Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Mfano mwingine hai hapa hapa tz, angalia huduma za hospital na mashule Kati ya private na public nazani utapata picha Kamili uzembe na ukosefu wa ufanisi ni jadi ya public enterprises hata upate rais malaika huwezi badili chochote natamani Sana uelewe hili
 
Amesahau kumalizia kibarua chake kuota nyasi
Kwa kuwa DPW wanataka kucentralize utendaji
 
DPW wanategemewa kuendesha magati sio zaidi ya manne pale TPA, yaani asilimia nane tu ya bandari nzima, Kuna mamlaka ya TPA pale, kuna mwekezaji mwingine anayetarajiwa kuja.

Kwanza na tuelewe nini kinafanyika pale bandarini kabla hatujaanza kutoa maoni yetu.
 
Mpaka sasa nyie watz mmeshashindwa mnataka mshindwe mara ngapi ndo mkubali hamuwezi? TPA inaendesha bandari zote tz Kwa mwezi analeta bilioni 700 na ajiendesha Kwa bilioni 600 so obviously Kwa mwezi anatengeneza faida ya bilioni Mia tu, sasa linganisha na tict kakodishwa gati moja tu lkn kila mwezi analeta faida ya bilioni Mia tatu, njoo Kwa DP world world anakuhakikishia kuwa bandari pekee ya dar atakuwa analeta faida tilioni 26 Kwa mwaka sasa unapingaje dili tamu hili ukiwa na akili timamu kisa wimbo wa uzalendo? Haya nyie wamutumbi mnaojisifu mnaweza kuendesha miradi yenu wenyewe hebu nambie kamradi kadogo tu kamwendokasi kanawatoa jasho kila siku mnasondeka watu na kuku, soko la abiria ni la uhakika kuongeza tu mabasi mmeshindwa kila siku abiria wanapiziana sababu ya mbanano.
 
Mjadala nawe utakuwa mgumu sana, kwa sababu unaonyesha wazi kuwa upo kwenye kukariri zaidi ya uhalisia uliopo uwanjani.

Nani kasema 'Private' sekta haina mchango au umuhimu katika maendeleo, hadi wewe ujikite huko moja kwa moja kana kwamba huo ndio msingi wa hoja hapa.

Rudi huko juu ulipoanzia kuni'quote' uelewe vizuri nilichoandika.
Serikali kushindwa kusimamia shughuli zake ndiyo iwe sababu ya kutaka kila kitu ifanye 'private'sekta?
Na kama hiyo haitoshi, wewe hapa huzungumzii kabisa ubovu uliomo ndani ya serikali kuwa nao kuwa kikwazo kikubwa kwa hiyo hiyo 'private' sekta unayoizungumzia hapa!

Ni wapi, nchi gani ambako 'private' sekta ilishamiri sana chini ya ruhwa na viongozi wasiojali kabisa yanayotokea nchini mwao?
Hiyo 'private' sekta itajiendesha tu hata kwenye uozo na kushamiri na nchi kupata maendeleo?

Ondoa akili yako kwenye kukariri vitabu na maandiko mbalimbali, jaribu kuelewa hali halisi ya mambo yanayoendelea ndani ya nchi husika.
 
Mimi naona huelewi ninachoeleza hapa.
Ubovu wa viongozi serikalini hauwezi kuwa ndiyo iwe sababu na kisingizio cha nchi kutoweza kufanya chochote na kusimamia maendeleo yake.
Kwa nini hutaki kuondoa ubovu huo ndani ya serikali?
Kwani serikali zinaundwa ili ziwe na viongozi wabovu, wala rushwa na wasiojali maendeleo ya nchi zao?

Mnazungumzia kibandari hicho hapo kana kwamba ni muujiza kabisa kuondoa takataka zote zilizopo hapo, kwa nini?
Kwa vile hao hao waliomo serikalini ndio wanaolea hali hiyo?
Kama ni hivyo, kwa nini hiyo serikali isibinafsishwe basi, si kubinafsisha ndilo suluhisho?
 
Kuna ulazima gani wa hiyo IGA ya kipuuzi vile..., lakini akili yako haikupeleki huko wewe; unadhani watu hawajui wanachopinga, bali ni wewe tu unayejua!
 
Ulichoambiwa kina ukweli wake,na kilichopo kina ukweli wake.
Najua logistics and port operations kwa kiasi chake,yote kwa yote Tanzania hatuna Transparency kwenye Kila sekta.Hiyo ndio shida kubwa,lack of professionalism and integrity Kila IDARA.
Lack of Vision and Mission katika Kila shirika la Umma.
TPA ikijiendesha yenyewe kwa ufanisi inawezekana hata mara mia ya hapa ilipo sasa,hatuna dhamira tu.
Wakipewa Investors kama DP world pia inawezekana shida ni hapo tu Makubaliano au ndio sijuo Mkataba haupo Transparent.
Mimi naita mikataba fiche, wapewe DP world iwapo tu mkataba urekebishwe vipengele kwa kadiri ya maoni ya wananchi na wadau wengine wa sekta mbalimbali.
Mkataba uwe wa Win Win situation.
Sio mkataba usio na kikomo hapo ndio kuna kelele nyingi, pamoja na mambo mengine.
 
Umeongea hoja nzito sana.
Siku nikiona ccm imeuawa kwa bunduki honey trap au kura ndo nitaamini tunaweza kujipanga upya. Tunahitaji mbinu mbadala.
 
Naona wewe siyo "Mmatumbi" na kama ungekuwa mmoja wao ungekuwa ni mmatumbi wa hovyo kabisa.

Unachoeleza hapa ni aibu kbwa sana kusemwa na mtu yeyote mwenye akili kichwani.
Nenda kalifikirie hilo.
 
Kuna ulazima gani wa hiyo IGA ya kipuuzi vile..., lakini akili yako haikupeleki huko wewe; unadhani watu hawajui wanachopinga, bali ni wewe tu unayejua!
Huo ubaya wa IGA ni wa kutengenezwa tu na wapotoshaji wachache na hilo naliona ni tatizo. Hii mikataba ya HGA ndio ya kupaswa kutuumiza vichwa kwani huko zinawekwa hizo financials huko ndio tulie na maslahi yetu ya kitaifa.

Ipo mikataba mingi sana inayoleta matunda mengi mpaka muda huu na hakuna hata mmoja unaoleta mjadala kama huu wa bandari. Nani kauona mkataba wa bomba la mafuta?, nani kaiona mikataba iliyojenga fly overs za Dar?.

Huyo mhusika mkuu aliyevujisha huu mkataba wa DPWna kuleta tafrani yote hii hivi sasa yupo kwenye mikono salama.
 
Sasa ni wazi akili yako haiko sawasawa.
Ungekuwa na akili iliyo sawasawa usingesema "ubaya wa IGA ni wa kutengenezwa".
Huo ubaya umetengenezwa na nani?

Hiyo unayoiita mikono salama haitakuwa salama tena karibuni.
Kama unalosema ni kweli kwamba yupo mwananchi huyo mzalendo, kumweka kwenye mikono yenu ya kishetani hii ni kumpa utambuzi stahiki wa uzalendo wake kwa nchi hii, na jina lake litakuwa ndani ya historia ya nchi.

Hili mmekwisha angukia pua, tafuteni tu njia za kubaki salama.
 
Kama kawaida ya kalamu lazima aweke matusi mawili matatu ili nafsi yake ifurahi, hawezi kupunguza kiburi chake anapoongea na mtu.

IGA inapotoshwa vifungu kwa faida ya kutengeneza kutokupendwa na wananchi kwa wingi wao, ndio upotoshaji unaotamba kwa sasa kwenye media, mambo ya fake news. Haiwezekani kila kizuri kikawekwa kwenye IGA ni ufupisho tu wa nini kinategemewa kufanyika mbele ya safari. Project contracts zinazoandikwa muda huu ndio zitakuwa na vipengele vingi zaidi, zitajumuisha matakwa ya wafanyabiashara kwa undani.

Mfumo unavyofanya kazi ni tofauti kabisa na mapovu yetu humu jukwaani.
 
Mpotoshaji ni yupi Kati ya hawa:-
1: Ninyi machawa mnaosema DP World watahusika na bandari ya Dar es salaam tu wakati mkataba unasema ni bandari zote zilizo kwenye bahari na maziwa au
2: Sisi Watanganyika tunao sema tunauwezo wa kuendeleza na kusimamia bandari zote,
 
Wapotoshaji wakubwa ni nyie mnaosema DP World atahusika na Bandari ya Dslm tu wakati mkataba unasema ni bandari zote zilizo Tz
 
🤔🤔🤔 Kama Zina "MAKE SENSE" vile.

#YNWA
 
Neno lako la chawa ulilotumia linaonyesha ni shabiki tu mwenye upande wake ambaye pia hana adabu kwenye maongezi.

Magati namba nane mpaka kumi na moja yatakuwa chini ya DPW, usitishwe na hayo yaliyoandikwa kwenye IGA atamiliki asilimia nane tu ya eneo zima la TPA.

Sisi watanganyika ni wazee wa blah blah nyingi lakini matendo yetu ni sifuri siku zote. Tunapopata kazi tunachokiweza ni kutengeneza michoro ya utapeli na wizi pamoja na kuanzisha makundi ya majungu yale ya kupigana vita.
 
Wapotoshaji wakubwa ni nyie mnaosema DP World atahusika na Bandari ya Dslm tu wakati mkataba unasema ni bandari zote zilizo Tz
Hiyo ni IGA ambayo ni kifupisho cha mradi mzima kwa ufupi utakuwa vipi, project contracts zinazoandikwa muda huu ndio pana zenye kuhusisha kila kitu. IGA ina kurasa 32 lakini hizo consession na lease plan zinakuwa na kurasa mpaka 200.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…