Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

1) Kuhusu rushwa sina hakika na hilo. kwa sababu hakuna mahali unatakiwa kulipa kwa cash.
2) Kuhusu mizigo kupotea, hii iliwa hapo awali, kwa sasa kuna ulinzi wa kutosha na kamera (cctv), zimewekwa bandari nzima
3) Kwa sasa ufanisi umeongezeka sana baada ya JPM kununua vifaa vipya vya kisasa, na matengenezo ya Gati na kina cha bahari. Ndio maana TPA wamepokea tunzo hivi karibuni kwa kuingizia serikali pesa kwa mashirika ya umma.
3) Out sourcing sio jibu sahihi. Bado hatujashindwa. Ndio kwanza matengenezo yanakaribia kukamilika. Tuwape japo miaka miwili tuangalie uelekeo.
4) Kuhusu mafisadi kula hicho hicho kidogo - Watakuwa watu wa Hazina/Serikali.... TPA hawakusanyi mapato.
 
Sasa kama bajeti inaandaliwa mapema, kwaninin serikali haitoi pesa kwa ajili ya kununa vifaa? ...
Hata wakipewa JWTZ...... serikali ndio inakusanya mapato kupitia Control namba.
 
Na hana uwezo wa kurejea huko kwa sababu hana uwezo wa kufanya maamuzi
 
CCM haitegemei kura kukaa madarakani, ni aidha tuingie kwenye machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi
Tusiruhusu akili zetu kuchoka namna hiyo.

Tukubali kwamba kuitoa CCM ni mchakato kama ilivyojichakata kujisimika kwenye veins za serikali.

Tukubali kuwa, siyo kila mabadiliko kwamba ni lazima tuyashuhudie kwa macho yetu bali tukubali kuwa msingi wa mchakato wa kuipumzisha CCM.

Jambo la kufanya ni kusimika uzalendo kwa wenetu. Tuwaeleze ukweli na watuone tunaishi kwenye huo ili wakija kutupokea wajue adui namba moja wa Tanzania ni mfumo mbovu wa CCM
 
Shida kubwa kwa Tanzania ni kuwapata hao wa kwenda barabarani.

Isingekuwa hivyo, nami ningesema tuanze kesho.

Lakini kwa 2024/2025, nasema kama CCM itabaki kuendelea madarakani kwa njia yoyote ile, huo utakuwa ni muujiza wa kipekee sana.
Ninachokiona huku Kilombero kwenye bonde la mpunga,ni kuongezeka kwa viwanda vya kuchakata mpunga na ungezeko la maghala ya kuhifadhia mpunga kila kona.
Utitiri wa majengo mapya kutoka kwa wakulima tena wakiezeka nyumba zao kwa Bati za rangi a.k.a msauz.Yaani ne Bandari halisikiki kabisa zaidi ya kwenye ofisi za umma na mitandaoni.
Kifupi Sa100 na CCM yake hawana wa kutoa madarakani hivi karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanasema bandari imeuzwa kwasababu kwenye huo mkataba hakuna sehemu panapo onyesho ukomo wa mkataba pia kwenye sehemu ya sahihi hapaonyeshi jina la mtu au cheo chake kuna sahihi tu, sasa huyo mwenye hiyo sahihi ni nani? amabaye serikali yetu imeingia mkataba nae kwanini jina lake halipo kwanini ajifiche kama ni mwakilishi wa DPW ?
 
Mfumo wa ccm tayari umekuwa kama ukoo wa mafisi, kambale au sangara!
Wanakula kila kitu hadi wao wenyewe!!
Cannibalism is real within ccm.
 
HAPANA, 2025 mbali ,watakuwa wameuza Kila ki2,

Tuungane na Nabii Mwabukusi kupeleka mashtaka mahakama ya umma iliyo juu ya zote, mabarabarani na Viwanjani Ili waovu watokomee!!
Tulia mkuu 2025 hatufiki," Nikungojapo chini shetani kaburini naenda" litapigwa Song
 
Hata mimi niliwatembelea kwenye banda lao pale sabasaba wanasema TPA haina shida ya ufanisi kwenye kupakua meli, ni janja janja tu ya wachache kutaka kufanya madili. Nchi hii kila kiongozi anayekuja akitaka kufanya dili kwenye rasilimali za nchi vizazi vinavyokuja vitakuta kitu kweli? maana watajikuta wanakaa kwenye ardhi ambayo ilishapigwa mnada kitambo.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…