Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Mnataka mharishe kwenye mabasi yao! Kama vipi andaa msosi wako mwenyewe toka nyumbani, beba vinavyobebeka!
 
Aise,. Hii itakuwa kweli, ndo maana bei za vyakula vya hovyo zinakua juu sana, ili ku-kapani mzani, Kati ya mwenye hotel na mwenye mabasi,
 

• Kuna mtu atakuja ku-comment, watu wabebe ma hotpot kutoka nyumbani,

• Yani unaongeza kero juu ya kero, huku hotpot, huku mizigo ya kawaida
• Kweli Africa is dark content
 
Sasa wanauza bei kubwa ili kukomoa??? Maana kama kama ni kuuza, tayari wana uhakika wa kuuza sababu wateja wanakuja tu. Wangeuza bei za kizalendo kama za mitaani. Angalau ile hotel Iringa pale Igumbilo wanauza vyakula bei ya kawaida.
 
Sana mkuu, hasa yule mama mwenye watoto, walishindia biscuit na soda mpaka wanafika mbeya.
Huyo mama nae ni mjinga na mpumbavu, yani anajua fika hotelini chakula ni bei ghali yeye anaenda na hela ndogo alafu anataka huruma. Ukiona chakula cha hotelin hukiwezi na una watoto pika chako nyumbani beba kwenye hotpot wenzako wakishuka kununua wewe unashuka na chako unakula hakuna mtu atakuuliza. MUACHE KUILAUMU SEREKALI KWA UJINGA WENU.
 
Kwa hapo ni sahihi sio rahisi kihivyo .
Kikubwa serikali ingeweka utaratibu wa chakula kwenye mabasi na bei elekezi bila kusahau watu wa afya kuhakiki hivyo vyakula maana uchafu ni mwingi pia .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Sasa wanauza bei kubwa ili kukomoa??? Maana kama kama ni kuuza, tayari wana uhakika wa kuuza sababu wateja wanakuja tu. Wangeuza bei za kizalendo kama za mitaani. Angalau ile hotel Iringa pale Igumbilo wanauza vyakula bei ya kawaida.
Nafikiri sababu ni demand kubwa, yaani lazima utakula kwa hiyo wanapandisha bei wanavyoona wao ingawa sio sawa
Kama hawapati wateja na vyakula vinalala labda, ila wanauza sana tu
Na sidhani kama kodi kuna kodi hapo bali kajenga mwenye mali hapo
 
Asante Mkuu kwa maoni yako! Kama LATRA wamepandisha nauli na serikali imeziba masikio haitaki kusikio kilio cha wananchi, na hili wanaweza wasikusikilize!
Mkuu nadhaini mtu akitaka kusafiri kama hana uwezo wa kula kwenye hotel hizo, afungashe chakula chake kwenye hotpots! Basi likifika kwenye maeneo hayo mtu anafungua chakula chake anakula!
 
Karibu mkuu, 😀😀, Madereva hawapo fair kabisa.
Ni sawa
Lakini Kwa wasafiri ,hasa ukiwa na watt andaa chakula alifajiri kabla hujaondoka kuepuka gharama!

Hiyo elf 5 angenunua viazi vya elf 3 angewahi kuamka ,akakaanga chips , akaweka kwenye container,!na soda take away 2 mbona fresh tu!
Au badala ya soda angenunua matunda ya buku 2 kipindi hiki maembe ta kutosha tengeneza juice,ilaze kwenye friji asbhi inakua imeganda kabisa,mpk muda wa kula masaa 5-6 inakua imeyeyuka kabisa!

Sipendi vyakula vya njiani naogopa kuumwa tumbo!

Labda kuku wa kuchoka,biscuit ,soda nje ya hapo hapana!
 
Kuna basi linaitwa SuperFeo ya kutokea Moshi kwenda Songea
Umeona sasa safari ilivyo kuwa ndefu 😐,

Abiria unaburuzwa kutoka Moshi saa 12 asubuhi chai saa 8 Dodoma pale FourWays wana hoteli yao chakula ni kiporo na sahani wanauza sh. 8000
Mamlaka kazi kuongeza nauli tu hakuna la maana wanalo fanya, hii nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…