Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Wamekumbushwa,tumesoma na kukulia hayo Mazingira,tunatafuta pa kujificha.

Mbadiliko huanza na sisi watu wazima.
Si lazima kupakia wote ila kwa idadi flani yatosha kupunguza hizo hali na msongamano.

Tumefanya sana hiyo michezo mpaka kujichanga na kudeal na baadhi ya makonda miaka hiyo chap chap mnapelekwa shule.

Lakini pia kama jamii au wazazi kujitazama huku mitaani kuungana na kusaidia watoto..ubinafsi umezidi sana.

Unanikuta na likitambi langu,nipo alone kwenye Gari. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€sema ukitoa lift nako kasheshe...

Wazazi tuwajibike na pia serikali iendele kuangalia namna njema ya kusadia katima sehemu hizo zenye Wanafunzi wengi asubuhi na jioni.Inawezekana kabisa.
 
Sijui bangi,aua hawakusoma hata kwanza!
 

La ajabu ni kwamba baadhi ya hao "makonda" ni wanafunzi (wa msingi, sekondari) ambao kutokana na huu usumbufu wa usafiri wameshindwa kuendelea na shule na kufanya hiyo kazi ya ukondakta na wengine pengine kubakia mitaani.......

Serikali isibaki tu kusimamia utekelezaji wa sheria za LATRA (kuwaachia wamiliki wa dalala au makonda jukumu la kuwasafirisha wanafunzi) bali ione haja au ijipambanue na kuonesha ushiriki wake wa moja kwa moja katika kutatua tatizo hili sugu.

Kwa sababu hili ni tatizo sugu nafikiri kwa serikali haitoshi tu kubaki kushurutisha wamiliki wa dalala au makonda wazingatie sheria za LATRA kuhusu hili tatizo bali ni wakati sasa wa serikali yenyewe kulichukua kwa uzito.

Jukumu na nafasi ya serikali katika kutatua hili tatizo ni zaidi ya kusimamia utekelezaji wa sheria au kushurutisha wamiliki wa dalala kusafirisha wanafunzi.
 
Mhe waziri, heshima kwako sister. I real like the way unavyo jichanganya na wananchi wako, binafsi nakupenda sana.
Ushauri wangu kuhusu adha ya wanetu kuhusu usafiri. Kwanza binafsi nahisi ni kuwaonea wafanyabiashara kufanya kazi ambayo sio yao, wana mikopo wale, wana tafuta pia faida while operational costs za biashara zao including kodi havina RUZUKU ya serikali. Anyway, hilo sio muhimu sana kwa muktadha wa uzi hu; nilikua nafikiria, muda wa watoto kwenda na kutoka shule, ndio huo huo wazazi wao nao wanakwenda makazini kwao; hivi ni lazima vipindi vianze saa 1 au 8 Tanzania nzima? Hatuwezi kurekebisha muda say saa 9 asubuhi halafu tuka adjust muda wa wao kutoka shuleni? Mida hi ya asubuhi, ndio mida ya wenye daladala kutafuta hesabu ya tajiri but kuanzia saa 2 walau daladala zinaanza kua na abiria wachache (of course hi inategemea na NJIA husika)nchi ni yetu, tutengeneze sheria rafiki kwa nchi yetu ili iwepo win win situation.
 
Hujambo? Ahsante Sana kwa maoni. Wataalamu watakaa na kuchambua maoni haya yote kisha tuje tukutane na wawakilishi wa Wamiliki mazungumzo yafanyike. Serikali na jamii tunatekeleza pamoja....
 
Mama, miongozo ya utaratibu wa wanafunzi ipo na madereva wote nakuhakikishia wote wa dala dala kuhusu wanafunzi wanaifahamu. Wao huchukulia advantage pale abiria wanapomgeukia anayewatetea wanafunzi.
Ok....naendelea kufutilia maoni na kujifunza mengi Sana kwa uchambuzi zaidi wa maoni haya kwa hatua zaidi. Ahsante Sana kwa elimu
 
Ok....naendelea kufutilia maoni na kujifunza mengi Sana kwa uchambuzi zaidi wa maoni haya kwa hatua zaidi. Ahsante Sana kwa elimu
Hongera gwajigirl unaitendea vyema nafasi yako laiti mawaziri wengine wangejichanganya Kama wewe hasa madelu tungetoa ushauri mzuri Kama unavyoupata wewe
 
Asante kwa kutoa mfano usiokuwa na uhalisia kwa LATRA
Aidha unapotoa maoni, kuwasilisha changamoto kuna aina mbili za matokeo
1. Kupata ufumbuzi wa hapo kwa hapo hii inategemeana na aina ya changamoto wasilishwa au maoni wasilishwi
2. Utaambiwa suala lako limechukuliwa kwaajili ya hatua zaidi, utapewa mrejesho ndani ya siku tatu za kazi juu ya changamoto uliyowasilisha. (Hii inategemeana na ukubwa wa tatizo lenyewe, kuna malalamiko mengine yanahitaji maafisa wa LATRA kufika eneo husika kwa nyakati tofauti ili kupata uhalisia, kuelewa kina cha tatizo na kujua ni hatua gani zichukuliwe na KWA STYLE IPI).
Unapopiga simu LATRA wakati unasubiri ipokelewe utaambiwa simu hii inarekodiwa, mosi inarekodiwa ili kuwa kama ushahidi katika utatauzi wa baadhi ya changamoto, mbili inarekodiwa ili kuiwezesha mamlaka kufahamu ni sehemu zipi korofi zinzohitaji kuwekewa mkazo zaidi, tatu inarekodiwa ili kuwapa nafasi wakaguzi ya kusikiliza na kuthibitisha ni kwa namna gani Mamlaka inatatua changamoto zinazowasilishwa.
Hivyo basi ushauri wangu kwako usiamue kwa mifano, chukua hatua kama umekutana na changamoto, wapigie simu LATRA, toa kero yako, kisha subiri kupata ufumbuzi wa kile ulichowasilisha na ikiwa zitapita siku tatu bila wao kukurudia, piga tena simu kujua wamefikia wapi, na ikiwa hakuna jibu chanya linaloonyesha mwanga wa kutatua ulichokiwasilisha, tafuta kuwasilisha changamoto yako kwa viongozi wa Mamlaka husika especially Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo ili aweze kufuatilia na kuwawajibisha wahusika

kwasababu lengo la kuwasilisha changamoto ni kupata ufumbuzi, ikiwa mpokea simu hatokusaidia kupata ufumbuzi, nashauri ni busara zaidi kusogea ngazi ya juu yake ili kuapata ufumbuzi wa kero husika
Tanzania ni yetu sote, tupaze sauti ili walioaminiwa kusimamia wafanye kazi zao, Tusiwaseme kwa mifano tunzi, bali tuwaseme kwa mifano hai, ili waendelee kuboresha usisimamizi wa majukumu waliyopewa kwa kuaminiwa kuwa wanastahili kwa kipindi husika.
 
Reactions: Lax
Haya ni matatizo sugu ya kila siku mkuu, kama upo nao karibu waambie wachape kazi tu.

Ushauri wako na mimi nimechukua
 
Hatari sana hawa latra wangetusaidia huku daladala hizi muda wa abiria wengi, zinajibanza nyuma kidogo ya vituo rasmi ili watupige bei kubwa kwa lengo la kupata siti. Hii changamoto ya miaka
Hii changamoto ni nyepesi sana Ndugu, wala usipate taabu unavuka vipi
Ikiwa umepanda kwenye gari na ukatozwa nauli zaidi ya ile iliyopangwa na mamlaka toka tarehe 8/12/2023 kisa umekaa kwenye siti au hata umesimama.
Piga simu LATRA muda wowote, wanapokea na wanatekeleza
(A) Huwa wanaomba kuongea na Konda ili kumpa elimu, akigoma utasikia anaomba kuongea na dereva na ikiwa dereva atakataa kuongea, Afisa husika ataomba kupata namba ya gari husika, kisha atamtafuta mmiliki wa gari husika kumueleza kadhia inayosababishwa na watoa huduma wake
Ikkiwa mmiliki atashindwa kutoa ushirikiano mzuri.

(B) Mmiliki, Konda, Dereva pamoja na mtoa lalamiko wataitwa LATRA kwaajili ya kupewa elimu, kisha watachukuliwa hatua kwa kwenda kinyume na masharti ya leseni zao.(kwanini wanaitwa pande zote mbili, mara nyingi konda akiitwa hawezi kukubali kuwa ametoza nauli zaidi ya ile iliyopangwa na LATRA, hivyo mtoa malalamiko anatakiwa kufika ofisini akiwa na tiketi aliyopewa kama uthibitisho kuwa alipanda kwenye gari husika, HAPO NDIPO ZILE SAUTI ZA KUREKODIWA ZINAPOKUJA KUSAIDIA KUTOA USHAHIDI WA SAUTI YA MHUSIKA)

Ushauri wangu kwako, tunapokutana na hizi changamoto tutoe taarifa ili Mamlaka husika iwajibike, tusizoee matatizo, tusichukuliwe kuwa ni hali ya kawaidia hawa watoa huduma wanapovunja sheria.
LATRA wameweka namba zao kwenye kila gari inayotoa huduma ya usafiri, lengo kubwa ni kuendelea kuboresha mawasiliano na jamii inayotumia usafiri, ili kuendelea kufanya maboresho ya sehemu zinazopungua.
CHUKUA HATUA, PIGA SIMU, KOMESHA UONEVU
 
Reactions: Lax
Pole!!!!
LATRA anamlinda mtoa huduma pamoja na mtumia huduma/Mlaji
Aidha kabla ya tarehe 8/12/2023 nauli ilikuwa Tsh 500-110 kulingana na umbali wa eneo unalosafiri, na baada ya hapo LATRA walifanya utafiti wa kina kwa kuangalia umbali, gharama za utoaji huduma, mfumko a bei pamoja na ongezeko la gharama ya nishati.

Kwa taarifa tu sio watoa huduma waliopandisha nauli ya daladala kutoka 500-600 nauli ya umbali wa KM 0-10, ila LATRA ndio waliohusika kutokana na sababu tajwa hapo juu.
Mdio maana baada ya kupandisha nauli, walilazimika kuweka namba za simu kwaajili ya kuendelea kutoa elimu na kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa utoaji huduma.
na kwa kufanya hivyo unaweza kushuhudia licha ya changamoto zinazoendelea kujitokeza na zinatafutiwa ufumbuzi kumekuwa na uhakika wa usafiri na kupunguza kabisa ile adha ya migomo ya daladala.
Ikumbukwe nauli hizi zimepangwa kwa kuzingatia umbali ambao mlaji anasafiri. mfano(0-10KM=600, 11-15KM=700, 16-20KM=800,21-25KM=900, 26-30KM = 1100)

Lengo la kupandishwa kwa nauli hizi ni kuwa na uwiano sawa kati ya mtoa huduma na mlaji kulingana na umbali anaosafiri . ila inapotokea sasa umezidishiwa nauli piga simu LATRA ili usaidiwe.
 
Nakuelewa mkuu, lakini huo mfano nachosema mimi ni tatizo sugu la miaka na miaka mkuu. Ni jambo la wao kuweka mkakati maana ni jambo linatokea kila siku inayoitwa leo. Muda maarufu kwa lugha ya kikoloni waita "rush hour". Hili ni tatizo la kiujumla sio la kuripoti gari moja.

Matumaini yangu upo karibu sana na latra. Fikisha hili mkuu
 
Hawana na Cha kumshauri kwasababu wote zero iq wamewekana tu.
 
😹😹😹 Katibu wao muenezi lazima ulipambanie kundi maalum la vidampa..!!
Hapo sasa, Katibu km Katibu, kazi ninayo na nina tamba nayo. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…