Hilo sio suluhisho maana kama serikali inaweza kununua V8 Au VX za milion 500 kila moja inashindwaje kununua basi hata kama hazina viti kwa ajili ya wanafunzi? Na ni kwa nini gari za serikali zikipita vituoni hazipakii wanafunzi wakati zinakuwa tupu? Bata wahed!Uwekwe muongozo wa idadi ya wanafunzi kwenye daladala,hiyo ni biashara.
Serikali imejaza makodi na tozo kibao kwenye mafuta bei hazishikiki halafu unaleta nauli ya 200.
Kuna jambo ni either watu wamesahau au hawajui kweli iko hivi,
Kwa daladala ndogo zile panya, iliwahi kuamriwa wapandishe wanafunzi wa 3, Coaster wanafunzi wa5, zilipokuja hizi Eicher na Tata wakaambiwa wapandishe wanafunzi 7. Hili la wanafunzi wa3 lilikuwa likifanya kazi tangu kipindi Mwaibula ni msimamizi wa daladala hapa Dar na ilifahamika hivyo.
Kinachosikitisha sasa hivi wazazi wenyewe hawana time ya kuwasimamia watoto wa shule, sababu ya ugumu wa usafiri sababu ya kipumbavu kabisa kwa mtu mzima, ukionekana unawatetea wale watoto wapande gari wawahi shule, abiria wenzio wanakubadilikia mpaka unashangaa kinachotokea. Jambo la kwanza Dr ni inatakiwa ianzie kwetu wenyewe wananchi. Wale watoto hawakai kwenye seat, huwa wanasimama.
Halafu wazazi wa wanafunzi hao hao ndio vimbele mbele wa kuiimbia CCM mapambio na kumshukuru mama kwa wanafunzi kunyanyasika na usafiri. Bata wahed!Wasaalam,
Kule x kuna hoja kwamba, baadhi ya "makonda" wa ma Bus ya abiria wanazuiwa wanafunzi kupanda ma Bus hayo.
Tangu kuja kwangu iliambatana na ujumbe uliokuwa umetumwa kwenda kwa CarolNdosi na uliosomeka "Carol , naomba usaidie hili, moja ya changamoto kuubwa ni wanafunzi kupanda daladala sijui ni sheria ipi inaruhusu konda kuaamua kupakia au kutopakia, kiufupi wakinamama wanaopeleka watoto wao asubuhi vituoni wanapitia shida sana"
Baada ya kuwasiliana na taasisi ya udhibiti (LATRA) na kwa kuzingatia kuwa, changamoto hii huenda inawakumba wazazi wengi, naomba kutoa mrejesho kwa majukwaa yote kuwa; Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi na kinachotakiwa ni Wazazi hao watoe taarifa LATRA waambatishe na namba ya gari husika. Namba ya LATRA hiyo hapo.
Ahsanteni kwa ushirikiano, tuwalinde watoto wetu🇹🇿
Shukrani kwa CarolNdosi kwa ushirikiano. Mkurugenzi @latra_tz ahsante kwa ushirikiano.
Maoni yenu mazuri hakika yatasomwa kwa tafakari zaidi✍🏻Me nafikiri ili kuondoa tatizo hili serikali ije na utaratibu wa kutoa vibari kwa watu wenye uwezo wa kununua magari kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi, wanapunguziwa Kodi Kisha wao wanaingia mkataba wa kuwapeleka wanafunzi shuleni na kuwarejesha kwenye vituo vilivyo karibu na nyumbn
Maana Mimi mwenyewe nimekuwa nikishuhudia kadhia hii wanayokutana nayo wanafunzi wengi wengine wanaaamka saa kumi za usiku kwenda kupigania usafiri na shuleni anafika saa tatu vivyo hivyo jion mtoto anafika nyumbani saa Mbili had saa tatu za usiku katika mazingira kama haya mtoto hawezi kufahuru lakini serikali ikihamua kutatua changamoto hii itaisha .
Kiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Tabia ya serekali kuumiza wanyonge ni ya kukemewa!Mbona serikali haiamuru wanafunzi kula mgahawani Bure? Kwani watoto hawapati njaa shuleni
Kwanini serikali iwaonee daladala, serikali haijui hii ni biashara
Msimamo wangu: ili kuepuka usumbu wanafunzi walipe nauli kamili
Watu wapo busy wanapigika na maisha na tofauti na wewe hii ndio kazi yako full time ya kuwakilisha na kurekebisha mambo wengine hata huo muda hawana na pesa tatizo (ukizingatia hata bundle halishikiki) sasa kutoa muda wa kwamba maoni yanaishia hapa au tunafungua na kufunga dirisha haya masuala ni mtambuka sasa wewe kusanya kila oni (let alone maoni) kila yanapoanguka iwe Bar, JF au kitaa kwenye kijiwe cha Gahawa na kuyafanyika kazi no matter kama muda umepita au haujafika (hakuna time limit katika kurekebisha au kuboresha)
Tatizo letu finger pointing imekuwa nyingi na divide and rule katika kutafutana uchawi badala ya kujikita kuboresha (after all tunajenga nyumba moja)
Mbona mchakato wa kutoa maoni huwa mrefu Sana na huku online huwa ni kuhitimisha tu? Huwa unaanzia na sample size ya jamii kubwa Sana huko ana kwa ana makundi mbalimbali yanatoa maoni muda mrefu na ndiyo maana kutunga Sheria mchakato ni mrefu kwa Sababu ya tafiti na ushirikishaji jamii kwa upana. Siku moja na wewe utaingia kwenye sample
Muheshimiwa waziri shida sio sheria au taratibu zilizopo kwenye makaratasi, shida kubwa ni uhalisia wa mambo.Na mimi najiuliza swali moja: unaenda kusajili biashara, unasoma Sheria na kanuni unaelewa kuwa, kwa utaratibu huu hapa sitapata faida, bado unasajili na maoni hutoi wala ushauri, unaingia kwenye mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo halafu unaenda kutekeleza unakiuka Sheria, watu wanakulalamikia, unasema msinilalamikie..... Jamani kwani hii inaitwaje jamani? 😁
Naam naam twende na mwendo huu, waziri atoe majibuUkiachana na sheria
Je mmefikiria kununua magari ya kuwabeba wanafunzi kama ambavyo wanafanya wenzenu wa Shule za private?
Jibu hili swali kwanza.
Ushawahi kuwa kondakta Nini maana Umeongea kwa uchungu SanaKiuhalisia ni vigumu
Msitumie sheria kuwakandamiza Watanzania masikini
Mwanafunzi anatoka Mbagala anasoma Mwenge, nauli analipwa 200 wakati mtu mzima analipa 1300
Konda anatafuta hesabu ya boss 150k
Konda anatafuta hela ya mafuta 250
Konda anatafuta hela ya dereva 50k
Konda anatafuta service za gari
Konda ana familia
Serikali imulazimishe kondakta ajaze wanafunzi atalipaje haya majukumu.
Serikali tafuteni njia ya kuwapeleka hao wanafunzi shule
Au walipe nauli kamili
Una hoja usikilizwe maana Hadi Kodi ya vocha ya 500 tunakatwa, wafanye hivo TUHivi Mama, huko kwenye vikao vyenu hamkuwahi kujadili Serikali kununua mabus yakutosha mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya Wanafunzi tu na wazazi wawe wanachangia kiasi fulani labda monthly.
Hii kero ipo miaka nenda rudi toka enzi zile za Tambaza mpaka Leo hapo Dar bado kunashida ya usafiri wa Wanafunzi tu, inamaana mpaka Leo hatuna solution?
Mama shida nyingine kuubwa mashule ya vijijini huko unakuta watoto wako kwenye highway wanaomba lift kwenye malori na magari yanayopita matokeo yake watoto wa kike wanakuwa kwenye hatari kwa hawa wahuni wa malori, na wengine.
Huko mawilayani kutokana na mashule kuwa mbali bodaboda wamekuwa ndio waume sasa wa mabinti. (Hatari sana)
Hili suala la usafiri wa Wanafunzi msiishie tu Dar es salaam hata mikoani sasa mnahitaji kuumiza kichwa, kwangu mimi naona suluhu ni Serikali kuanza school buses kuanzia kwenye miji mpaka mawilayani na vijijini huko.
Kwenye hizi highways mabus ya Wanafunzi yawe yanazungukuka muda wa kuingia na muda wa kutoka.
Kila Mkoa kwenye highways zake unakuwa na mabus yake maana tuna miji mingi mabarabarani, wilayani pia kila kwenye population kubwa inawekwa bus..nk
Huu umbali wanaotembea hawa watoto naamini hata upeo wao unakuwa mdogo mashuleni huko.
Haujanielewa haya mambo inabidi yasiwe na mwisho sababu yanabadilika kila siku na kama wazo / maoni fulani yamekuja leo haimaanishi yasifanyiwe kazi sababu mchakato mrefu ulikuwepo na wakati umepita (ndo, ndo, ndo si Chururu; i.e ni bora kuboresha kidogo kidogo kila wakati kuliko kusubiri miaka ili kufanya ad hoc changes ambazo sometimes ni politically motivated) na huenda badala ya hapa kuongelea ni nini hakikufanyika kama kuna ONI lolote haimaanishi hauwezi kulichukua na kuliweka kwenye notepad yako ili ukiona sasa yamekuwa mengi au kuna tatizo uweze hata kupeleka muswada wa kubadilisha sheria iliyopo na hata kama Sheria bado haijawekwa haimaanishi jambo fulani haliwezi kurekebishwa...Mbona mchakato wa kutoa maoni huwa mrefu Sana na huku online huwa ni kuhitimisha tu? Huwa unaanzia na sample size ya jamii kubwa Sana huko ana kwa ana makundi mbalimbali yanatoa maoni muda mrefu na ndiyo maana kutunga Sheria mchakato ni mrefu kwa Sababu ya tafiti na ushirikishaji jamii kwa upana. Siku moja na wewe utaingia kwenye sample
Hii ndo akili ya mtanzania halisi Sasawazazi walazimishwe kununua baiskel kwa wanafunzi wao itapunguza tatizo kwa kiasi flani.
Ahsante kwa mchango wako, sasa hapa ndiyo na hizo simu za msajili mmezipata ambazo nadhani wengi walikuwa hawazijui, nadhani Sasa nao wanaweza pia kutoa maoni moja kwa moja.Muheshimiwa waziri shida sio sheria au taratibu zilizopo kwenye makaratasi, shida kubwa ni uhalisia wa mambo.
Mimi Nina imani hata wewe ukipitia comments kama ilivokawaida yako(nikusifu kwa hili) uhalisia utauona kua kuna changamoto kubwa na mtu nambari moja wa kubeba mzigo huu ni serikali..
Mfano jana nimetoka mahali majira ya saa 2 usiku nipo katika sehemu ambayo asilimia 90 ya watu wanaushuka hapa ni wanatafuta daladala nyingine ya kufika majumbani mwao na muda mwingine wanabidi waongeze na boda au bajaji huko mbele. Lakini unakuta shehena na ya wanafunzi kati sare zao za shule nao wapo katika wimbi hili.
Ni dhahiri usafiri mgumu, ni wazi hawa wanafunzi huko wanapokwenda kupata muda wa kujisomea ni changamoto, dhahiri tutazalisha wahitimu wa kuungaunga. Lakini si wizara ya elimu usafirishaji au kitengo kingine chochote unaona kipo mbele kutatua kitu chochote kwa haraka na ukubwa wake.
Suala la maoni yanatolewa sana mkuu.(Na maoni mengine yanaweza pia kuja indirectly kupitia lawama)
Na suala la maoni mkuu kama serikali mngeweka kitengo maalumu cha malalamiko. Na kitengo hiki kiwe kinafikia hatua ya kutatua kabisa lalamiko fulani au kero kwa wakati.
Wasilisha hili kwenye kabineti zenu huko mkuu
Ni kweli kabisa maoni ni hatua endelevu na hapa sasa mmejua na mawasiliano ya kituo cha LATRA nadhani sasa ni kuendelea kutoa mrejesho moja kwa moja. Ahsante Sana kwa muda wako.Haujanielewa haya mambo inabidi yasiwe na mwisho sababu yanabadilika kila siku na kama wazo / maoni fulani yamekuja leo haimaanishi yasifanyiwe kazi sababu mchakato mrefu ulikuwepo na wakati umepita (ndo ndo ndo si Chururu; i.e ni bora kuboresha kidogo kidogo kila wakati kuliko kusubiri miaka ili kufanya ad hoc changes ambazo sometimes ni politically motivated) na huenda badala ya hapa kuongelea ni nini hakikufanyika kama kuna ONI lolote haimaanishi hauwezi kulichukua na kuliweka kwenye notepad yako ili ukiona sasa yamekuwa mengi au kuna tatizo uweze hata kupeleka muswada wa kubadilisha sheria iliyopo na hata kama Sheria bado haijawekwa haimaanishi jambo fulani haliwezi kurekebishwa...
Case in point kuwekeza katika Usafiri wa UMMA haiitaji Sheria kubadilika bali ni political willingness na wewe kuzungumza na wadau katika sekta husika, after all nadhani wewe una uwezo zaidi wa kuongea nao kuliko mtu wa kitaa na ukizingatia Sekta zote / Wizara zote zinategemea na kuingiliana, pia uozo wa Wizara ya Mwenzako unaweza kukuharibia wewe...
Point yangu kuu ni kwamba tukijikita kwenye technicalities hatuwezi kukosa sababu au someone to blame....
Anayenyanyasa watoto si mwenye daladala, ni huyo anayekwepa wajibu wake wa kuwalipia nauli kikamilifu watoto.We khanisi lazima utetee unyanyasaji kwa watoto!
Nakushukuru, na naomba nikazie, yaani mfano hao latra wapewe haya maoni alafu wakae kimya wasifanye lolote, kinachofata ni nini? Hii ndo changamoto kubwa ya taasisi hususani za serikali, unanyimwa huduma na hakuna na pakulalamika na kushughulikiwa kero husika matokeo yake ni ongezeko la mabango ya usitoe rushwa.Ahsante kwa mchango wako, sasa hapa ndiyo na hizo simu za msajili mmezipata ambazo nadhani wengi walikuwa hawazijui, nadhani Sasa nao wanaweza pia kutoa maoni moja kwa moja.