PostGE2025 Madeleka: Nashangaa mpaka leo Polisi wameshindwa kukamata mtu hata 1 wa mauaji ya Oktoba 29, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Your browser is not able to display this video.

Peter Madeleka:"Sasa kwa nini kwenye tukio hili kubwa, tena ambalo linahusisha mauaji ya watu zaidi ya mia tano, Polisi hawafanyi kazi yao, TISS pia inafanya kazi gani? Eh? Kwa hiyo kwenda kujificha kwenye kivuli kwamba kuna Tume yenye sura ya kimataifa, kuna majaji kutoka Uganda, na wengine wametoka Namibia, kwa hiyo ni hatua tupongeze... tutapongeza kwa sababu kupongeza mimi hakunipunguzii kitu. Mimi hata nikiamua nakusifia wewe kuanzia asubuhi hadi jioni, kwani nitapungukiwa nini? Lakini je, hiyo itakuwa imekusaidia? Itakuwa hizo sifa zimekusaidia kuondoa tatizo ambalo unalalamika nalo mtaani?"

"Lakini, huwezi kutegemea Tume ya mtu huyu mmoja, kwa maana Tume ya Rais. Rais ndiye anamiliki Tume. Hiyo Tume iende ikachunguze mambo yanayohusu jamii nzima. Haya mambo madhara sio ya Rais, yaliyotokea tarehe 29... yamemgusa kila mtu. Sasa kukabidhi haya mambo yote kwa Rais, akiamua hiyo ripoti akiificha utamfanya nini? Ama akiamua ripoti hajaichapisha hajampa mtu, utamfanya nini? Na sheria ndio imesema Tume ni yake, na ripoti ni yake. Kwa hiyo hata akiamua haipi ripoti, utamfanya nini? Lakini mwanao kafa..."

"...mumeo kafa, mkeo kafa, duka lenyu limechomwa, kituo chenyu cha mafuta kimechomwa... Mimi nilikuwa nadhani, kulikuwa kuna haja ya swala hili la Oktoba 29 na vitu viliyotokea likashughulikiwa kwa namna ambavyo tunashughulika na makosa yanayotokea nchini mwetu siku zote. Na hii ingesaidia kupunguza haya makelele makelele. Eh? Yaani mpaka leo hii mimi nashangaa Polisi kweli wameshindwa kukamata hata mtu mmoja? Polisi! Aliyeua mtu! Polisi wameshindwa kujua aliyechochea ni nani? Wanamwelea Lilla ndio aje awaambie bana, 'Jamani aliyechochea ni huyu'? Lilla maskini ya Mungu, mimi ninavyofahamu ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Siyo hata askari Polisi, hajawahi hata kupeleleza chochote Lilla! Hajui hata upelelezi unafanyikaje! Kwa hiyo mimi nilikuwa natarajia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ingeingia kazini ikatuletea majibu. Polisi hata kama hawaaminiki, wangeingia kazini wakatuletea hata hayo majibu yasiyoaminika. Mbona kwenye mambo mengine wanafanya bado watuletea majibu?

Kwa mfano juzi hapa Polisi waligundua kwamba kuna ugaidi, wakazuia yale maandamano ya tarehe saba mwezi wa saba, na waliweza kupeleleza wakazuia. Sasa leo wanashindwaje kupeleleza kutuambia aliyechochea ni nani mpaka tumsubiri Jaji Lilla? Mpaka tuchukue majaji kutoka Uganda, twende na Namibia kuchukua majaji wao watusaidie? Mimi siamini kama hili jambo ni gumu kiasi hicho."


Pia soma: Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha
 
Huyu asiwe na haraka, mwache aendelee kushangaa,
Utakamataje mtu yeyote wakati hujui kama kuna kosa lolote lililotendwa na yeyote?, ndio maana tumeunda Tume ya Uchunguzi kuchunguza kama kuna jinai yoyote!.

Tuache kuwalaumu askari wetu shupavu waliozima zile vurugu za October 29 kwa utekelezaji amri halali ya kuwashughulikia wahuni wale, ambapo kulitokea vifo 518, miongoni mwao kuna waliouliwa kwa bahati mbaya, hao ndio tunawachunguza, tukiwabaini, sheria itachukua mkondo wake.

P
 
Rais alisema waliohusika walitoka nchi jirani, na baadaye akasema walilipwa pesa.
Wewe chawa bwege unaongea utumbo gani?.
 
Yaani Pasco kaka yangu watu 500 wameuwawa kweli kusiwe na kosa hata moja!
 
Unatetea vitu ambavyo vinajulikana, tume niku buy time yaani tunamaanishwa serikali ina mkono mrefu kweli ishindwe kujua tukio la 29 oktoba nani na nani wanahusika kweli?
 
Ni kwa sababu wao ndio wanahusika, kwa hiyo wanapindisha pindisha, mbona hushangai tukio la Tundu Lisu hakuna hata mmoja aliyekamatwa, hata mshukiwa tu halafu wakati la sababa hata halijafanyika lakini unasikia tumekama vijana 130 walikuwa wapanga njama, yaani wapanga njama wamekamatwa, lakini wauaji mpaka leo hayupo hata mmoja aliyekamatwa
 
Japo Madeleka sikuamini hapa umeongea ukweli. Mfano, hayo yangefanywa na kikundi binafsi kunawatu wangekuwa walishakamatwa na wananyea ndoo mpaka sasa hata hukumu ya kunyongwa ingekuwa imeshatoka. lakini, kwakuwa kuna sintofaham ndani ya mifumo ndo maana tunaona jinsi Fedha zetu zinavoliwa juu ya jambo hili huku wananchi tukitaabika na maisha ya vitu kupanda bei...KATIBA MPYA Ni mwarobaini wa haya.
 
Aibu naona mimi
 
Polisi waua Majambazi Polisi wana investigate mtu aliyeuawa unlawful siyo vibaka
 
Polisi hao wanaozuia mikutanoa na press za CHADEMA wiki au mwezi mmoja kabla wakisema kuna viashiria vya vurugu walishindwa kujua tangu April 2025 joto la siasa limepanda na kungetokea vurugu ku wa kama zile?

Mwisho wakaingia barabarani na majumbani kupiga risasi kila wanayemuona watajichunguzaje?
 
Yaani Pasco kaka yangu watu 500 wameuwawa kweli kusiwe na kosa hata moja!
Mpaka sasa bado hakuna kosa hata moja ndio maana hakuna yeyote aliyewajibika,
Hili la uwajibikaji nimelizungumzia sana humu https://www.jamiiforums.com/threads...shia-rais-wetu-kubeba-mzigo-wa-karma.1946897/

Na kwa matukio ya October 29, baada ya Ripoti ya Jaji Chande kutoka, niliandika
https://www.jamiiforums.com/threads...biria-au-tuseme-kitu-na-tufanye-kitu.2434335/ humo nilisema
Ukiona watu 518 wameuliwa kwa risasi za polisi, na hakuna yeyote aliyewajibishwa, inaamaana hata mamlaka zetu hazijui waliowaua watu hao 518 ni kina nani ndio maana sasa tumeunda tume ya uchunguzi, tukiwabaini, sheria inafuata mkondo wake!.
P
 
Kwa hiyo polisi wa kisasa wanasubiri tume iseme kuna kosa ndio ifanye ukamataji mwanasheria nguli? Hivi tulipoteza akili nyerere alipokufa nini? Mbona tumekua taifa la mazombie?

Kuna haja gani ya kuwa na dci, dpp, na takataka zingine na manyota yao huko juu sasa km tunataka majaji wastaafu wa namibia na uganda ndio watuambie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…