Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Sheria ya ajira za muda itungwe kuleta ufanisi na tija
 
Kama Rais anayetakiwa kuchukua hatua analalamika kama sisi, wananchi tufanyaje?
 
Hakuna na haijawahi kutokea duniani mwekezaji mgeni akaweka kipaumbele cha kwanza cha tija kwa mwenyeji.
Wapi nimesema tija kwa mwenyeji? Mimi nimesema wizi bandarini utaisha na delays zitaisha maana wawekezaji hawawezi lea uzembe maana wanatafuta faida. Sasa how we share the profits ndio kizungumkuti ila ufanisi tu ipo wazi wanatuzidi miles away. Mfano pale airport enzi hizo ipo chini ya mbongo ilikua mizigo inapotea, wizi, ucheleweshwaji ila alipokuja Mabeberu kama NAS au Swissport ni mbingu na ardhi.
Sisi tutaambulia ziada. Na ujinga wanaolishwa Watanzania hauzingatii weledi wa ukuaji wa mtaji ambapo kwa muda mrefu wawekezaji wageni wameutumia mwanya huo kujinufaisha na watawala wetu.
Mbona sheria zilibadilika za bodi kuwa na composition ya wabongo, undillutable shares, local content so tukiibiwa ni uzembe tu lakini sheria zilibadilika so hata mtaji ukikua na mgao unakua and so on.
 
Bandari ni shamba la bibi,wanaopinga uwekezaji wanajua kabisa hayo yanayoelezwa na huyo mtu wako wa Bandari ndio ukweli wenyewe kwamba Kuna upigaji na wananufaika wengi ndio sehemu ya wapiga kelele?
 
Hiyo namba 3 sahihi kabisa yaani pale kuna MAMIRIJA ya size zote tena mengi mno, ndiyo mimi kusema kama TISS wangekuwa wanafanya kazi yao japo hata kwa 40% maelezo yako namba 4 yangetimia walai!!!!!!!
sasa kitengo kinasimamiwa na lumumba??? TISS JAMANI MJISAHIHISHE.
 
Huyo itakua ni kuli hapo bandari. Wakati YY anasema kua hakuna mwenye misuli kabisa iweje paibiwe pesa
 
Hiyo namba 3 ina ukweili. Wakubwa wenye mafungamano na TEC ndio kikwazo.
 
Wizi ni kitu kimoja ila je Kuna sheria ya wafanyakazi wasio kuwa na ufanisi kufutiwa mikataba? Yaani mfano mtu wa masoko Bodi ya Kahawa unakuta kalala tu na kahawa imeporomoka bei Kuna sheria ya kumfuta kazi sababu hajafikia KPI?

mfano TTCL kuendana na ripoti ya TCRA imepoteza wateja zaidi ya laki 2 hivi inakuaje meneja masoko bado yupo ofisini? Unakuta anahamishwa anaenda NMB!! Lakini ingekua ni private sector lazima atumbuliwe usipofika KPI.

Nadhani imefika wakati KPI zifuatwe serikalini, umeambiwa ulete wateja 1000 Kila mwezi walete, ukishindwa utimuliwe sio mtu anakula mshahara tu huku ATCL Haina wateja!! Ndio nachopinga
 
Nasikia Mwendazake alikuwa akichota kila siku toka kwa Kakoko, na kujenga kwao Chato.
 
Wapo watanzania madalali wanauza rasilimali zetu wakisema hatuwezi kuzisimamia
Utakuta kiongozi wa serikali anakuambia pale bandarini kuna ufisadi sana ndiyo maana tumeamua tubinafsishe.
Kazi ya serikali nini?
Viongozi wanaangalia matumbo yao na familia zao huku wamesahau majukumu yao.
Viongozi hawahawa ndiyo wanahujumu uchumi halafu kibaya zaidi wanavururuga hadi uchaguzi ili wale vizuri.
Tuna watanzania wenye akili ambao wanaweza kusimamia rasilimali 100%.
TTCL yenyewe ni mtaji tosha lkn shirika limekufa
 
Very Nice idea
Shida yenu nyie viongozi mnajali masilahi yenu tu.
Hii nchi inatakiwa ipambaniwe, mikataba au uongozi wa ovyo unatakiwa ufutiliwe mbali.
Katiba inatakiwa irekebishwe, raisi asiwe na mamlaka makubwa na awe chini ya sheria.
Zuma na Trump leo wapo mahakamani wanashitakiwa ila Tanzania rais hashitakiwi.
Miamala ya simu tumekamuliwa, tunahitaji tulipe kodi ila vipato haviruhusu kulipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…