PostGE2025 Madeleka: Nashangaa mpaka leo Polisi wameshindwa kukamata mtu hata 1 wa mauaji ya Oktoba 29, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Duuh! kwa umri wako njaa na uchawa havitakuwa na manufaa sana.
 
Hata mimi nakushangaa wewe kwa kushangaa linalojulikana.
 
This attitude is very disappointing.
Kuhalalisha mauaji ya watu wasio na silaha sio suala la tofauti ya maoni.
Bahati mbaya ni mtazamo wa watu wengi.
Ni mtazamo unaotufanya tuone ni jambo la kawaida kumuua mwizi wa viatu Kariakoo.
Tubadilike. Maisha ya binadamu yana thamani.
Mwizi wa viatu leo anaweza kubadilika akipewa second chance akawa raia mwema mlipa kodi.
 
Samia Kaunda tume ya chande ripoti kaficha, hii tume anataka kuangalia sijui vitu gani, hawa watendaji wa serikali kwa sababu wanapiga mpunga wa posho za tume basi kila wakati wanashauri kuunda tume za uchunguzi. Sidhani kama hizi tume zitasaidia kuondoa kiini cha tatizo la maandamano. Maandamano ya oktoba 29 yalisababishwa na wizi wa kura unaofanywa na tume ya uchaguzi kila unapofanyika uchaguzi mkuu. Watu wamechoka kuona wizi wa kura unafanyika halafu ccm inatamba kushinda kwa kishindo, kiubinadamu halii hii ina udhi wapiga kura wengi sana hata kama wengine hawasemi. Chuki hizi hazihitaji maridhiano zinahitaji Rais mwenyewe kukomesha wizi wa kura kama ana dhamira nzuri ya kuleta utulivu hapa nchini.
 
Well said.
 
Wewe na CHADEMA wenzio!
Mimi na CHADEMA wenzangu, since when nimekuwa CHADEMA maana this is breaking news to me.
As far as I remember sijawahi na wala sitarajii kuwa kwenye chama chochote cha siasa but I won't stop fighting for human rights and civil liberties.
 

Yaani watu wamekufa halafu unasem.a hamna kosa lolote?
 
Mkuu, inawezekana una data za ndani kweli... hii amri "halali" ilitolewa lini, na nani, na wapi?
 
Pasco hakika magufuli alikutendea haki he knew you na hata wale waliokupa kura moja walikutendea haki watu pekee waliokosea ni waliokupa degree ya Sheria sijui Hadi kuwa wakili hao walikosea.
 
Mkuu, inawezekana una data za ndani kweli... hii amri "halali" ilitolewa lini, na nani, na wapi?
Mtu ukiwa trend reader mzuri, kuna vitu huhitaji kuwa na data kuvijua, majeshi yote wanafanya kazi kwa command, yako chini ya CinC, ukiona mpaka ripoti imetoka wamekufa watu 518 and no one amewajibika, CDF, IGP na DGIS wote wako ofisini, hushangai!.

Ile issue ya 1976 kule Mwanza, walikufa mahabusu 4 tuu mikononi mwa polisi, Nyerere alisafisha kutoka juu kwa msaidizi wake mkuu Kawawa alikuwa ndie VP na PM, alishushwa cheo kuwa waziri asiye na wizara maalum, waziri wa mambo ya ndani Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa nchi ofisi ya rais anayeshughulikia Usalama wa taifa, Peter Siovelwa, waliamriwa nizikute mezani barua zenu za kujiuzulu, IGP Samuel Pundugu na DGIS, Emelio Mzena, walistaafishwa kwa manufaa ya umma, wakuu wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Peter Kisumo na Mabawa walitenguliwa, ma RPC, RSO, OCD na DSO wa miko yote miwili, kwanza walistaafishwa kisha wakapandishwa kizimbimbani!, na hakuna tume iliyoundwa kubaini hayo!.

Utaratibu wa matumizi ya silaha kwa jeshi la polisi, unasaini silaha, na unasaini full magazine ya risasi, na wakati wa kurudisha silaha, una toa maelezo ya kila risasi uliofyatua. Sasa wamekufa watu 518, hakuna yeyote aliyewajibika, akili haijakuambia tuu ulikuwa ni utekelezaji wa amri halali?.

Mimi baada ya kumaliza JKT kwa mujibu wa sheria, nilijiunga straight na JWTZ, kwenye deppo ya JW, kuna wakati unapewa amri ya hovyo kukupima utii, kama kuambiwa lala chini!, unalala!, ruka kichuchura, unaruka!, galagala kwenye dimbi la maji machafu, unatakiwa kwanza kutekeleza amri, kisha complaini baadae.

Moja ya sifa za askari wote ni kulenga shabaha, order ya shoot kwa anti riot ni shoot to destabilize them, walitakiwa kuwa shoot miguuni ili kuwalaza chini, na shoot to kill, sasa kama watu 518 wamekufa no one amewajibika, bado unahitaji data kujua ni amri halali au?!.
Hili mimi nimeliandikia makala kibao https://www.jamiiforums.com/threads...idia-uharibifu-wote-kwa-kuusababisha.2397507/ humo nimeshauri
p

P
 
Yaani watu wamekufa halafu unasem.a hamna kosa lolote?
Tanzania ni nchi inayofuata kanuni za kimataifa za innocent until proven guilt, kunapotokea kosa lolote, lazima kwanza uchunguzi ufanyike kubaini kosa ndipo tusema kuna kosa, ni kweli wamekufa watu 518, kitendo cha mpaka sasa hakuna aliyewajibika, hii maana yake kwa mujibu wa mamlaka, hakuna kosa lolote, tusubiri matokeo ya ripoti ya uchunguzi, kukibainika kosa, wahusika watawajibishwa!.
P
 
We mzee umechanganyikiwa itakua
Ina maana matukio ya uhalifu yanayotokea mtaani watu hawakamatwi mpaka uchunguzi wa tume ufanyike???
 
sawa, lakini. Kwanini, uchunguzi unaenda taratibu mno na kwa gharama kubwa? Kwani wakikamatwa ndo kusema watahukumiwa wote hata kama kumetumika muda mwingi na gharama kubwa? Kwanini, mauwaji ya kirai ya kawaida yakifanyika huwawanasombwa na wasio husika halafu mahakama inaamua? Mimi nilitarajia baadhi ya sehemu kuliko tokea mauwaji viongozi sahv wangekuwa chini ya vyombo vya sheria. au uchunguzi unaofanywa sahiv ni kuangalia kama kuna udanganyifu ulifanyika kinyume cha maelekezo? Inafikirisha. KATIBA MPYA wakati wake ndo huu.
 

Brother acha hizo story ujue tunakuheshimu sana kaka mkubwa.
Unasemaje kuhusu watu kibao wanaokamatwa na Polisi kwa tuhuma mbalimbali halafu wanawapeleka Mahakamani wakati uchunguzi bado?
 
Things work opposite in TZ, unawekwa ndani na polisi wanasema upelelezi bado unaendelea. Ukipelekwa mahakamani it's just for mentioning na unarudi rumande for the very same fuckin' excuse kwamba upelelezi bado unaendelea na remandees wamejaa mahabusu na vituo vya polisi kwa sababu hizohizo za upelelezi bado unaendelea sasa kwanini hawa serial killers(askari) ya kwao yamechukuliwa kinyume na taratibu zilizozoeleka?
 
Anajishangaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…