Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini


Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Mnataka mharishe kwenye mabasi yao! Kama vipi andaa msosi wako mwenyewe toka nyumbani, beba vinavyobebeka!
 
Kilichopo nyuma ya pazia nikuwa huwa kuna fedha inawarudia sina hakika km ni hao madereva au kampuni kwa ujumla na hili nilithibitishiwa na mmoja wa mabosi wa kampuni ****** tulitoka moro kwenda dar kufika mdaula kuna sehemu sio ya miaka mingi sana ya kuchimba dawa hapo ndyo huyo boss ilivyo julikana yupo humo ndani akaletewa chakula tena akibembelezwa apokee yule boss akasema anataka na hesabu ya mabasi ya kampuni yake yaliyo leta wateja wakasema wataiandaa na kuiweka kwenye group.
Nika muhoji kwani kuna chochote kinaingia kwa huu mfumo? Akanijibu kuwa biashara ni fursa ya bishara nyengine
Aise,. Hii itakuwa kweli, ndo maana bei za vyakula vya hovyo zinakua juu sana, ili ku-kapani mzani, Kati ya mwenye hotel na mwenye mabasi,
 
Mtanzania anachuuzwa km bidhaa, ulipe nauli bado wakufanyie biashara tena, unapelekwa hotel wanayotaka wenye basi, na ni dili. Wafanyakazi wa basi wanakula bure na mwisho wa mwezi mwenye hoteli awapa posho. Hizo hotel vyakula vyao ni viporo na bei ya juu. Hotel ziko porini ili usiende kwenye migahawa ya bei ya chini. Ukiingia Highway Korogwe kwanza wanavyojisikia na kudharau abiria, sahani ya wali 8000 na vinyago 3 vya nyama. Abiria hushindia biscuit. Unateswa ndani ya nchi yako na walafi wachache. Kwanini LATRA isitoe maelekezo abiria wapate chakula mjini sehemu zenye migahawa mingi? Mtu mweusi ni laana, hatosheki, mlaku. Hizo hoteli hasa Dar-Arusha ni za wenye mabasi wamezijenga porini usiwe na option

• Kuna mtu atakuja ku-comment, watu wabebe ma hotpot kutoka nyumbani,

• Yani unaongeza kero juu ya kero, huku hotpot, huku mizigo ya kawaida
• Kweli Africa is dark content
 
Jali afya yako unapoondoka nyumbani una hakikisha una vyakula vya kukaanga kama kuku au nyama na chapati zako kabisa na chupa za maji
Hapo utaishinda njaa na safari

Kula hovyo tatizo hao wanauza mpaka vilivyolala na ukianza kulalamika tumbo unalaumu tena
Kiukweli hoteli za vyakula barabarani huwa bei kubwa sio Bongo tu ni kila mahali duniani
Ukienda hata Ulaya ni hivyo hivyo tena utashangaa wanavyopandisha bei mpaka unanunua kwa shingo upande
Kwa bongo huwa najipanga toka nyumbani, sio kwa sababu ya bei hapana bali naogopa kuanza kumsumbua konda
Sasa wanauza bei kubwa ili kukomoa??? Maana kama kama ni kuuza, tayari wana uhakika wa kuuza sababu wateja wanakuja tu. Wangeuza bei za kizalendo kama za mitaani. Angalau ile hotel Iringa pale Igumbilo wanauza vyakula bei ya kawaida.
 
Sana mkuu, hasa yule mama mwenye watoto, walishindia biscuit na soda mpaka wanafika mbeya.
Huyo mama nae ni mjinga na mpumbavu, yani anajua fika hotelini chakula ni bei ghali yeye anaenda na hela ndogo alafu anataka huruma. Ukiona chakula cha hotelin hukiwezi na una watoto pika chako nyumbani beba kwenye hotpot wenzako wakishuka kununua wewe unashuka na chako unakula hakuna mtu atakuuliza. MUACHE KUILAUMU SEREKALI KWA UJINGA WENU.
 
• Upo sahihi kabisa mkuu, ila siyo kila mtu anauwezo wa kutembea na kuku,
• Unakuta familia haina kuku, familia haina bata,
• Familia inaishi kwa kula ugali wa dona, na maharagwe

• Mkuu hapa tuzungumzie kwa watu wote, kuazia safari za maskini mpaka safari za mwenye Kipato cha juu. Je hizo kuku atazihimili? MENEMENE TEKERI NA PERESI
Kwa hapo ni sahihi sio rahisi kihivyo .
Kikubwa serikali ingeweka utaratibu wa chakula kwenye mabasi na bei elekezi bila kusahau watu wa afya kuhakiki hivyo vyakula maana uchafu ni mwingi pia .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Sasa wanauza bei kubwa ili kukomoa??? Maana kama kama ni kuuza, tayari wana uhakika wa kuuza sababu wateja wanakuja tu. Wangeuza bei za kizalendo kama za mitaani. Angalau ile hotel Iringa pale Igumbilo wanauza vyakula bei ya kawaida.
Nafikiri sababu ni demand kubwa, yaani lazima utakula kwa hiyo wanapandisha bei wanavyoona wao ingawa sio sawa
Kama hawapati wateja na vyakula vinalala labda, ila wanauza sana tu
Na sidhani kama kodi kuna kodi hapo bali kajenga mwenye mali hapo
 
Asante Mkuu kwa maoni yako! Kama LATRA wamepandisha nauli na serikali imeziba masikio haitaki kusikio kilio cha wananchi, na hili wanaweza wasikusikilize!
Mkuu nadhaini mtu akitaka kusafiri kama hana uwezo wa kula kwenye hotel hizo, afungashe chakula chake kwenye hotpots! Basi likifika kwenye maeneo hayo mtu anafungua chakula chake anakula!
 
Karibu mkuu, 😀😀, Madereva hawapo fair kabisa.
Ni sawa
Lakini Kwa wasafiri ,hasa ukiwa na watt andaa chakula alifajiri kabla hujaondoka kuepuka gharama!

Hiyo elf 5 angenunua viazi vya elf 3 angewahi kuamka ,akakaanga chips , akaweka kwenye container,!na soda take away 2 mbona fresh tu!
Au badala ya soda angenunua matunda ya buku 2 kipindi hiki maembe ta kutosha tengeneza juice,ilaze kwenye friji asbhi inakua imeganda kabisa,mpk muda wa kula masaa 5-6 inakua imeyeyuka kabisa!

Sipendi vyakula vya njiani naogopa kuumwa tumbo!

Labda kuku wa kuchoka,biscuit ,soda nje ya hapo hapana!
 
Kuna basi linaitwa SuperFeo ya kutokea Moshi kwenda Songea wana kiburi na dharau kwa abiria. Abiria unaburuzwa kutoka Moshi saa 12 asubuhi chai saa 8 Dodoma pale FourWays wana hoteli yao chakula ni kiporo na sahani wanauza sh. 8000. Kuna hoteli nzuri Babati hasa pale Himiti bei ndogo
Kuna basi linaitwa SuperFeo ya kutokea Moshi kwenda Songea
Umeona sasa safari ilivyo kuwa ndefu 😐,

Abiria unaburuzwa kutoka Moshi saa 12 asubuhi chai saa 8 Dodoma pale FourWays wana hoteli yao chakula ni kiporo na sahani wanauza sh. 8000
Mamlaka kazi kuongeza nauli tu hakuna la maana wanalo fanya, hii nchi
 
Back
Top Bottom