Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda


Huenda pengine Watu hawaoni UMUHIMU wa kutoa maoni yao kwa sababu maoni yao hayo yamekuwa yakipuuzwa au kutozingatiwa au labda huenda muda wa kutoa maoni ulikuwa mfupi Sana au utaratibu wenyewe wa kutoa maoni yao siyo rafiki kwao.
Tubadilishe hiyo mbinu ya kuualika umma ili Kutoa maoni yao juu ya suala hili la mchakato mzima wa Mabadiliko ya Sheria za nchi.

Mathalani, nchini Australia, mialiko ya maoni juu ya mabadiliko ya Sheria za Nchi hiyo huwa yawekwa kwenye mitandao rasmi ya Serikali kwa muda wa kutosha wa takribani miezi mitatu hadi miezi Sita kabla ya Rasimu ya Sheria husika haijafikishwa Bungeni na kujadiliwa na Wabunge wa nchi hiyo. Muswada wa Sheria husika huwa unawekwa wazi kabisa mapema kwa kipindi chote hiki cha miezi mitatu hadi miezi sita.

Mwananchi anapowasilisha Maoni yake kwenye Mtandao wa. Serikali au kwenye Ofisi ya Serikali ya kupokea maoni huwa Anapatiwa Namba Maalumu ya Utambuzi wa Usajili wa Maoni yake, for future reference. Hakuna Sheria inayotungwa kwa mtindo wa zimamoto kwenye nchi hiyo, that's why Sheria zao zinapotungwa huwa zinakuwa hazina mapungufu makubwa yaliyo mabaya.
 
Reactions: K11
Ahsante kwa maoni.


View: https://www.instagram.com/reel/C1eTEzWqzyY/?igsh=MWl3Mmk4b3N5YmJrcg==
Hii link ni ya Instagram ukurasa wa bunge na hapa ni mfano wa tangazo la wito wa wananchi kutoa maoni kipindi fulani ambapo kulikuwa na miswada ya sheria unawasilishwa. Unaweza kusikiliza na kutoa maoni tafadhali.

Ahsante Sana kwa ushirikiano wako kwenye mijadala yetu, pamoja tunajenga maendeleo na ustawi wa jamiiβœπŸ»πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
 
Hili ni gumu sana, konda anatetea upande wake, mzazi anatetea upande wake na serikali, hapo mchawi ni serikali, imeshindwa kutafuta mabasi kwa ajili ya wanafunzi? mbona makruza ya mawaziri na wakurugenzi inanunua, huu ugomvi wa konda n mwanafunzi hauwezi kuisha. Hao uliosema tuwapigie wamekaa maofisini tu, kwa sababu hili tatizo sio la leo au jana
 
haya mambo yanaumiza sana mkuu, yaani hata mwananchi unashindwa kuielewa hii serikali kama kweli ipo kwa ajili ya wananchi au kujinufaisha wao wenyewe
 
Uwekwe muongozo wa idadi ya wanafunzi kwenye daladala,hiyo ni biashara.

Serikali imejaza makodi na tozo kibao kwenye mafuta bei hazishikiki halafu unaleta nauli ya 200.
 
Acha habari zako magari ya wanafunzi tanzania nzima pesa yake unaijua unataka wananchi tuendelee kukamuliwa mpaka damu
Mabasi 100 yameandikwa ubavuni TANZANIA MILITARY yanaweza kutumika kubeba wanafunzi asubuhi na jioni, haya tayari yapo yameshanunuliwa. Dar yakiwa kama 40 hivi yatasaidia sana kuliko hivi sasa unaona asubuhi na jioni yanapita yakiwa na wanajeshi wasiozidi 10.

Jokate Mwegelo alipost video instagram ikiwa inaonesha mabasi zaidi ya 100 ya CCM yakiwa yanapita mitaa ya Dar, haya kama yapo 40 Dar yanaweza pia kufanya kazi hiyo asubuhi na jioni, hakuna gharama ya kununua maana tayari yamenunuliwa, zilipwe hizo mia 5 kama nauli kuchangia uendeshaji na utunzaji wa basi.
 
Sasa ukibeba wanafunzi 10, kuna hasara gani, watoto ni wadogo, hawakai kwenye seat hata space wanayotumia ni ndogo kuliko watu wazima, na bila kusahau so long as wanafanya hii nayo ni kutoa huduma kwa jamii, wakiwemo wanafunzi. Ni kitendo cha asubuhi na jioni tu, muda mwingine waendelee kutafuta hesabu ya Boss, kipindi tunasoma kiborilon Moshi, Matajiri wa magari ya kichagga walikua wana utu sana, unakuta gari imechukua route ya wanafunzi tu wanakwambia hawapakii abiria wengine, sijawahi kusikia wamefilisika kwa hili. UTU ni muhimu sana kuliko hayo makaratasi ambayo tutakufa tutayaacha.
 
Kuna jambo ni either watu wamesahau au hawajui kweli iko hivi,

Kwa daladala ndogo zile panya, iliwahi kuamriwa wapandishe wanafunzi wa 3, Coaster wanafunzi wa5, zilipokuja hizi Eicher na Tata wakaambiwa wapandishe wanafunzi 7. Hili la wanafunzi wa3 lilikuwa likifanya kazi tangu kipindi Mwaibula ni msimamizi wa daladala hapa Dar na ilifahamika hivyo.

Kinachosikitisha sasa hivi wazazi wenyewe hawana time ya kuwasimamia watoto wa shule, sababu ya ugumu wa usafiri sababu ya kipumbavu kabisa kwa mtu mzima, ukionekana unawatetea wale watoto wapande gari wawahi shule, abiria wenzio wanakubadilikia mpaka unashangaa kinachotokea. Jambo la kwanza Dr ni inatakiwa ianzie kwetu wenyewe wananchi. Wale watoto hawakai kwenye seat, huwa wanasimama.
 
Unatumia akili kuchangia au ili mradi tu na wewe uandike? Nauli ya Mwenge Mbagala nauli sh ngapi?
 
Hivi wewe Kwa unavyoona serikali ya ccm inaweza kuyafanya hayo mabasi kuwa ya wanafunzi zaidi ya kutaka kukamua wananchi tena
 
Me nafikiri ili kuondoa tatizo hili serikali ije na utaratibu wa kutoa vibari kwa watu wenye uwezo wa kununua magari kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi, wanapunguziwa Kodi Kisha wao wanaingia mkataba wa kuwapeleka wanafunzi shuleni na kuwarejesha kwenye vituo vilivyo karibu na nyumbn
Maana Mimi mwenyewe nimekuwa nikishuhudia kadhia hii wanayokutana nayo wanafunzi wengi wengine wanaaamka saa kumi za usiku kwenda kupigania usafiri na shuleni anafika saa tatu vivyo hivyo jion mtoto anafika nyumbani saa Mbili had saa tatu za usiku katika mazingira kama haya mtoto hawezi kufahuru lakini serikali ikihamua kutatua changamoto hii itaisha .
 
Kasome sasa Sheria yako kisha uulize kwa kurejea vifungu halafu LATRA watakuja na elimu husika kwa kina
Mimi nadhani si busara kujificha kwenye kichaka cha sheria wakati hiyo sheria imeshindwa kutatua tatizo husika
Shida hapa ni serikali mnakwepa jukumu lenu kuhusu hawa watoto.Asilimia kubwa ya wachangiaji wametoa pendekezo linalotekelezeka pasipo shida
1. serikali inunue magari ya kubebea wanafunzi maana uwezo wa kufanya hivyo inao
2.Serikali itoe ruzuku kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri ili wasione shida kuwabeba wanafunzi
Sasa mh. waziri unapong'ang'ania kua watoa huduma wafuate sheria huku haya mengine ya upande wa serikali ukipiga kimya inatufanya tuwe na maswali kama kuna nia ya dhati kutatua hii changamoto au ndio zile sarakasi za siku zote.
 
Watu wapo busy wanapigika na maisha na tofauti na wewe hii ndio kazi yako full time ya kuwakilisha na kurekebisha mambo wengine hata huo muda hawana na pesa tatizo (ukizingatia hata bundle halishikiki) sasa kutoa muda wa kwamba maoni yanaishia hapa au tunafungua na kufunga dirisha haya masuala ni mtambuka sasa wewe kusanya kila oni (let alone maoni) kila yanapoanguka iwe Bar, JF au kitaa kwenye kijiwe cha Gahawa na kuyafanyika kazi no matter kama muda umepita au haujafika (hakuna time limit katika kurekebisha au kuboresha)

Tatizo letu finger pointing imekuwa nyingi na divide and rule katika kutafutana uchawi badala ya kujikita kuboresha (after all tunajenga nyumba moja)
 
Hata ww muheshimiwa unaweza kupeleka pendekezo hilo kwenye mamlaka husika ili kuondoa kero hii, serikali ikianza kuwalipa ruzuku hao wenye magari hili jambo linaisha.
Tena kwake ni rahisi zaidi maana anahudhuria vikao vya bunge pamoja na vikao vya baraza la mawaziri, ana jukwaa kubwa la kulisemea hili , ila anapiga dana dana sana .
Mheshimiwa amekazania daladala wafuate sheria iliyowasajili kutoa huduma ila suala la serikali kununua mabasi ya wanafunzi au kutoa ruzuku halizungumzii kabisa
 
Kwakweli mhe wazir umefanya kazi nzuri, ni kweli changamoto ni kubwa. Na inatokea sababu wasafarishaji wamefocus kupata faida na ku ignore makundi maalumu kama wanafunzi, waja wazito, walemavu
 
Acha zako wewe kwani wanafunzi wanasafiri muda wote? Yaani asubuhi au jioni tu washindwe kupakia wanafunzi hata watatu kisa hesabu ya boss ? Nyie ndio mnakaliaga kimya huu upuuzi
Umenena vyema sana mkuu
 

Acheni siasa katika kila kitu.

DSM kuna idadi kubwa ya wanafunzi , na hao Madereva wanakimbizana kufikisha hesabu zao.

Hivyo huwa wanaweka utaratibu wa kupakia idadi ndogo ya wanafunzi na Abiria wengi.

Tujitahidi kutumia AKILI tuje na suluhisho na sio Kama hivi


Wenzenu Kenya Shule zote za serikali zina Magari ya kuwaleta wanafunzi Shule na kuwarudisha.


Je kwanini msifikirie kutoa ruzuku kwa wamiliki wa Magari au kununua Magari maalumu ya kuwabeba wanafunzi.
 
Kwakweli mhe wazir umefanya kazi nzuri, ni kweli changamoto ni kubwa. Na inatokea sababu wasafarishaji wamefocus kupata faida na ku ignore makundi maalumu kama wanafunzi, waja wazito, walemavu
Na mimi najiuliza swali moja: unaenda kusajili biashara, unasoma Sheria na kanuni unaelewa kuwa, kwa utaratibu huu hapa sitapata faida, bado unasajili na maoni hutoi wala ushauri, unaingia kwenye mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo halafu unaenda kutekeleza unakiuka Sheria, watu wanakulalamikia, unasema msinilalamikie..... Jamani kwani hii inaitwaje jamani? 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…