Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - mwanza
• Dar - - mbeya
• Dar - - kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi walio jiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walicho nacho. Karibia vituo vyote wanavyo paki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, alafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakua watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyo ambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini


Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Nakumbuka magufuli alizuia huu upuuzi akatoa order garii zote zipaki ndani ya stendi watu walenstend
 
Tanzania kila kitu ni madili madili tu kwa anayepata furusa ,hapo utakuta madereva katika hizo hotel wanalipwa mishahara,hapo ndio ule msemo kula urefu wa kamba yako unamaanisha ,all in all ukiona gharama kubwa kununua pika nyumbani weka kwenye hotpot more especially kama una watoto wengi alafu uwezo wako unaona hauta mudu gharama za hizo hotel.

all in all ukiona gharama kubwa kununua pika nyumbani weka kwenye hotpot more especially kama una watoto wengi alafu uwezo wako unaona hauta mudu gharama za hizo hotel.
Haya mambo ndo hayatakiwi, kwa nini mtu mmoja utese watu zaidi ya 40, Kama siyo uzembe wa Serikali/Mamlaka ni nini🤔
 
Lilikukuta jambo? Pole mimi huwa naulizia kabisa kwa konda tutakula wapi?😀 kuna siku eti asubuhi saa 5 gari ipo hotelini watu wananunua chakula, mimi nikahisi ni breakfast tu kutakua na hotel nyingine tutakula so sikununua,kumbe ndiyo imeisha hiyo hamna hotel tena aargh nililalamika sana😀
Nilinunua nyama, ilikuwa ngumu na mbaya.. nijikaza finyango kadhaa.. tumbo likaja kuniuma.

Tokea hapo hunilishi safari ya bus.. na ninafikaga niko mzima, sijawahi fika nimelegea
 
• Mkuu kwani safari ya Dar to Arusha, inatumia masaa mangapi?
• Je ukiwa nyumbani huwa unakaa mda gani ndo upate chakula
• Mkuu safari ya Dar to Arusha, kama umebeba watoto nao watakaa bila kula.
• Kuna hawa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, tunawasaidiaje ili wasiumwe zaidi matumbo yao?
Nyumbani nakula na hicho chakula kitafanya kazi.. sasa umekaa tu napo unakula nn?
 
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini


Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
😍
 
Bebelea chakula kama una watoto.....wengi nhiani safari inabidi ujipange kwani hujui kuna kula ? Pika chips na nyama beba kutoka nyumbanii....
• Hapa hatuzungumzii kubeba chakula, tunazungumzia Abiria Akiwa yupo safarini, awe huru siyo ale chakula aina moja tangu asubuhi,

• Mbona mbona bei za mafuta inapanda holela lakini wananchi wanavumilia?
 
Ni kweli aisee tena Sisi wa Dar Kyela ni hatari masaa 14 aku, konda akitangaza tu sasa tunaingia hotelini, nakua wa kwanza kuanza kutoka😀😀 sitaki vidonda vya tumbo mimi na hapo nakua nimekula Biscuits zote na kajuice nilikobeba🙌
• Ndo hivyo aise, Abiria awe huru, Siyo kupelekwapelekwa kama mfungwa.

• Sasa masaa 14, utembee na hotpot 😄, mambo mengine bhana.
 
Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu, kuna mgahawa mkubwa pale , wanauza vyakula fresh na gharama zao ni za kawaida sana. Basi likisimama pale lazima ninunue nyama choma na ndizi.

• Nayakubali sana mabasi yanayoelekea dodoma huwa yanapaki nje kidogo ya atendi ya msamvu

Kama ni hivyo Afadhali mkuu, Utoe nauli kubwa, kwenye Gari tena upelekeshwe 😐,
 
Nikisafiri kuelekea mbeya huwa sigusi kitu mpk tunapita iringa. Kuumwa tumbo wakati wa safari ni hatari au kabla ya kisafirinahakikisha nimepiga high dose ya metronidazole

Nikisafiri kuelekea mbeya huwa sigusi kitu mpk tunapita iringa
Kwa nini mkuu, iwe hivyo?


kabla ya kisafiri nahakikisha nimepiga high dose ya metronidazole
🤔🤔, Utapata Resistant ya metro mkuu, Siyo vizuri kutumia dawa kama hauumwi
 
Back
Top Bottom