Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Nakumbuka magufuli alizuia huu upuuzi akatoa order garii zote zipaki ndani ya stendi watu walenstend
 

all in all ukiona gharama kubwa kununua pika nyumbani weka kwenye hotpot more especially kama una watoto wengi alafu uwezo wako unaona hauta mudu gharama za hizo hotel.
Haya mambo ndo hayatakiwi, kwa nini mtu mmoja utese watu zaidi ya 40, Kama siyo uzembe wa Serikali/Mamlaka ni nini🤔
 
Nilinunua nyama, ilikuwa ngumu na mbaya.. nijikaza finyango kadhaa.. tumbo likaja kuniuma.

Tokea hapo hunilishi safari ya bus.. na ninafikaga niko mzima, sijawahi fika nimelegea
 
Nyumbani nakula na hicho chakula kitafanya kazi.. sasa umekaa tu napo unakula nn?
 
😍
 
Bebelea chakula kama una watoto.....wengi nhiani safari inabidi ujipange kwani hujui kuna kula ? Pika chips na nyama beba kutoka nyumbanii....
• Hapa hatuzungumzii kubeba chakula, tunazungumzia Abiria Akiwa yupo safarini, awe huru siyo ale chakula aina moja tangu asubuhi,

• Mbona mbona bei za mafuta inapanda holela lakini wananchi wanavumilia?
 
Ni kweli aisee tena Sisi wa Dar Kyela ni hatari masaa 14 aku, konda akitangaza tu sasa tunaingia hotelini, nakua wa kwanza kuanza kutoka😀😀 sitaki vidonda vya tumbo mimi na hapo nakua nimekula Biscuits zote na kajuice nilikobeba🙌
• Ndo hivyo aise, Abiria awe huru, Siyo kupelekwapelekwa kama mfungwa.

• Sasa masaa 14, utembee na hotpot 😄, mambo mengine bhana.
 
Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu, kuna mgahawa mkubwa pale , wanauza vyakula fresh na gharama zao ni za kawaida sana. Basi likisimama pale lazima ninunue nyama choma na ndizi.

• Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu

Kama ni hivyo Afadhali mkuu, Utoe nauli kubwa, kwenye Gari tena upelekeshwe 😐,
 
Nikisafiri kuelekea mbeya huwa sigusi kitu mpk tunapita iringa. Kuumwa tumbo wakati wa safari ni hatari au kabla ya kisafirinahakikisha nimepiga high dose ya metronidazole

Nikisafiri kuelekea mbeya huwa sigusi kitu mpk tunapita iringa
Kwa nini mkuu, iwe hivyo?


kabla ya kisafiri nahakikisha nimepiga high dose ya metronidazole
🤔🤔, Utapata Resistant ya metro mkuu, Siyo vizuri kutumia dawa kama hauumwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…