Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Tokea kinilambe mwaka 2016’ Dom to Dar sijawahi rudia kula njiani.

Eet sum more na fanta watakayonipa nafika niendako.
Lilikukuta jambo? Pole mimi huwa naulizia kabisa kwa konda tutakula wapi?πŸ˜€ kuna siku eti asubuhi saa 5 gari ipo hotelini watu wananunua chakula, mimi nikahisi ni breakfast tu kutakua na hotel nyingine tutakula so sikununua,kumbe ndiyo imeisha hiyo hamna hotel tena aargh nililalamika sanaπŸ˜€
 
πŸ˜„ Siyo ulafi mkuu, safari ya masaa kumi na mbili kwenye basi, njaa lazima uipate tu.
Ni kweli aisee tena Sisi wa Dar Kyela ni hatari masaa 14 aku, konda akitangaza tu sasa tunaingia hotelini, nakua wa kwanza kuanza kutokaπŸ˜€πŸ˜€ sitaki vidonda vya tumbo mimi na hapo nakua nimekula Biscuits zote na kajuice nilikobebaπŸ™Œ
 
Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu, kuna mgahawa mkubwa pale , wanauza vyakula fresh na gharama zao ni za kawaida sana. Basi likisimama pale lazima ninunue nyama choma na ndizi.
wanapaita stend ya dodoma... ndo bas nying zinapopak pale zinazoend dom
 

Jipikie chakula chako kama parcel unajilia tu njiani, sio lazima kununua wanapopaki.

Pale singida au manyoni kama sikosei wana chakula lakini bei zao sio rafiki kwa mtu wa hali ya chini. Serikali inapaswa kuangalia hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…