Amaizing Mimi
JF-Expert Member
- Feb 2, 2019
- 489
- 1,102
Mi naomba kujuzwa ni mtaa gani yanapatikana madukaya vifaavya salon za kiume (vikorombwezo vyote)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Plastick au kioo???Naombeni kuuliza ni wapi naweza pata chupa za kuanzia robo lita mpaka lita moja kwa ajili ya kuwekea asali au.mafuta ya kupikia?Na vipimo vya kupimia robo lita mpaka lita.Ahsanteni
Plastik nduguPlastick au kioo???
Anauza vitu fake huyo David,, David sport wear Anapost viatu alivyo navyo dukani alipost sendo fulan kali za Adidas nikapiga sim niletewe ila kilicho letwa ni fake yaani ni tofauti na kwenye picha... kuanzia hapo nikajua tu huyu mswahili
Mtaa wa swahili karibu na peteol station ya OryxMi naomba kujuzwa ni mtaa gani yanapatikana madukaya vifaavya salon za kiume (vikorombwezo vyote)
mimi nahitaji za kiume reja reja naweza pata?Ilala boma mtaa wa Tabora na Pangani. Pia keko utapata au Kariakoo magodawn ya wahindi.
Sisi tuko Ilala boma bei zetu poa hata difichi angalia hapa chini. Nitext wasup uje uchukue balo grade A 0762815104
View attachment 2640929
View attachment 2640930
Msaada wa kupata chimbo la hizi miwani za rayban kwa bei jumla
Dah! Msimu wa mavuno huu. Unataka ukawapige matukio ya kutosha hao Wasukuma wa watu, huko Bariadi siyo!!wakuu nahitaji chimbo la jeans za wasukuma zile machinga wanauza 5k. zenye kuchuja rangi
Hahahaaaha....ndiyo maana yake, lete connection sasaDah! Msimu wa mavuno huu. Unataka ukawapige matukio ya kutosha hao Wasukuma wa watu, huko Bariadi siyo!!
Hahaha nilikutana na kijana wa chuo amevaa jinsi imeandikwa BABA LAO, nikajisemea huyu kama sio msukuma basi wa mbulu.Hahahaaaha....ndiyo maana yake, lete connection sasa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hahaha nilikutana na kijana wa chuo amevaa jinsi imeandikwa BABA LAO, nikajisemea huyu kama sio msukuma basi wa mbulu.
🙏🙏👊👊Wapendwa week end inaendaje?
Wanasema kizuri kula na mwenzako....na nomeona niwashirikishe fursa hii adimu hasa kwa wale wanaofika kariakoo na kujikuta wanauziwa bei ghali kuliko hata huku mtaani...
[emoji117][emoji117][emoji117]
SOMA HAPO UKIPENDA SAWA USIPOPENDA PITA KIMYA
Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko,
Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc.
Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.
Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc.
Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro.
Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau?
Mapazia ya kukata jora Kama unaenda Posta upande wa chuo cha DIT na CBE, Ukishavuka ule ukuta kuna duka la mfanyabiashara ana asili ya india anauza bei nzuri na mara nyingi Jumamos anakua na bei ya SALE kwahyo unaweza kupata majora ya mapazia kwa bei chee na kila design.
NA UKITAKA DAGAA ZA KUKAANGA FRESH KABISA KUTOKA MWANZA YANI KUTOKA ZIWANI STRAIGHT KWA MLAJI UTAZIPATA KWA HUYU HAPA 0654688288
NATUMAIN MTAKUJA NA MACHIMBO MENGINE SEMENI HAPA. copy and paste