Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Tokea kinilambe mwaka 2016’ Dom to Dar sijawahi rudia kula njiani.

Eet sum more na fanta watakayonipa nafika niendako.
Lilikukuta jambo? Pole mimi huwa naulizia kabisa kwa konda tutakula wapi?😀 kuna siku eti asubuhi saa 5 gari ipo hotelini watu wananunua chakula, mimi nikahisi ni breakfast tu kutakua na hotel nyingine tutakula so sikununua,kumbe ndiyo imeisha hiyo hamna hotel tena aargh nililalamika sana😀
 
😄 Siyo ulafi mkuu, safari ya masaa kumi na mbili kwenye basi, njaa lazima uipate tu.
Ni kweli aisee tena Sisi wa Dar Kyela ni hatari masaa 14 aku, konda akitangaza tu sasa tunaingia hotelini, nakua wa kwanza kuanza kutoka😀😀 sitaki vidonda vya tumbo mimi na hapo nakua nimekula Biscuits zote na kajuice nilikobeba🙌
 
Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu, kuna mgahawa mkubwa pale , wanauza vyakula fresh na gharama zao ni za kawaida sana. Basi likisimama pale lazima ninunue nyama choma na ndizi.
wanapaita stend ya dodoma... ndo bas nying zinapopak pale zinazoend dom
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - mwanza
• Dar - - mbeya
• Dar - - kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi walio jiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walicho nacho. Karibia vituo vyote wanavyo paki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, alafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakua watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyo ambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini


Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki

Jipikie chakula chako kama parcel unajilia tu njiani, sio lazima kununua wanapopaki.

Pale singida au manyoni kama sikosei wana chakula lakini bei zao sio rafiki kwa mtu wa hali ya chini. Serikali inapaswa kuangalia hili
 
Back
Top Bottom