Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Ndugu mdau,
huenda uzi huu umegusa 100% ya wadau wa Jf, na kwamba mpaka unapost uzi huu kuna wadau wana madeni ya kwenye simu labda amekopa muda wa maongezi, data au pesa kwenye mtandao husika na yupo analitumia hivi sasa jukwaani, na hii inaweza kua hadi 90% ya wadau wameshawahi kupitia madeni haya, mpaka inafikia mdau moja anamwambia mwenzake anaetaka kumtumia pesa asitume kwenye namba hii coz ina changamoto kidogo, ntakupatia namba nyingine, kumbe changamoto ya hiyo namba ni deni la muda wa maongezi, mb au pesa na mtandao husika.

madeni mengine ya fedheha ni haya ya kausha damu daily au weekly. madeni haya yanawaotesha sana watu vipara na vigimbi maana yanakimbiza watu mchakamchaka wa kiwango kibaya sana.
Na wengi wenye madeni haya hua na stress hatari zaidi na kuwasababishia utamaduni wa kukosa hamu ya kula, hamu ya tendo la ndoa na kwakweli kukosa usingizi kabisa, na kumfanya mdaiwa kua kwenye hatari ya kupata changamoto ya afya ya akili.

madeni mengine ambayo nayo ni ya fedheha lakini yana staha kiasi ikiwa mdaiwa atajisalimisha kwa mkopeshaji mapema ni pamoja na madeni ya kwenye vikoba, saccoss au kwenye mabenki.
Athari za madeni ya kwenye units hizi humuathri na kumfedhehesha sio tu mkopaji bali pia huifedhehesha familia na pengine kubadili kabisa maisha ya familia husika. Ni madeni ambayo husababisha changamoto za moyo, mstuko wa moyo na pengine hata kupoteza makazi au kupoteza maisha ikiwa hazitachukuliwa tahadhari za mapema.

In fact ni vizuri kukopa ikiwa una malengo, nia na umejizatiti kusonga mbele kiuchumi. Na kwasababu hiyo kukopa hakuepukiki katika kujinasua na unyonge wa kiuchumi.

kopa kistaarabu kuepuka fedheha na athari mseto za madeni physically and mentally.

In fact binafsi nimekopa na kudaiwa sana tu, na kwakweli nitaendelea kukopa licha ya stress mbalimbali ikiwa matumizi ya mkopo wenyewe yameenda mrama na uhakika wa marejesho una tia shaka.πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
 
nilipomalizaga tu Form six nikapata kazi ya kuwa nakopesha watu kwenye kampuni flani ya mikopo. ule uzoefu wa kukopesha na kuanza kudai marejesho na ule usumbufu na kadhia nilijikuta tu nachukia kukopa. Mungu akanisaidia nikajikuta nina marafiki ambao hata nikiwa nimetigwa tunaazimana pesa bila hata kujieleza utarudisha lini .
 
Aiseee hata hivyo we ni mwanifu wengine natupa line
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Madeni kama yote hapa nipo normal as usual lakini madeni yangu ni ahadi sio ya kukopa help labda hapa MGODI Vodacom ndio na deni zaidi ya hapo sina deni la kitu au pesa labda Ahadi tu
Ahaaa sawa maana ahadi ni deni
Ila deni la Ahadi haliwezi kukufanya usicheke
 
Pole ilikuaje aisee
Nilikopaga kama 50k kwa jamaa angu niongezee ninunue. cm nikamwambie narudisha kesho."jamaa akasisitiza iwe kesho mana anataka asafir kuelea dar na hiyo 50k ndo anayotegemea.."nikamwambia ok""mana kuna boss mmoja nikikua nafanyaga kazi kwa kaahidi razima atanipa hela yangu jioni mana ndo kaenda ATM kutoa pesa jioni..."naenda anasema kaporwa.. njiani dah..! jamaa niliemkopa nae anasisitiza nimlipe asubuhi na mapema""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…