Madaktari wa Bongo washindwa kutema yai

BICHWA KOMWE - and DR Mambo Jambo mje mtoe muongozo kwenye hili.
Ukiniuliza mimi Ntakwambia kuna Shida nyingine tofauti na Language barrier..
Kwanini..
Kwanza Daktari ndo translator Mkubwa kwenye tasnia..

Kwa sababu anasikiliza Hostoria ya Mgonjwa kwa Kiswahili anaiandika maelezo kwa kingereza..
Halafu akishaiandika anaelezea kwa kiswahili kwa mgonjwa..

Pili sitaki kuamini kwamba Daktari akiwa Muhimbili anakuwa anaongea Kingereza vizuri ila akiwa Temeke,Mwananyamala na Ubongo kingereza kinamponyoka...

Maana yake ni kwamba Daktari akipata ajira mubimbili anaingiwa na pepo la kingereza anaongea.kingereza fresh kabisa....

Daktari huyo huyo akiajiriwa Temeke au Kigamboni pepo la kingereza linamtoka anakuwa hajui kingereza na anakuwa mkali..

Kuna kitu ambacho kinafichwa nyuma ya pazia..

Anywei..
Mafunzo ya Udaktari yote MD mpaka Zaidi ya hapo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza hata Practical.zake zote hufundishwa kwa kingereza Presentation za wagonjwa Wodini plus mitihani ya Wagonjwa na clinical yote ni kwa lugha ya kingereza hata akiwa wodini ni hivyo hivyo...

Sasa ghafla mtu ambaye kasoma kingereza miaka 6 bila Chembe ya kiswahili ghalfa anasahau kingereza????
 
Usidanganye watu wewe,wewe kama una watoto unawasomesha kwenye hizo shule zinazofundisha Kiswahili tupu? Halafu katika hizo nchi ulizozitaja hapo kuna nchi ombaomba hapo! Ni nani anamuhitaji mwenzie zaidi kati yetu na wao.
Bado tuna uhitaji wa kujua lugha za kigeni hasa Kiingereza.
 
Lugha bubu Tena, inabidi ufundishwe , AU wewe ile lugha unaichukulia poa
 
Viongozi wengi wanaosema kiswahili kitumike hadi chuo kikuu wana roho mbaya na wana nia ovu ya kuhakikisha vizazi vyao vinaendelea kufaidi keki ya taifa. Kiswahili hakina ubavu wowote kwenye ishu za kuleta hela. Wakongo na waburundi ukikutana nao wanakuambia kifaransa ni lugha ya kimaskini wako bize kujifunza kiingereza. Kama una mtoto mwepushe na hizo siasa za kuwa kiswahili ni lugha ya kufundishia hadi chuo kikuu
 
Cha ajabu ni nini? Rais Magufuli na msafara wake Zimbabwe walishindwa kutema yai mpaka rais wa Zimbabwe aliyewhi kuishi hapa akawasaidia kutafsiri kwa kiingereza.
 
Mtu ambae hajawahi kuishi nje akisikia foreigner tu anahisi ni bingwa wa Kiingereza.
 
Mkuu Hata Mimi nilikataa , mpaka pale nilipo jihakikishia mwenyewe yalio tokea, kuwa na language barrier, MD wetu English Yao ni ya kukariri kwa walivyo fundishwa Tu, nje ya hapo ni Chenga
 

huu ni uongo wa hali ya juu
Kwenye masomo ya saiyansi au kufanya kazi za kisaiyansi kinachotumika kule kwa asilimia 90 ni lugha ya kisaiyansi ambayo inatumia kingereza ila sio cha moja kwa moja kama kuelezea Fuvu la mtu wa kale AU kuelezea, Pan Africanism au pengine Slavery & feudalism. Saiyansi haiko hivyo na ndio sababu hufanya watu waliosoma masomo hayo wasiwe mahiri sana wa lugha ya kingereza
Kwenye saiyansi huwa ni fact tu, hakuna blaa blaa....Waliosoma masomo ya saiyansi watanielewa....
By the way, huko Sudan na Ethiopia, kingereza chao ni cha kuunga unga tu kama cha kwetu
 
Haha tatizo watu hamtaki kuambiwa ukweli
Nadhani wewe ndo unakubali kudanganywa. Sudan hakuna kiingereza cha kutisha na hakipo kabisa. huwezi kwenda dukani kununua kitu na kiingereza chako mtu akakuelewa, labda ukutane na wajasiriamali wa kutoka Uganda. Tusiwe wepesi wa kulishwa matango PORI, narudia tena Sudan hakuna kiingereza cha kutisha ni kile tu cha kujifunzia na tena huenda wao ndo hawajui kiingereza hivo kuwa shida kuwasiliana.
 
Mtu ambae hajawahi kuishi nje akisikia foreigner tu anahisi ni bingwa wa Kiingereza.
Labda angeniambia Kuhusu wasudani kujua kutumia silaha na kuthamini ngómbe kwa sababu kule ngómbe akizaa watapiga risasi usiku kucha. Naa kila mtu kutembea na AK 47 kama masai na sime.
 
Hata mimi nilibisha kama wewe , Lakin tulikuja kuupata ukweli English haipandi Kwa ma daktari wetu
 
Kujifunza kiswahili for that period of time ya practical ni uongo, is why english ipo, even madkatari wetu entire syllabus ni english, sasa kama wamefuzu na hawajui, i doupt kiwango cha elimu yetu
 
Labda angeniambia Kuhusu wasudani kujua kutumia silaha na kuthamini ngómbe kwa sababu kule ngómbe akizaa watapiga risasi usiku kucha. Naa kila mtu kutembea na AK 47 kama masai na sime.
Mkuu unakosea Sana kutoa maamuzi ya jumla,
 
Mkuu sijasema nawaoga wasudani,
 
Maokoto yapo au ndo kuwasumbua tu Madaktari wa watu na mwisho hawapewi chochote??!
 
Hata hivyo walirudishwa mwaka wa 3 kutoka wa 5, baada ya kuonekana uwezo wao kuwa mdogo, lakini bado Sio kesi kushindwa kufanya mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…