Macho yangu yananidanganya?

Hao wachache wanaojua kiongozi anatakiwa aweje ndio hao wanasema tz haihitaji barabara ma ndege za abiria,madaraja na stand za kisasa!!!

unajua kwanini???wana pesa hawategemei serikali kwa mambo kama hayo.
 
WaTZ ni wanafiki sana kuna wakati wakipost watu wamefurika picha za kampeni mnadai cjui sio wapiga kura cjui hawana kazi cjui wamekuja tu kumshangaa mgonjwa aliyepona risasi. Ila watu wakijaa kwenye msiba wa mtu basi woooote wanampenda sana?

JPM ni Rais wa kwanza kufia madarakani sp imewagusa wengi hata wasio mkubali mie binafsi sikuwahi mkubali lakini nlipokea msiba nkiwa naangalia mechi ya Chelsea Atletico..... Niliacha hapo hapo nikaangua kilio!!

Sio kila kitu ni siasa wakuu wote ni binadamu
 
Hizi habari za kupendwa hazijaanza kusemwa leo. Swali ni kwa nini nguvu kubwa ilikuwa inatumika kuzima upinzani hasa kipindi cha chaguzi. Pale kwenye siri ya sanduku la kura ndiyo kipimo cha kweli cha hisia za mtu.

Naangalia huko whatsapp status, watu wengi ambao najua kabisa hawakuwa wanamkubali alipokuwa hai lakini sasa wanaweka picha na maneno ya huzuni.

Misiba katika tamaduni zetu ni social activity, inatujumuisha. Ni ngumu sana kujitenga na wengine hata kama marehemu alikuwa mtu usiyemkubali. Hivyo, hauwezi kutumia tukio hilo kama kipimo.
 
Wanaomchukia ni wachache wenye uwezo ambao ni rahisi kueneza kwenye mitandao nk
 
Watu wa Hali ya chin walimpenda sana
Sasa ombeeni utawala huu unaokuja
Usiwe upande wa wenye nacho watu mtatia
Akili
R.i.p jpm

Ova
 
kwanini ulilia bro si ungeagiza bia unywe???

mbona unaonekana una roho ngumu tofauti na matendo yako???

wanaosemaga kwenye kampeni watu walijaa kuhakiki muujiza wa Mungu ndio hao hao leo wanasema watu wamejaa msibani kuhakiki muujiza wa Mungu.ajabu wanalia na kuzimia.
 
Marehemu yeye kwani alidhibiti au alitengeneza mafisi yake!!? Mambo hamyajui kaeni kimya wabaguzi wakubwa.
 
Wakazi wa Pwani na hususani Wanaume wa Dar hupenda kulia bila hata ya sababu, sisi wa Mikoani huenda tunalia kwa kuogopa kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…