Peter Madeleka:"Sasa kwa nini kwenye tukio hili kubwa, tena ambalo linahusisha mauaji ya watu zaidi ya mia tano, Polisi hawafanyi kazi yao, TISS pia inafanya kazi gani? Eh? Kwa hiyo kwenda kujificha kwenye kivuli kwamba kuna Tume yenye sura ya kimataifa, kuna majaji kutoka Uganda, na wengine wametoka Namibia, kwa hiyo ni hatua tupongeze... tutapongeza kwa sababu kupongeza mimi hakunipunguzii kitu. Mimi hata nikiamua nakusifia wewe kuanzia asubuhi hadi jioni, kwani nitapungukiwa nini? Lakini je, hiyo itakuwa imekusaidia? Itakuwa hizo sifa zimekusaidia kuondoa tatizo ambalo unalalamika nalo mtaani?"
"Lakini, huwezi kutegemea Tume ya mtu huyu mmoja, kwa maana Tume ya Rais. Rais ndiye anamiliki Tume. Hiyo Tume iende ikachunguze mambo yanayohusu jamii nzima. Haya mambo madhara sio ya Rais, yaliyotokea tarehe 29... yamemgusa kila mtu. Sasa kukabidhi haya mambo yote kwa Rais, akiamua hiyo ripoti akiificha utamfanya nini? Ama akiamua ripoti hajaichapisha hajampa mtu, utamfanya nini? Na sheria ndio imesema Tume ni yake, na ripoti ni yake. Kwa hiyo hata akiamua haipi ripoti, utamfanya nini? Lakini mwanao kafa..."
"...mumeo kafa, mkeo kafa, duka lenyu limechomwa, kituo chenyu cha mafuta kimechomwa... Mimi nilikuwa nadhani, kulikuwa kuna haja ya swala hili la Oktoba 29 na vitu viliyotokea likashughulikiwa kwa namna ambavyo tunashughulika na makosa yanayotokea nchini mwetu siku zote. Na hii ingesaidia kupunguza haya makelele makelele. Eh? Yaani mpaka leo hii mimi nashangaa Polisi kweli wameshindwa kukamata hata mtu mmoja? Polisi! Aliyeua mtu! Polisi wameshindwa kujua aliyechochea ni nani? Wanamwelea Lilla ndio aje awaambie bana, 'Jamani aliyechochea ni huyu'? Lilla maskini ya Mungu, mimi ninavyofahamu ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Siyo hata askari Polisi, hajawahi hata kupeleleza chochote Lilla! Hajui hata upelelezi unafanyikaje! Kwa hiyo mimi nilikuwa natarajia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ingeingia kazini ikatuletea majibu. Polisi hata kama hawaaminiki, wangeingia kazini wakatuletea hata hayo majibu yasiyoaminika. Mbona kwenye mambo mengine wanafanya bado watuletea majibu?
Kwa mfano juzi hapa Polisi waligundua kwamba kuna ugaidi, wakazuia yale maandamano ya tarehe saba mwezi wa saba, na waliweza kupeleleza wakazuia. Sasa leo wanashindwaje kupeleleza kutuambia aliyechochea ni nani mpaka tumsubiri Jaji Lilla? Mpaka tuchukue majaji kutoka Uganda, twende na Namibia kuchukua majaji wao watusaidie? Mimi siamini kama hili jambo ni gumu kiasi hicho."
Pia soma:
Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha