgumu bro. Hata hao maboss walikuwa fresh graduates pia, na wao pia walikosea na kufundishwa. Wadogo zetu tunawapenda sana na tutawafundisha pindi wanapokosea.
Utanisamehe Ila kutamka neno boss sijawah kuwapigia magoti Ata wazazi au kuwa omba samahani🤣sembuse mtu baki tuKuna jamaa kasema tatizo Gen Z hawako serious, unakuta mtu anamuita Boss - Bro😂😂
=====
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Intelligent, 1 kati ya mabosi 6 wana wasiwasi kuhusu kuajiri Gen Z tena, na 1 kati ya 7 huenda wakakwepa kabisa kufanya hivyo mwakani. Hizi ndiyo sababu:
Kutokujiongeza
Asilimia 50 ya viongozi walioulizwa wanahisi kuwa wahitimu wapya hawaonyeshi juhudi zinazotarajiwa na waajiri.
Kutokuwa na maadili ya kazi (unprofessionalism)
Hii inajumuisha kutofuata taratibu za sehemu ya kazi kama vile kuheshimu muda, matumizi sahihi ya lugha, na mavazi yanayoendana na mazingira ya kazi.
Kuchelewa mara kwa mara
Kuwasili kazini au kwenye mikutano kwa kuchelewa kumeleta usumbufu kwa mabosi na wafanyakazi wenzao.
Kutokuwa na Mpangilio
Waajiri wana wasiwasi juu ya uwezo wa Gen Z wa kudhibiti majukumu yao na kupanga kazi kwa ufanisi.
Mawasiliano Duni
Viongozi wanataja changamoto katika jinsi waajiriwa wapya wanavyowasilisha taarifa, iwe kwa maandishi au kwa mazungumzo.
Changamoto ya kushindwa kumudu majukumu ya kila siku kazini
Zaidi ya asilimia 20 ya mabosi wanasema wahitimu wapya wanashindwa kumudu mahitaji ya kila siku ya kazi.