Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Subwoofer na home theater pande zipi
Viatu vya kike vya kina mama bei nafuu vya kuuza vijijini mfano hiki
20230316_165918.jpg
 
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.

Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.

Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.

Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.

Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.

Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .

Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.

vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.

Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani

Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
Oy viatu vya kinamama bei chee hasa kuuza vijijini chimbo lipo wapi?mfano wa kiatu
20230316_165915.jpg
 
Habari ndugu wanaJf,

Mimi ni kijana wa kitanzania mchapakazi na mwaminifu sana niliejipatia uzoefu wa kununulia watu bidhaa, kuwafungia bidhaa na kuwasafirishia bidhaa kutoka dar es salaam hasa kariakoo kwenda mikoa mbali mbali.

Uzoefu huu niliupata wakati nasoma chuo x ndani ya jiji la dsm pale ndugu na marafiki waliponiomba kuwafanyia manunuzi ya bidhaa na kuwasafirishia hadi mkoani.

Baada ya kuhitimu chuo nimeendelea kuifanya kazi hii na sasa nilitamani kupata watu wapya nitakaojenga nao uaminifu ili na wao wapate huduma bora ya ununuzi wa bidhaa na kufikishiwa hadi mahali walipo.

Ipo hivi,kwa wakazi wa dar es salaam ninakununulia bidhaa yoyote ile ndani ya kariakoo na kukuletea mahali popote ndani ya dar es salaam kwa wakati. Kwa wakazi wa mikoani nitakununulia bidhaa,nitakufungia na kukusafirishia kwa njia uipendayo wewe (basi au lori). Nipo vizuri sana hapa kwasababu najua malori ya mikoa yote yanapatikana wapi na mabasi yenye huduma nzuri kwa usafirishaji mizigo.

Pia kwa wale watakaopenda niwaelekeze machimbo ya bidhaa mbalimbali ndani ya kariakoo usisite kuwasiliana nami na kama utapenda zaidi unaweza kuongozana na mimi nikakufikisha hadi chimbo husika.

Naombeni order hizo ndugu watanzania wenzangu ili wewe uokoe muda na nauli na mimi nipate rafiki/mteja na jamaà wa kudumu.

NAIPENDA SANA HII KAZI NA NAIFANYA KWA UAMINIFU MKUBWA SANA.

MAWASILIANO: 0745645035(call/sms/whatsap).

Karibuni sana uniagize Kariakooo.
Nitakutafuta kaka tufanye kitu
 
  • Thanks
Reactions: Xlz
Anauza vitu fake huyo David,, David sport wear Anapost viatu alivyo navyo dukani alipost sendo fulan kali za Adidas nikapiga sim niletewe ila kilicho letwa ni fake yaani ni tofauti na kwenye picha... kuanzia hapo nikajua tu huyu mswahili
Basi ni mswahili.
 
Nenda maduka ya wasomali

pale uhuru road zinapopak bajaj za fery koote yale maduka ya pc na laptop accessories bei simpo
Kuna duka lingine lipo kituo cha mabasi ya sinza pale limeangaliana na msimbazi polisi la pc wasomali wanauza pei nzuri sn
 
1: Chimbo la mashuka na mapazia nenda pale bib titi road next to geti la Cbe bei cheee,
2: ukitaka vitambaa vya suit kali visivyopauka nenda Khimji ya pale karibu na samora na morogoro road kwenye mataa zinapopita mwendokas kushusha kituo cha jiji(sio khimji ya karibu na clock tower)
3😛erfume nzuri za kupima kila harufu nenda city mall floor ya chin kuna mwarabu anapima kuanzia 5k unaweza changanya ladha(cocktail)
4: Raba kali bei rahisi za kiume ingia chocho ya kushoto kama unatoka Msimbaz polisi unaambaa na barabara ya mwendokas kama unaenda gerezan mwisho wa kituo cha mwendokas kula kushoto ingia hiko kinjia chenye meza nying za machinga upande wa kushoto kwako kuna maduka ya chini na juu zama huko
5: Heels kali za kike mbele ya hio njia nliokuelekeza namba 4 hapo juu nenda mbele before hujavuka congo kushoto kwako kwenye kona kuna maduka ya heels za kike
Mwamba anaujua mji sio ww unaruti moja tu kazini home mwamba anatisha sn
 
Hapo kwa Kitenge kuna jamaa anaitwa Kanu, aisee wale jamaa wapo serious na biashara mno,
M/Mungu aendelee kuwabariki
Hivii Mfano Watu Wa Mikoan wakihitaj mawasiloano ya hao watu wanaweza pata?
 
Naomba kwa mwenye kufahamu, anielekeze chimbo la vitu vya kuchezea watoto kwa bei nafuu, Baiskeli, Toys n.k
 
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.

Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.

Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.

Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.

Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.

Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .

Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.

vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.

Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani

Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
Vipi kuhusu Hair Wigs, Extensions, Hair Pieces & All about hair
 
Back
Top Bottom