Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Madeni yasikufanye ujiue au kujivua utu, vumilia yatapita tu

Nawasalimu sana ndg zangu, ningependa kushea nanyi mawili matatu yanayohusiana na maisha na kwanini hupaswi kuukatisha uhai wako kisa madeni,

1. Mimi ni mwajiriwa niliyekata tamaa na maisha kutokana na changamoto za maisha nazopitia kwani hata kula yangu shida na kuvaa ndio usiseme, nina suruali tatu na shati tatu tu.

2. Mara kibao nimejitahidi kuwashirikisha ndg na jamaa zangu wa karibu kuhusiana na hali ya ugumu wa kimaisha naopitia lakini hakuna nachoambulia zaidi ya dharau kutoka kwao na kejeli.

3. Kuongeza deni juu ya deni sio dawa ya kujikomboa kutoka kwenye madeni bali ni kuongeza ugumu wa maisha

4. Nimelazwa ndani mara kibao kisa madeni ya watu na mtu asikudanganye huwezi jishughulisha vyema kwa lolote lile ukiwa na madeni.

5. Madeni ni mabaya sana yani tena sana, yanarudisha nyuma, yanadharirisha ila yote na yote usiutoe uhai wako wala usiuvue utu wako kisa madeni, maisha inabidi yaende tu mie madeni yangu nayamaliza 2027 .

6. Hata siku hii ya leo sijala kitu lakini Mungu ni mkubwa najua yeye ndio anayeijua kesho yangu .

Ukiona hayakuhusu kaa kimya Mungu asije akakupatia mtihani kama huu pia.
Mwamposa anaposema madeni NI Roho unatakiwa uombe Sana Roho hiyo Ife na ulipe kirahisi mnambeza na kumsema vibaya.
 
Nadaiwa
Songesha 3000
MPAWA 34,000+
TIMIZA 8000+
KAMILISHA 89,000
TIGO NIVUSHE 119,000
AIRTEL nadaiwa deni fulani 420,000
Serikali Manispaa 1,000,000 (hii silipi maana wakitudaka wote magereza yatajaa)

Na hapa nimetulia nina amani zote na bia nakunywa utafikiri sidaiwi.
 
kuna nyakati nilikuwa na madeni, hadi nilitamani kubadili namba ya simu kila kona deni.. ni mwendo wa kukonda.. tu.. ila nilijifunza sana.. sasa hivi sikopi hata iweje aisee 😅😅 napambana na hali zangu tu
😀😀😀nilidhani peke angu kumbe ni hali ya wengi

Unajikuta unadaiwa na kila mtuu kila kona hadi sio poa
 
😀😀😀nilidhani peke angu kumbe ni hali ya wengi

Unajikuta unadaiwa na kila mtuu kila kona hadi sio poa
huwa nyakati ngumu sana.. unawaza kila aina ya wazo baya na zuri ili kujikwamua ila wapi.. wakianza piga simu wanakuwa kama wametumanaaa .. 🥲🥲🥲 acha tu.. mie nikisikia mtu anadaiwa au hata anae jitundika kisa madeni huwa naelewa mapito yao . navaaga vile viatu vyao kwanza
 
Nilijua ni mimi tu aisee najutraaaaa na sitokaa nikarudia nimedharirika nimepoteza direction ya maisha hakuna kinachoenda kwe maisha nna sket mbli tshert mbil na sijui yatapita yaend wap ni kam yapo kuninyoosha aman naiskia kwenye redio nimechoka yule alojirusha ghorofan nataman ngekuwa mimi nipumzike kwa kwel but all in all Mungu mwema[emoji24][emoji24]ila hii hali sikia tu
Jiue tu maana ukishafikiria jambo ni sawa na umejiua
 
huwa nyakati ngumu sana.. unawaza kila aina ya wazo baya na zuri ili kujikwamua ila wapi.. wakianza piga simu wanakuwa kama wametumanaaa .. 🥲🥲🥲 acha tu.. mie nikisikia mtu anadaiwa au hata anae jitundika kisa madeni huwa naelewa mapito yao . navaaga vile viatu vyao kwanza
Kama hujapita huwezi uelewa
 
Back
Top Bottom