Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

TTCL yenyewe ni mtaji tosha lkn shirika limekufa
Sasa wanaambiwa muachane na Biashara ya simu mbaki na mkongo wa Taifa tu unategemea nini? Mbona "Rudi nyumbani kumenoga" ilishika kasi! Na kweli kweli tukarudi, Sasa isiweje tuambiwe Tena Leo imepoteza wateja laki mbili?
 
Sio kweli serikali itateua watu wale wale kuongoza hiyo authority kama kina Chenge, Hawa Ghasia n.k Sasa unategemea ufanisi au uhuru wa taasisi? Hao ndio wataiba kweli kweli
Nyie kila siku mnajinadi kuwa vipo vyombo vya usalama makini kama vile Polisi na TISS. Sasa mbona hao mnaosema ni wezi na mafisadi hawashughulikiwi na hizo taasisi zenu?
 
Utapatikana ufanisi na wingi wa mapato halafu? Tutarudi tena kujadili matumizi ya hayo mapato.

Tutaziba mirija ya watu huko bandarini hali ya kuwa kwengineko huko mirija yao bado inaendelea kufanya kazi.
 
Sasa wanaambiwa muachane na Biashara ya simu mbaki na mkongo wa Taifa tu unategemea nini? Mbona "Rudi nyumbani kumenoga" ilishika kasi! Na kweli kweli tukarudi, Sasa isiweje tuambiwe Tena Leo imepiteza wateja laki mbili?
Shida ya serikali inalea wezi na wezi wenyewe wapo kwenye serikali na ni viongozi wakubwa.
Halotel ni ya juzi tu lkn huwezi kuilinganisha na TTCL.
Ukitafuta laini ya Voda, Tigo, Airtel na Halotel zipo nyingi sana mtaani, tafuta ya TTCL utajua shirika lishakufa.
Na kwasasa, TTCL hata waweke mkongo wa taifa tayari ishakufa. Watanzania wengi hawana pesa ya kumudu gharama za internet.
Leo ili utumie 5GB inatakiwa uweka na 10,000 kwa maisha gani?
 
Nani kakwambia uwekezaji maana yake umeshindwa kuendesha?

Hizo fikra mgando ndo zinawafanya kila siku muwe nyuma kimaendeleo
Usifananishe uwekezaji wa nchi zenye akili na huu wakwetu ambao mnaohubiri wenyewe kushindwa kusimamia uendeshaji wa bandari hadi wizi kukithiri.
 
Sahihi.Mm nimeshalisema hili.Hatujawa serious na Bandari.Mbona TRA,Maliasili,Tanroads nk zinaendeshwa na wabongo na hawacheki na Raia.Hawa jamaa ukiingia kwenye anga zao utawatambua.
 
Ni kweli kabisa tunaweza kutengeneza faida zaidi ya tutakayopata toka DPW. Hii ya kumpa DPW kwa sababu tu ya upigaji na wizi ni kituo cha wala. Hivi DPW ni police. Inawezekanaje majeshi yetu haya na vyombo vya usalama kushindwa kudhibiti wizi!?

Kama report ya CAG imetoka na watu hawachukuliei hatua Unadhani kweli Rais na team yake wako serious na ubadhirifu unaoendelea nchini. Report ya CAG mpaka sasa imefichwa chini ya carpet.
 
Unaposema TPA ni mafisadi sijakuelewa?....Malipo yote yanafanyika baada ya kupata Control namba. Pesa inaenda Hazina. Bila control namba uwezi pata huduma. Sasa hapo ufisadi upo wapi?
 
Pesa zote zinakwenda Hazina. TPA wakiomba pesa kwa ajili ya kununulia vifaa vya kazi, Hazina wanasema hakuna pesa. Sasa hapo lawama ya nani?
 
Unaposema TPA ni mafisadi sijakuelewa?....Malipo yote yanafanyika baada ya kupata Control namba. Pesa inaenda Hazina. Bila control namba uwezi pata huduma. Sasa hapo ufisadi upo wapi?
Mafisadi in terms of rushwa maana unaelewa urasimu uliopo. Hata mizigo huwa inapotea sana mazingira ya kutatanisha.

Kingine ufanisi wao upo chini sana na serikali pia CAG amekiri wameshindwa kazi. Sasa solution ni kufanya outsourcing tu maana hata ukibadili wafanyakazi wanaokuja ni Wezi zaidi.

Cha ajabu watu wanakazania ooh bandari itauzwa wanasahau hata sahivi haijauzwa ila Kuna mafisadi machache yanakula hiko hiko kidogo kinachopatikana
 
Pesa zote zinakwenda Hazina. TPA wakiomba pesa kwa ajili ya kununulia vifaa vya kazi, Hazina wanasema hakuna pesa. Sasa hapo lawama ya nani?
Sio kweli hili, bajeti huandaliwa mapema kulingana na makadirio ya Mapato na huidhinishwa, Sasa kivipi pesa ikosekane? Huwa Wana miradi hewa kibao ndio inakula Hela Wala shida Yao sio vifaa ila wizi tu. Unakumbuka kesi ya flow meter kuzimwa? Au Makinikia kusafirishwa bila kukaguliwa kama kilichokua delcared kwenye karatasi ndio kipo ndani ya container?

TPA are bunch of embezzlers, hiyo bandari mara 10 wapewe hata JWTZ pengine tutaona Mapato yakipaa ila hao TPA Are shit.
 
Kwenye ubepari hutengenezi monopoly ya taasis Fulani kushikilia platform za uchumi. Ni ulimwengu wa ushindani . Huyu DPW anatengenezewa mazingira ku monopoly uchumi wa Tanzania
 
Vipengele vya mkataba boss. Wengi tunaunga mkono uwekezaji ila mkataba uboreshwe
 

mimi natamani wanipe niendeshe banandari.

nahisi point ya 3 ina ka ukweli fulani. Tanzania tuna matajiri wengi why wasipewe tenda hii kwa mkataba mzuri ?
 
Bajeti itakata ? Kwani serikali na mapato yote inayokusanya haiwezi kuendesha? Na mliweka vip bajeti iishe wakati huo kabla DP hajasaini mkataba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…