Macho yangu yananidanganya?

Macho yangu yananidanganya?

Sababu ni kilinganishi tu, sababu inaweza kuwa ya msingi au la! Halisia au ushabiki mandazi tu. Kwenye misiba watu huenda na nia nyingi, wengine ni sababu za uhakiki tu.
Kama watu wasingejitokeza kwa wingi hivi mngefurahia sana.

Mngesema ‘si unaona...jamaa lilikuwa halipendwi. Hakuna hata mtu aliyesikitika’.

Binadamu hakosi la kusema.
 
WaTz walishazoea manyanyaso toka majumbani mwao, walishazoea maisha magumu, toka huko walikokuzwa walishazoea kupigwa na kugombezwa hovyo hawakuwa wanaona shida yoyote juu ya uongozi wa JPM, isipokuwa wachache, wachache sana wanaojitambua, wanaotambua kiongozi anatakiwa aweje.

Hivyo ni kweli kuwa wanyonge hawajawahi kuwa na shida na JPM na wanampenda, hata akijibu shit utawaona wanavyocheka na kufurahi, Hivyo walikuwa wananampenda mtu wao.

100%

Magufuli alikuwa anaongea lugha tunayoielewa sisi maskini lakini haileweki kwa watu wanaopenda facts and figures.

Sisi hatujali sijui masuala ya kodi maana hayatuhusu. tuna kitambulisho cha 20k kwa mwaka, mengine mtajua wenyewe😊😊

sisi tunatandaza biashara zetu popote hadi kwenye kingo za barabara na hakuna wa kutugusa. mtajua wenyewe mnaolalamika na magari yenu mara sijui tunawachafulia au kuingilia taratibu za mji, hayatuhusu 😊😊

sisi tujichoshe kusoma ripoti sijui za world bank, IFM au wengine kutafuta nini. sisi tukishaambiwa tunafanya miradi yetu kwa pesa za ndani na hatuwategemei mabeberu. imeisha hiyo, kazi kwenu mnaopoteza muda kusoma mavitu yasiyowaingizia pesa

Sisi mambo ya kufukuzwa kazi, kudhalilishwa na boss, kuwekwa ndani kisa umeropoka mbona kwetu fureshii. kila siku wana wanaingia jela af hatujali wala nini
 
Umati usikusumbue, bali ni umati wa watu gani. Hoja ya vyama vingi umati ulikataa kwa 80%, lakini 20% wakashinda. Kwa watu wa akili za kawaida na za chini wana upeo mdogo ktk kufikiri na kuamua. Na usishangae pamoja na tahadhali ya ugonjwa wa mfumo wa kupumua, wanajazana, kurundikana na kukanyagana. Wengi Wana enda na watoto, mpaka wa migongoni.
 
Nyani Ngabu Magufuli ni Sankara Mpya wa Afrika.

Akina fatuma, maria sarungi, lissu watakufa watu watalinganisha heshima watakayopewa kwenye jamii na ya Hayati Magufuli.

Endapo lissu, fatuma au maria watafia au kuzikwa Tanzania maiti zao zitachezewa na kudharauriwa milele.
 
hata misiba ya wezi inakuwaga na watu mkuu tena wengi tu, ni kweli wapo wengi waliompenda na wewe ukiwepo lakini pia wapo wengi tu waliomchukia na katika marais wote waliotawala Tanzania marehemu aliongoza kwa kuchukiwa. Kafa Nyerere, Mkapa je uliona watu wakinywa bia kufurahia vifo vyao? uliona watu wakikamatwa kwa kosa la kufurahia vifo vyao?
Ww dish lako limeyumba sana I see!
Hajawahi tokea rais aliyependwa kama Magu Tz isipokuwa JK Nyerere!
 
Jamaa alikuwa anapendwa tuwe wakweli Tu kama watu wanapita mpka kwenye njia zisizo halali pale taifa ili kumuaga Tu Mheshimiwa basi wanaosema alikuwa anachukiwa Wana lao Jambo japo ninkweli huwezi pendwa na kila mtu
Inatofuati gani na nyomi ya CCM kwenye kampeni? Haya mambo huwa yanaratibiwa.
 
Nyani Ngabu Magufuli ni Sankara Mpya wa Afrika.

Akina fatuma, maria sarungi, lissu watakufa watu watalinganisha heshima watakayopewa kwenye jamii na ya Hayati Magufuli.

Endapo lissu, fatuma au maria watafia au kuzikwa Tanzania maiti zao zitachezewa na kudharauriwa milele.
Mtu akifa amekufa hata akitupwa barabarani zingine ni mbwembwe tu
 
Nadhani ulikuwa umelenga kumtukana Lissu zaidi ya kuzungumzia mema ya Magufuli.Sidhani kama kuna uwiano sawa uliotakiwa kuonyeshwa kwa kila mtu kwa namna gani anavyomchukulia Magufuli.Hili halikuwa shindano bali ni msiba.Hukumuona Mnyika kwenye mazishi?Kaenda kufanya nini pale?Mbona Tundu Lissu kaongea machache sana baada ya kifo cha Raisi.Unajua kwa nini?
 
Mi nadhani tuendelee kuamini mila na desturi zetu hasa mtu anapofariki ndo zinazotufanya hivyo.Ukitaka kila mmoja approve kwa namna anavyompenda au anavyomchukia nadhani utakuwa si ustaarabu na kinyume cha mila zetu.Hata hivyo “wanaomtuchukia “kama wapo hawajapewa nafasi hivyo ya kuonyesha namna wanavyomchukia,hata hivyo hawawezi kupata nafasi hiyo.Tuendelee kuamini tunampa heshima ya mwisho kiongozi wetu kuliko kutaka ku-prove idadi wa wanaompenda wapo wangapi!
Ni kweli, tuchukulie tu kuwa anapendwa sana, binafsi sio sababu ya hii mivutano.
 
Back
Top Bottom