Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Kwa nini hubebi Ugali toka huko kwenu Mbagala? Tafuta ma-hotpot ya kutosha.
Tatizo letu watanzania tymezoea shida kiasi ambacho tumeshasahau kuzitatua bali tunaongeza shida ili kupunguza shida. Hili ni tatizo la serikali kutowajibika na siyo watu kubeba ugali. Magari yanatakiwa kusimama stendi ili watu wawe na uchaguzi wa hotel.
 
Kuna kiziwa pale chalinze kati ukiwa unaenda Tanga wapo kibao tu.
Utauziwa kidari au paja unatafuna hao
Hakuna kitu kama hicho. Hakuna tai wengi kiasi hicho. Yaani uwakamate leo kesho na keshokutwa na bado wawepo tu? Ukiniambia kula vibudu naweza kukubali lakini siyo tai wala ndege mwingine. Halafu wengi hapa hamna uzoefu wa kula nyama za viumbe wa porini ndiyo maana mnasema hivyo. Nyama ya kanga tu ukiiona unajua huyu siyo kuku ije iwe tai?
 
Hivi ukichukua Karanga zile za 500 mbili...na Juice ya 3000 na Maji ya Buku..

Total 5000...mbeya hufiki!??
Kwa nini unataka kupangia watu wale nini? You are very selfish! Hivi mtu kama wewe ukipata uongozi si utakuwa hatari sana kuliko hata CCM? Kwanini kusiwe na mpango wa magari kusimama stendi kama zamani? Mbona zamani stendi kulikuwa na hotel na vyakula vizuri tu tena bei nzuri?
 
Dah niliudhika sana Ally's kutoka Dar-kwenda Mwanza...badala ya kupaki dodoma mjini kwenye hotel/migahawa mizuri .wameenda kulipaki basi karibu na bahi...vyakula vimepoa na vibaya kinoma.

Ok kutoka hapo ineenda kusimama tena nje ya mji wa Singida..chakula kibaya na bei kubwa vile vile..

wameenda kulipaki basi karibu na bahi...vyakula vimepoa na vibaya kinoma

• Unaona sasa kero hii, Vyakula haieleweki, bei juu,
• Wanafanya makusudi kwa sababu wanajua mtanunua tu.
 
Sijui wanatuchukuliaje wasafiri sababu hatuna option nyingine🤔 ila kuna siku nilienda Moshi na Kilimajaro Express sijui ni hotel yao ile atleast wanajitahidi chips safii nikashangaa maana nishazoea Mbeya kwetu mwendo mdundo chips zimepoaa 😀(sijui ni ulafi ila lazima nile njiani)
Tokea kinilambe mwaka 2016’ Dom to Dar sijawahi rudia kula njiani.

Eet sum more na fanta watakayonipa nafika niendako.
 
Na supu ya kichwa, Daah, haya maisha, niyakuacha tu. 😀
Hakuna kitu kama hicho. Hakuna tai wengi kiasi hicho. Yaani uwakamate leo kesho na keshokutwa na bado wawepo tu? Ukiniambia kula vibudu naweza kukubali lakini siyo tai wala ndege mwingine. Halafu wengi hapa hamna uzoefu wa kula nyama za viumbe wa porini ndiyo maana mnasema hivyo. Nyama ya kanga tu ukiiona unajua huyu siyo kuku ije iwe tai?
We una asili ya ubishi,kanga mi nakula fresh tu ila sio tai.
Alikua na shombo flani kumzidi bata ndo kilinishinda.
Sili hata bata mwenyewe
Hakuna kitu kama hicho. Hakuna tai wengi kiasi hicho. Yaani uwakamate leo kesho na keshokutwa na bado wawepo tu? Ukiniambia kula vibudu naweza kukubali lakini siyo tai wala ndege mwingine. Halafu wengi hapa hamna uzoefu wa kula nyama za viumbe wa porini ndiyo maana mnasema hivyo. Nyama ya kanga tu ukiiona unajua huyu siyo kuku ije iwe tai?
We ni mbishi tu.
Kanga si kuku tu nakula fresh.
We utanieleza mi kuhusu kula nyamapori huku nilikua nazurura na wawindaji mpk Swaz na Bots.
Alikua na shombo flani kumzidi bata ndo kilinishinda.
Sili hata bata mwenyewe
 
Usi complicate mambo ngoja nikupe life hacks, kuna kitu kinaitwa lunch box. Wewe kabla hujasafiri kwenda huko unakokwenda jiandalia chakula chako kifunge vizur, wakat wenzako wanasuka kwenye gari wewe ndio kwanza unatoa kuku wako unamla taratibu,

Hapo ume save cost mkuu,
• upo sahihi mkuu, je wote Abiria wafanye hivyo?
• Natujue kabisa kuna watu vyakula vya baridi hawezi kabisa kula.
 
Kutoka mwanza had dar wanakula nala pale Dodoma chai tu ya 200 inauzwa pale buku, chapati za mia tatu, pale buku

Serikali ilitizame hili suala vizur makampun yana waumiza wateja wao

Kutoka mwanza had dar wanakula nala pale Dodoma chai tu ya 200 inauzwa pale buku, chapati za mia tatu, pale buku
. Chapati ni ile ile, chai ni ile, lakini bei inakuwa tofauti, ni mambo ya ajabu sana.

. Sasa kama basi lingepaki sehemu rafiki, Abiria watakula wanachotaka na kwa bei rafiki kabisa.
 
Sawa kabisa siku tulipita chalinze pale kulia tukaona tukale kidogo maana tulitoka mtwara.
Aisee naagiza kuku kienyeji chips likaletwa bonge la paja.
Mmh kula kidogo likanishinda ladha.
Nikaja kuambiwa badae ni yale mandege Tai yana miguu mirefu hivi ndo nimeuziwa.

Aisee naagiza kuku kienyeji chips likaletwa bonge la paja

• 😄😄Dah, Litakua hilo paja halikuiva vizuri mkuu,

• Tupe na radha ya ndege Tai, anamafuta sana, au kawaida tu.
 
Beba chakula chako kutoka kwenu,
Mabasi hayawezi kupeleka watu kwa mama ntile kusiko hata na vyoo vya kujisaidia abiria.
Mabasi hayawezi kupeleka watu kwa mama ntile kusiko hata na vyoo vya kujisaidia abiria.

• Mana ntilie wanajisaidia wapi?
• Sasa huoni hapo kama kuna fursa nyingine ya ujenzi wa vyoo.
• Garama ya Choo bure, chakula 8000/- na garama ya Choo 200, chakula bei kuazia 1000/15000 - 3000, ni wapi patafaa kwa Abiria ?
 
Back
Top Bottom