Vitimbi gani hvo ulipata pole sana waaminifu wapo wachache
1. Alikua anataka kunitawala yaani yeye awe juu mimi niwe chini yake, yaani mimi niwe kama mwanamke na yeye awe mwanaume
2. Tendo la ndoa mpaka atake yeye au ajisikie
3. Jeuri na kiburi vyote vyake ana majibu ya hovyo yaani anaweza kunijibu anavyotaka kama anamjibu mwanae
4. Alikua anatabia ya kunikorofisha makusudi nikichukia ananisema vibaya kwa majirani na ndugu zake mwisho mimi naonekana mbaya ( HII NDIYO SABABU KUU ILIYOPELEKEA NIMUACHE )
Yaani naweza kusema yeye alikua akifurahi kuniona mimi nikiwa matatizoni maana kama kuna mtu ananidai basi yeye atasimama kidete utadhani yeye ndo anayenidai
5. Mbishi...ukimwelekeza kitu kwa nia ya kumwelewesha ye hataki anajiona mjuaji kwa kila kitu
Yaani yeye akishasema kitu ndo kasema hivyo anachotaka ni utekelezaji tu(FINAL SAY )
6. Hataki kusemwa au kukosolewa pindi anapokosea ( kuna kipindi alikua akionea watoto wa dada yangu kumbe wale watoto mmoja ambaye ni mkubwa alikua akiwaambia wazazi wake Baba na Mama ila wao walikua hawamwambii kwa kuhofia ataonekana hapendwi ila siku mtoto akaja kushtaki kwangu nikamchana kwamba anachokifanya sio kitu kizuri....AKANUNA HUYOOO...akaona haitoshi akajitenga yeye na mtoto wetu wa kwanza akawa anamtenga asicheze na wenzie, kuona hivi nikamwita tena kisha nikamwambia tena mbele ya Dada, alichosema dada ni kwamba hizo taarifa ye aliambiwa muda tu ila alishindwa kuniambia mimi kwa kuhofia nitaona anamchukia wifi yake )
7. Mbinafsi...Changu chake....chake ni chake hata kama mimi ndo nilipambana au nilifanikisha mpaka akakipata ila ni mwiko kunishirikisha...( Kuna kipindi alikua akifanya biashara flani sijawahi kushirikishwa kuhusu mapato wala nini yaani akimaliza biashara hela inafichwa hukooo...ila mimi nikirudi kazini nikitoka tu akawa anasachi mifuko ya suruali zangu ajue kuna pesa kiasi gani akikuta pesa, kesho yake ataanza kuniambia anadaiwa nikimwambia sina hela atanijibu zipo kiasi fulani kwenye suruali yangu yaani hata kama tayari ipo kwenye bajeti ya kodi ya nyumba ye atataka itumike anavyotaka yeye mwisho wa siku naanza kuhangaika peke yangu ye ananiangalia tu )
8. Anaigiza....yaani yeye anaishi ili kuwafurahisha majirani au watu, yupo tayari kwenda kumsaidia kazi jirani huku zilizopo ndani hakuzimaliza kisha baadae anaanza kulalamika kuchoka nikimwambia ananijibu mimi MSHAMBA WA MAISHA
9. Ameharibiwa na vipindi vya kwenye runinga hasa hivi vya kina Mama Terry bila kusahau na Bongo Movie
10. Anapenda kujionyesha....yaani anataka kuonekana yeye yupo juu kwa lugha nyepesi hataki kuishi katika uhalisia anataka kuonekana anaishi maisha fulani hivi ya hadhi ya juu
N.B;
KIPINDI CHA UCHUMBA TABIA HIZI SIKUWAHI KUZIONA MAANA NILIANZA NAE MAHUSIANO 2014 HADI 2018 MWISHONI NDO TULIFUNGA NDOA