MENEMENE TEKERI NA PERESI
JF-Expert Member
- Mar 11, 2022
- 5,392
- 14,646
Anhaa Nyafwili pole sana , zamani kidogo kila nikisafiri nikala vyakula njiani basi tumbo lanipa uharo .Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.
• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma
Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.
Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.
1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?
2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini
Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Basi nikaja na mbinu ya kujitengenezea kuku wangu namkaanga vizuri naweka na chipsi za kuzugia si unajua mimi ni chipsi damu damu bro basi nikipanda gari nikipewa ile take away safari yangu inakuwa imeisha .
Kwa hii njia niling'oa mademu wengi maana unakuta nasubiri warejee kutoka huko wanakouziwa uchafu kwa gharama wanakula wanamaliza , kila mtu ananikaribisha mimi ni mwendo wa ahsante wanahisi nina shida kweli kweli .
Sasa dakika kumi mbele wao wanakuwa ombaomba kwangu maana navitoa vipande vyangu vyote vya kwio kwio naanza kula kwa madaha basi kwakuwa mimi kwenye basi ni mwiko kukaa na mwanaume mwenzangu ni hapo utaanza kushangaa mara jirani nionjeshe basi maana sinaga neno karibu kwenye jasho langu .
Akikaribia kaumia , maana mtongozo uanzia hapo anapohisi kuku wameisha namsubilia wakati wa kigiza ndiyo namtoa mwingine wakati ambao dereva amepambisha moto basi ni mwendo wa kulishana vidali vya kuku mpaka nafika nakuwa mwenye maamzi ni mimi twende lodge au nimuache aende mtoto wa watu .[emoji848]
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app